Barua ya wazi kwa Mzee Jakaya Mrisho Kikwete: Hivi wakati unaweka ndani Masheikh wetu ulikuwa unafikiria nini?

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,526
2,000
Kilichofanyika USA kwa kuwapeleka Guantanamo washukiwa wa ugaidi wa Alqaeda ni sawa na kilichowaleta Tanzania bara washukiwa wa ugaidi wa Uamsho. Mahakama ya Tanzania haina jurisdiction kwenye makosa yanayofanyika ardhi ya ZNZ kwa kuwa ZNZ ina Mahakama yake.

Mahakama ya Rufaa pekee ndiyo suala la Muungano.
Waliletwa kinyume cha sheria, wakashikiliwa kinyume cha sheria, na wameachiwa bila ushahidi wowote wa kuwatia hatiani.
Tunajua vizuri kuwa ishu ya Masheikh wa uamsho ni vuguvugu lao la kutaka zanzibar yenye mamlaka kamili na wala siyo Ugaidi.
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,526
2,000
Siku moja ukiwa Rais ndiyo utajua...
Nadhani unafahamu vizuri kuwa suala la kubambikizia watu kesi lipo, hata Samia amewahi kulizungumzia hilo.

Kwa hiyo kwa mujibu wa mwenendo wa kesi za hawa masheikh, ambao ushahidi dhidi yao haujapatikana mpaka leo ikiwa ni mwaka wa nane ni dhahiri wamebambikiziwa kesi
 
Majulao

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
409
500
Huyu Jamaa aliyeleta huu Uzi anatakiwa awekwe ndani kwa uchochezi wa kufukua makaburi. Wenyewe wamekaa kimya maana wanajua walikosa, wewe eti inakuja kukuuma leo! Kwa hiyo unataka kusema kuwa walikamatwa bila kosa? Tuanzie hapo. Halafu ukiitwa utoe ushahidi uko tayari?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,133
2,000
..ukimya wa Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuhusu suala la Mashekhe wa Answar Sunna unahuzunisha.

..Hivi nikisema Watanzania tuna uwezo mkubwa wa kuvumilia dhuluma na ukatili wa watawala wetu nitakuwa nimekosea?
 
Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,856
2,000
Mzee Jakaya!

Shikamoo mzee, nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Naomba nikupe taarifa tu kuwa jela kuna Masheikh zaidi ya 150 , na wengi wao waliwekwa ndani kipindi cha utawala wako. Hivi mzee ulikuwa unafikiria nini kwa mambo haya?
Hapa unapoteza muda. Hata akikwambia itakusaidia nini wakati si rais tena?
 
mbongo_halisi

JF-Expert Member
Apr 16, 2010
5,542
2,000
Nakumbuka Mzee Mohamed Said aliwahi kueleza namna sheikh Ponda na wenzake walivyozunguka nchi hii kumpigania JK mwaka 2010........hii nchi dini na siasa zimejaa wasanii.
Binadamu ubadilika, kwani Sheikh Ponda unafikiri hana matamanio? Mbona kuna Waislam wengi tu wanamponda Sheikh Ponda sembuse JK, gaidi ni gaidi tu.
 
ras jeff kapita

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
12,634
2,000
Mzee Jakaya!

Shikamoo mzee, nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Naomba nikupe taarifa tu kuwa jela kuna Masheikh zaidi ya 150 , na wengi wao waliwekwa ndani kipindi cha utawala wako. Hivi mzee ulikuwa unafikiria nini kwa mambo haya?
Sasa hv unaandika kwa amani kabisa huku umechanua miguu....

Kwa sababu ya amani iliyopo!!?
 
kipuyo

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
1,710
2,000
Naona wachangiaji wanaconclude kuwa Masheikh ni Magaidi lakini leo wako ndani mwaka wa 8 na hakuna Ushahidi ulioletwa mahakamani wa kuwatia hatiani.

Hii precedence ya kukubali tu baadhi ya watu kumbikiziwa kesi za Ugaidi, kuwanyanyasa bila ushahidi wa uhusika wao, kamwe haitoishia kwa hawa waislamu, Wapo watu watakuja kubambikiziwa kesi za hivihivi na tutakosa moral authority ya kuwatetea kwa sababu zamani tulishaunga mkono raia wengine kubambikiziwa kesi za aina hii kwa sababu tu ya hisia za Udini wetu.

Leo tutanzaje kuwatetea akina Adamoo, wakati at the same time tunaunga mkono wengine kuwekwa ndani bila ushahidi wa ugaidi?
Hivi unajua kuwa kama baadhi ya hao jamaa wasingewekwa ndani upande wa Pwani wote ungekuwa na makundi kama yale ya Somalia na yale ya Msumbiji?
Hata kama tunapenda dini tusitumie kichaka hicho kutenda uhalifu.
Hebu tuwe wakweli na tuipende nchi yetu.
Haki itendeke
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,526
2,000
..ukimya wa Waislamu na Watanzania kwa ujumla kuhusu suala la Mashekhe wa Answar Sunna unahuzunisha.

..Hivi nikisema Watanzania tuna uwezo mkubwa wa kuvumilia dhuluma na ukatili wa watawala wetu nitakuwa nimekosea?
Huu Ukimya wa Waislamu ni juhudi za makusudi na mkakati maalum wa System wa kuwanyamazisha ili waufyate kwa sababu by nature waislamu siyo watu wa kukaa kimya hasa kwenye mambo ya maslahi ya dini yao. Nadhani unakumbuka vizuri harakati za waislamu kipindi cha Mwinyi na Mkapa

Kwa hiyo part ya mkakati wa kuwanyamazisha waislamu "wasisumbuesumbue" watawala ni kuwakamata masheikh ambao wana misimamo na influential ambao hawajatoe a line ya wstawala kisha kuwabambikizia kesi za ugaidi na kuwaweka ndani ili kuwatisha waislamu wengine kuwa na nyie mkisimama na kuleta mambomambo yenu tunawapa kesi za ugaidi!

Kibaya zaidi power struggles baina ya waislamu wenyewe kwa wenyewe serikali inaside na BAKWATA kwa kuwakamata masheikh wanaopinga mambo ya BAKWATA na kuwapa kesi kama hizi ili kufuta nguvu za upinzani dhidi ya BAKWATA. Lengo ni kuisimika BAKWATA kama chombo kikuu cha waislamu nchini kwa kuwa ni chombo cha System na wanaweza kukicontrol watakavyo. Kwa hiyo watawala ili waweze kuwatawala waislamu vizuri hawataki rabsharabsha zao, ndiyo maana ya juhudi hizi za kusilence masheikh wao na eventually kusilence waislamu nchi nzima.

System iliinfiltrate misikiti kibao nchini kwa kusimika masheikh wa mrengo wao, nadhani unakumbuka mambo ya mapinduzi na kuchapana bakora msikitini ili kuondoa uongozi fulani wa msikiti na kuweka mwingine katika miaka ya 2000, ile yote ilikuwa kazi ya systme na Everist Chahali ndoye aliyetoboa siri hiyo, akasema kuwa walifanya hayo mambo wakati akiwa bado kitengo
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
110,290
2,000
Bwana "Kombora la Taifa" labda nikwambie tu, kuna wakati mambo ya Dola na usalama wa nchi huwa ni magumu sana kuyaletea ushabiki.

Wangekuwa ni viongozi wa CDM tungesema. JK ni CCM anakandamiza CDM, wangekuwa ni wakristo tungesema JK Muislamu anakandamiza Ukristo, wale ni masheikh wa kiislam na JK ni muislam naamini lipo jambo ambalo kuna wakati raia hatupaswi kuhoji bali kuamini tu Dola inatenda sawa kutulinda..

Wale wahuni wa mkulanga, Tanga na kule kibiti wengine informers wao na supplier + coordinators wao tulikuwa tunaishi nao mtaani kuwatarget na kuwatia mkononi ni kazi ya Dola kimyakimya.

Si ajabu leo hii ukiwekewa hadharani ya bwana mabunduki pale french embassy unaweza kustaajabu lakini inabaki kuwa taarifa za dola.

Kupatikana kwa Osama Bin laden na kuuwawa kulitokana na taarifa kutoka kwa mtoto mchunga kondoo kule tora bora wakati tena mambo yameshapoa. U-smart wa akili wa wale USA uliwafanya kutomdharau yule dogo na baadaye kuishia kumtesa guatanamo kupata proper lead.
Guantanamo ndiyo jela anayo stahili kufungiwa Makonda na Sabaya
 
Iboya2021

JF-Expert Member
Dec 1, 2020
1,628

ndiyo maana baada ya hao mashehe kukamatwa zanzibar ikatulia tindikali ikamaliza kazi ya kutesa watu bado tu hupati jibu basi utakuwa mbishi tu
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
110,290
2,000
Linapokuja suala kama hili wengi hapa JF huwa hawako sympathetic na Waislamu, sijui kwa nini!

Huwezi kuona hoja za Ulinzi na usalama zikiapply kwa kesi ya Mbowe, huwa tunaconclude kuwa Mbowe kaonewa. Ila kwa Masheikh huwa tunasema serikali "inalinda" nchi dhidi ya ugaidi
Umetumwa na ZZK tunakujua wewe
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom