Nimefurahishwa na utendaji wa ofisi ya Msajili wa NGO chini ya wizara ya Dorothy Gwajima. Tatizo lipo kwenye ngazi ya mtaa na kata

Tozo

Member
Aug 23, 2021
76
154
Niseme wazi mimi huwa ni mlalamikaji pindi nikihudumiwa sivyo. Lakini Kwa hili napenda niipongeze wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu chini ya mwanamama mhe. Dkt Dorothy Gwajima.

Nimehudumiwa vizuri pasipo urasimu wowote mpaka kufanikisha usajili wa shirika lisilo la kiserikali (NGO) kwa njia ya mtandao.

Naweza kusema nilicheleweshwa na ngazi ya wilaya, kata na mtaa,lakini ilipofika ngazi ya taifa huduma zilienda kisayansi zaidi.

Unatuma document zinasomwa na baadae wanakupa marekebisho ya kufanya, ukikamilisha unahamia hatua nyingine.

Mwisho wanakwambia njoo uchukue cheti chako cha usajoli. Hakika mama huyu kumbe siyo umahili wa kuongea tu hata vitendo ni mchapakazi mzuri katika kusimamaia watendaji wa wizara yake. Hongereni sana wizara hususani ofisi ya msajili wa NGO kwa kazi nzuri.

Kule kwenye kata na mtaa ndipo Kuna shida. Kukuandikia barua tU ya utambulisho wanakwambia kamati ikae, maana yake uwalipe posho wajumbe qa kamati ya mtaa. Ikifika ngazi ya kata unaambiwa hivyo hivyo. Wizara iangalie namna bora ya kuondoa dosari hii.

Kule nhazi ya wilaya haina shida kwani wizara tayari imeweka mratibu wao kusimamia mchakato wa usajili.
 
Mtaa na kata mara nyingi hawajui hayo mambo .... oh mpaka utoe darasa mkuu. Mtendaji wa mikocheni aliomba mpaka katiba yangu na lunch juu
 
Mimi waliniambia niwalipe wajumbe 10 posho ya sh. 30,000 kila mmoja. Wanijadili nilipokataa. Na kwenda kumuuliza Mkugenzi wa Manispaa kama hup ni utaratibu. Akampigia simu mwenyeliti wa mtaa apitishe hiyo barua. Wakati wa kupitisha akaandika mtaa wake una NGO nyingi hawezi kuzihudumia NGO hizo, eti nitafute mtaa mwingine. Nilipomuuliza hizo NGO zilizopo unazihudumia kivipi? Akasema si unajifanya mjanja tafuta mtaa mwingine.
 
Idara nyingi zilizo chini ya Waziri Dorothy Gwajima zipo smart. Huyu mama mkwara wake siyo wa mameno tu.
 
Mimi waliniambia niwalipe wajumbe 10 posho ya sh. 30,000 kila mmoja. Wanijadili nilipokataa. Na kwenda kumuuliza Mkugenzi wa Manispaa kama hup ni utaratibu. Akampigia simu mwenyeliti wa mtaa apitishe hiyo barua. Wakati wa kupitisha akaandika mtaa wake una NGO nyingi hawezi kuzihudumia NGO hizo, eti nitafute mtaa mwingine. Nilipomuuliza hizo NGO zilizopo unazihudumia kivipi? Akasema si unajifanya mjanja tafuta mtaa mwingine.
Achana nae huyo we tafuta mtaa mwingine . Kwani ofisi si huwa zinahama mkuu. Yaani unaweza kutoka manzese ukaenda kufungua ofsi ubungo.
 
Niseme wazi mimi huwa ni mlalamikaji pindi nikihudumiwa sivyo. Lakini Kwa hili napenda niipongeze wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu chini ya mwanamama mhe. Dkt Dorothy Gwajima.

Nimehudumiwa vizuri pasipo urasimu wowote mpaka kufanikisha usajili wa shirika lisilo la kiserikali (NGO) kwa njia ya mtandao.

Naweza kusema nilicheleweshwa na ngazi ya wilaya, kata na mtaa,lakini ilipofika ngazi ya taifa huduma zilienda kisayansi zaidi.

Unatuma document zinasomwa na baadae wanakupa marekebisho ya kufanya, ukikamilisha unahamia hatua nyingine.

Mwisho wanakwambia njoo uchukue cheti chako cha usajoli. Hakika mama huyu kumbe siyo umahili wa kuongea tu hata vitendo ni mchapakazi mzuri katika kusimamaia watendaji wa wizara yake. Hongereni sana wizara hususani ofisi ya msajili wa NGO kwa kazi nzuri.

Kule kwenye kata na mtaa ndipo Kuna shida. Kukuandikia barua tU ya utambulisho wanakwambia kamati ikae, maana yake uwalipe posho wajumbe qa kamati ya mtaa. Ikifika ngazi ya kata unaambiwa hivyo hivyo. Wizara iangalie namna bora ya kuondoa dosari hii.

Kule nhazi ya wilaya haina shida kwani wizara tayari imeweka mratibu wao kusimamia mchakato wa usajili.
Aisee yaani ndio nimetoka kutifuana na hawa maafisa wa kijiji na kata, nasema ujinga ni kitu mbaya mno! nina miezi mitatu bado nipo katika level ya kata na wilaya. Mwanzoni niliambiwa hivyo hivyo eti kila mjumbe 10,000/= na wapo 12, lakini nilikuja kuwapa 10,000 tu kwa kuwahadaa tu wakiwa na mtendaji na wajumbe kama watatu tu lakini ni baada ya kuwasiliana na kiongozi wa juu kidogo.

Sasa shida ni site verification: anakuja binti afisa maendeleo wa kata anakataa ofisi bila vigezo vya msingi na hata ukimwambia basi kuna ofisi nyingine pale nayo ya kwangu anasema nitakuja wiki ijayo. Hawa wanatafuta safari ili walipwe posho ya siku.

Huko wilayani nayo haijawa rahisi, maafisa hawajui ni nini hasa kinapaswa kuwepo ili mtu asajili NGO, huyu atakuambia hiki mwingine kile ni shida tupu. Maafisa wengi ni wajinga mno, sikupata kufikiri, kiburi na kujifanya ujuajij huku ni watupu.

Kama huko taifani mambo ni shwari nafarijika sana. Siku zote watu wajinga ni hatari kwa maendeleo na wanoko wakubwa!

Mtu unahitaji kuwa mpole sana ili ufanikiwe hasa kama hutoi rushwa.
 
Back
Top Bottom