Barua ya Lema kutoka Gerezani Arusha

Barua ya Lema kutoka Gerezani Arusha

Mahanisi siku hizi wana watoto?

Matusi ya nini? Huyo jamaa yenu anataka kutuletea balaa. Hivi vinchi vya afrika vikitikingishwa kidogo tu kutulia inakuwa noma. Sasa huyo anaona kifo cha mkuu wa nchi kama suala la utani utani tu

Subiri asomeshwe huko
 
Mkuu vijana wa geto pale ufipa hawataki kukubali kua huyo kibaka kafanya kosa la uhaini,atoe ushahidi mahakamani kama kweli aliota,watu wanafanya mchezo na matishio ya kuangamiza,kule marekani wakat Mashambulizi ya Trade center yanapangwa yalickika maneno ya kawaida yakapuuzwa na yaliyotokea mpaka leo yamekua historia sasa mtu akurupuke kaota Rais atakufa alaf apuuzwe akiuawa mtajibu nini mliopewa dhamana yakumlinda Acheni kulialia anachopata kinamstahili na natamani angekua Rwanda

Aote mtu asiote mtu immanuel akimwita kamwita tu
 
najaribu kufikiria ni jinsi gani watu watakavyofurika kwenye mkutano atakaoufanya Lema mara tu,atakavyotoka Gerezani
 
Barua zote 11 mtume Paul aliandika akiwa gerezani mapaka leo ndo masomo yanayo somwa sana makanisani. Na ndo mafundisho waliyofundishwa wakristo
Basi Lema asililie Kutoka Kisongo ili awe kama My. Paulo yaani awazidi Mandela na Steve Biko na Patrice Lumumba
 
Binadamu wote tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hata tukiwa madarakani au wakuu kiasi gani
Jibu Maswali, hakuna mtu aliyesema ataishi milele. Yani ufanye ujinga uachwe kisa eti kila mtu atakufa, nini maana ya kuwepo vyombo kama mahakama na vyombo vingine vya kusimamia sheria.
 
Nchi yangu Tanzania! Waliokamatwa na mabunduki 17 kwa uwindaji haramu wa tembo (uhujumu uchumi) wamepata damana ndani ya siku 3 alieota na kusema ameota nini ananyimwa damana!!!......kisa? Kumpendezesha aliewateua!! Katiba katiba katiba......! Ikulu ni mahala patakatifu..msipigane ndani ya ikulu ni mwiko na laana........
Nnaona umesahau na fujo aliyomfanyia mkuu wa mkoa alipokuwa anahutubia pia usisahau na matusi aliyomfundisha mkewe kumtukana mkuu wa mkoa kwa simu pia usisahau mengine mengi ambayo mimi na wewe hatuyajuwi.

Tukumbuke tu, kuwa upinzani si kuwa hodari wa matusi.
 
Amkeni jamani . ..tuiheshimu serikali iliyoko madarakani ili tupate baraka kutoka kwa MAULANA MOLA WETU RHABUKA
 
Hebu andika hilo tusi alilotukana.
Akiandika atakuwa ametukana yeye kwa kulikariri hilo tusi.
Kilichomfanya Lema aozee jela kinafahamika, ni ile hotuba yake ya ndoto na humu ilizagaa. Fuatilia utaipata, lkn kukariri tusi ni kitukana pia.
 
Matusi hayana dhamana?? Sheria lazima ifuatwe usitishie hata majaji na mahakimu kisa wewe ni mfalme na hujaribiwi!! Mfalme huwa hapigi pigi mke wake hadi kuzimia! Tena ikulu! Busara busara busara
Nnaona umesahau na fujo aliyomfanyia mkuu wa mkoa alipokuwa anahutubia pia usisahau na matusi aliyomfundisha mkewe kumtukana mkuu wa mkoa kwa simu pia usisahau mengine mengi ambayo mimi na wewe hatuyajuwi.

Tukumbuke tu, kuwa upinzani si kuwa hodari wa matusi.
 
Matusi hayana dhamana?? Sheria lazima ifuatwe usitishie hata majaji na mahakimu kisa wewe ni mfalme na hujaribiwi!! Mfalme huwa hapigi pigi mke wake hadi kuzimia! Tena ikulu! Busara busara busara

Wacha porojo, tuwekee mashtaka yake hapa si kutowa vitu kichwani mwako.
 
Lema ana akili sana kuliko wanavyo mdhania. Hakika hii barua mtakuja kushangaa baadae ni moja ya mambo yatakayo tumika kutambulisha harakati za Lema maishani mwake. Hata wakina Mandela barua zao wakiwa jela zimewaongezea umaarufu sana kwenye maisha yao ingawa ni za kawaida tuu.
Kuna tofauti kati ya barua iliyo andikwa na mtu akiwa hospitalini na yule aliyeko jela kwa sababu za kisiasa
Naona umeamua kujipafaraja kuwa Lema ni Mandela 😀😀😀
 
Back
Top Bottom