Barua ya kipuuzi kwa media

Barua ya kipuuzi kwa media

dazipozi

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
1,137
Reaction score
106
Nauchukia mziki wa bongo, nachukia media nyingi za bongo. Maswali mengi yatajijenga vichwani mwenu, kujiuliza kwanini nimeamua kuandika waraka huu kwenu; Mapresenter njaa. Labda nianze na hadithi fupi. Nilipoanza mziki mwaka 2009, sikuwa na wazo la kufanya mziki ili uwe kama biashara kwangu. Lakini kwa wale waliosomea biashara wataelewa “kiasi ambacho unawekeza, ndio mori inapozidi kupanda. Hamu y...a kutamani biashara yako izidi kukuwa” hivyo ndivyo ilivyokuwa kwangu na mwenzangu Jafaryzo Baizo wakati tunaanza mziki tulichukulia kama ni jambo la kujiburudisha. Baada ya kufanya baadhi ya ngoma hata wazazi wakaturuhusu, wakathubutu; kutupa pesa ndogo ya kuingia studio, ikaongeza tamaa yetu ya kufanya vitu vikubwa zaidi ili tuweze kujitangaza. Sisi ni wanafunzi, Lakini tulijinyima tukafanya bonge moja ya video kutoka Kwetu studio. Nadiriki kusema ni kwa gharama zetu, kuanzia pesa tuliyomlipa Mussah, modals tuliowaleta. tulitoa mifukoni mwetu. Ni kiasi kikubwa tuliwekeza bila jasho na msaada kutoka kwa mtu yeyote. Siwezi kusema ni kiasi gani tulilipa lakini ni gharama kubwa kwetu. Nashukuru Mungu video ilitoka kwa wakati, hakukutokea tatizo la aina yeyote. Sasa dhumuni la barua hii, ni hapa. Tukiwa na video mkononi, Huku tukiwa na uhakika wa kufanya Interview, kama sio airtime ya kutosha katika station moja kubwa ya Tv. Tuliahidiwa na marafiki ambao si vyema nikawataja. Ambao wapo katika hiyo station. Nikisema marafiki ni marafiki wanaonifahamu vizuri na mimi ninawafahamu. Si urafiki ambao umeanza baada ya hizi kazi za muziki. Lakini cha kushangaza hakuna kitu, tumeambulia patupu. Amani sana kwa Tony Tbway Escaber kwa moyo wa huruma na uthubutu na wa kirafiki uliotufanyia japo kwa matatizo kidogo ya kiufundi ilisababisha video kutokwenda hewani. Huwa najiuliza zile video za kina P-square, STL, Keko, P-Unit na wale wengine wanaokuja kutuchukulia mamilioni ya pesa katika show kama Rick rossT/Sh Milioni 220, Ludacris na wengineo wengi hivi huwa wanalipia hizo mnazoziita promotion? Kwanini hamna huruma? Kwanini hamjiulizi mara mbili underground kama mimi, nimekufuata unipigie video yangu, niliyojinyima kula chipsi shuleni nikala sambusa; nimekufuata kwa ndala na suruali nyeusi iliyobadilika rangi matakoni na kuwa nyeupe, nitapata wapi laki moja au mbili ya kukupa ili uicheze video yangu? Nimetoa labda laki moja studio kutengeneza audio, nikatoa laki saba kutengeneza video, bado kuna hela za kuburn cd, Dv, hata nauli pia….. sisi tuna kazi gani ya kupata hizo pesa? Ukikaa kwenye station tv za siku hizi video za kibongo hupigwa mara chache sana tofauti na za huko ghaibuni. Napenda nifahamu jamani hao pia wanatoa hizo pesa za promotion? Kama ni za wabongo utaona za Yule Yule msanii mmoja, video mbili ambazo ni nyimbo mbili tofauti. Inaniuma sana nikiona mnatukandamiza halafu mnasema underground wanasumbua sana. Hivi mmesahau kabla hujapata huo upresenter ulikuwa mtaani? Umeisahau ile njaa iliyotafuna utumbo wako hata ukadiriki kusema maisha ni magumu? Ukajaribu kuongea ongea kuangalia kama sauti yako inafaa kuwa mtangazaji? Japo ulisomea udaktari wa mifugo? Kiukweli inabidi tubadilike watanzania. Tuthamini kwanza vya kwetu ili na sisi tukapige show kubwa tukachota madolari nchini kwao. Tusiishie kupiga katika birthday party za pedeshee mmoja huko ughaibuni.Mx
 
Kama kuna mwenye kuwajua hao wahusika tafadhalini waambieni wasome andiko aliloandika dazipozi hapo juu. Nimesoma habari hii kwa masikitiko makubwa. Ningetamani kama kuna blog ya tv station husika habari hii iwekwe humo ili wajirekebishe. Pole sana!
 
Last edited by a moderator:
Dogo jipe moyo uongeze juhudi ipo siku watakutafuta kwa udi na uvumba
 
dazipozi mdogo wa lazima una majungu. majina ya wahusika huwataji na hata hiyo stesheni hutaji that means hutuamini kuwa tunaweza tukawakemea?, hapa ni uwazi mtupu we ungewataja tuwajue ili walau tukupe hata historia zao uwajua, lakini unatia majonzi na hako kamwandiko ulikoandika nako kadogo basi shida tu. ila kumbuuka kipaji haking'ang'anizwi mchek dogo janja alivyotolewa na yule presda wa manzese, bi cheka na temba so ka una kipaji utakuja wika, shida ya mayanki wa siku hizi kila mtu akiwa na jins akavaa mlegezo nae anajiita msanii, we tunga li songi lako kali wala hutabaniwa na litarushwa ila tunyimbo twenu huto hadi ukapambwe na shooting ndo kanoge?
 
Hebu angalieni na nyimbo mnazoimba! Unajua nowa days mnaimba tu ilimradi!!,mbona nyimbo za hapo nyuma zilibamba bila video!! Pole kwa usumbufu unaopata!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom