Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Yes 50/50

TZS will receive Corporate tax, SDL + Royalty + Management fees + Dividend = Barrick receipt of Management fees + Dividend.

They will only fix us on loan from Barrick since interest is not a distribution of profit.
Afadhali wewe unajaribu kutoa maelezo kuliko wale nyumbu wenye kubisha tu kama vile ni Simba vs Yanga!
 
Bila mkataba kuwekwa hadharani ufafanuzi wa kuungaunga hautasaidia kupata majibu sahihi katika hili ,miaka mingi baadaye tutaelewa hesabu hii ngeni ni ya kweli au si ya kweli
 
Afadhali wewe unajaribu kutoa maelezo kuliko wale nyumbu wenye kubisha tu kama vile ni Simba vs Yanga!
Kama unongea na kujibizana na nyumbu bila shaka na wewe utakuwa nyumbu. Tujifunze kujadiliana kwa staha
 
Mmmh haipo hivyo na kunamabadiliko ya mrabaha toka 2017

Hisa 16% (Free share) dhamana ni Ardhi na madini
Tozo zingine zipo kama kawaida bila kuangalia ni serikali au Barrick, maana hapo ni Twiga Kampuni, Mrabaha (Royalty) ni 6% na Inspection fee 1% ya Mauzo ghafi (Hizi zitatolewa kwenye gharama za uendeshaji)
Hii 30% Corporate ni pale mtaji utapokuwa umerudishwa (breakeven) ndo hapo pakujiuliza Accacia ilishaanza kulipa sasa je, itaanza upya au wataendelea? Ndo wataalam watudadavulie

Mkuu ukisoma vyema michango ya watu tunahatua walao kidogo, ila naona bado tunatawaliwa na mikataba ya kina karl peters na wenzake, ukiangalia aina ya mikataba ambayo tunaingia bado haiaksi uhalisia,

16% iwe ya ardhi na madini, halafu
84% iwe ya mitambo na kusimamia
Kwel kabisa inaingia akilini? Hiv kati ya ardhi(madini) na hyo mitambo ya mwekezaji ipi inathamani? Nan atapata hasara ikiwa mwingine hayupo? Kwa ufahan wangu, madini na ardhi haviishi thamani, ila hyo mitambo inaisha thamani..


Tufanye sisi hatuna uelewa wa madini, hatuna skills za kutosha, je kunahaja gani ya kuyachimba? Maana kuyaacha na kuyachimba kwa kumiliki 16% free share haiondoi matatzo tulio nayo..

Kunamdau hum kasema walao kwa sasa hyo 16% inaonekana,!!!!!!!! Sawa inaonekana je italeta matokeo kwenye jamii? Bado nilitamani nione si tu kunamwanga walao tungesogea 40% ingeeleweka..

Nataka kuamini kuwa hii mikataba ni ya karl peters, ila inakuja tu kwa chupa tofauti, inapaswa kama tunaona hatuna uwezo wa kusimamia tuache kuchimba tusomeshe watu wetu kisha tuweke oda ya kuinfrastructure sis wenyewe kwenye masini, tunashindwa nini? Tunawatu zaidi ya 50+ kwel tumekosa mtu wa maono?

Kama tunanunua ndege je hyo miuondombinu inaghalim kiasi gani ambapo kama taifa tukiamua kujinyima tutashindwa kwa manufaa ya vizazi vijavyo?

Au ndo ule usemi kuwa IN GOLD WE TRUST unachukuwa nafasi yake?

Tuwapongeze ila bado walao tufike 40% kwa migodi yetu yote hapo tutazungumza lugha moja...
B
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie

Ninavyoelewa ni kwamba mgawanyo wa faida unatokana na kiasi cha hisa
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Kama faida ni 50/50, hiyo 84/16 ina maana gani.
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie

Hawa watu hawako wazihata siku moja. Wanajitahidi kuwadanganya watu na kufanya vitu kisiasa.

NB:
Husitegemee jino lenye afya kwenye kinywa kilichooza
 
Umejitahidi kueleza vizuri na kistaarabu kuliko wale waimba mapambio na kuabudu wanaoishi kuporomosha matusi. Kwa vile bado makinikia yataendelea kupelekwa nje tusitegemee makubwa. Pia tusijitangazie ushindi dhidi ya acacia kwani ni walewale ila wamebadili majina na maelezo kutuweka sawa
Kwa ujumla, maadui ni sisi wenyewe, kwa ujuha wetu!
 
Tumeambiwa kuwa serikali inamiliki hisa 16 na mabeberu watamiliki hisa 84 lakini wakasema faida itakuwa 50/50! Kama ni hivyo kwa nini na hisa zisiwe 50/50? Nahisi kuna kitu hakiko wazi naomba kama kuna mtu mwenye ufafanuzi wa hili anisaidie
Ni hivi, kama wana hisa, ni hivyo - 84/16 tofauti na awali ambazo zilikuwa 100/0! Sasa unapokuja kwenye mgao wa faida baada ya biashara kufanyika, ni 50/50. Yaani kwenye FAIDA mgao ni sawa. Wakati huo mmeshagawana faida kutokana na shares. Kwa vyovyote vile, Barrick watapata zaidi kutokana na hiyo 84/16 kwa ajili ya uwekezaji, uendeshaji na usimamizi. Karibu lete hoja!
 
Sijawahi Kumuelewa Profesa Kabudi na tokea aseme mwenyewe kuwa aliokotwa Jalalani basi nikimwona anazungumza huwa naliona Jalala tu na siyo Maelezo yake. Huku mnasema hisa zao ni 84% na Sisi Watanzania zetu ni 16% halafu hapo hapo tena mnasema kuwa Faida tutagawana pasu kwa pasu. Hivi hii inaingia Akilini Kweli? Acheni kutufanya Watanzania wote labda ni ' Mapopoma ' kama mlivyo baadhi yenu. Mleta Mada ( Uzi ) yupo sahihi, namuunga Mkono na ana Hoja Kubwa, ya maana na ya msingi kabisa.
Hoja ipi au hiyo ya Kabudi, Gentamycine?
 
Mantiki haikubali, inawezekanaje hisa ziwe 16% halafu faida tugawane sawa na yule mwenye hisa nyingi za 84%. Tunaaminishwa kitu ambacho akili ya kawaida na hata hata kwenye ibiashara haiko hivyo.

Vv
 
Kampuni ya Twiga Minerals Company Limited ni alama ya ushindi kwa Rais wetu John Pombe Magufuli katika vita ya kiuchumi dhidi ya Mabeberu.

Na; Fahami Matsawili.

Miaka miwili iliyopita Rais wetu John Pombe Magufuli alitangaza vita ya kiuchumi ya kulinda rasilimali za Watanzania dhidi ya Mabeberu wa ndani na nje ya nchi yetu.

Alianza kwa kuzuia Makinikia ya mchanga bandarini ili kujua kinachosafirishwa ndani kina uhalisia na makubaliano ya mikataba yetu na Malipo kwa Taifa, akaunda Tume 2 za Madini kuchunguza, mwisho akapeleka mswaada wa Sheria 2 za Madini na rasilimali za Taifa bungeni kwa hati ya dharura....

Kama kawaida yao Mabeberu wakawatumia Zitto na Tundu lissu kupiga kelele ili kuupotosha Umma wa Watanzania kwa Hatua alizokuwa anachukua Rais wetu John Pombe Magufuli dhidi ya Mabeberu hawa ona sasa Leo wameufyata hawa watu hatuna budi kuwatangaza kama maadui wakubwa wa Taifa letu na Watanzania.

Leo hii tunayo Sheria ya Madini ambayo imezaa matunda ya kampuni ya Twiga Minerals Company Limited baada ya serikali na Kampuni ya Barrick kukubaliana hivyo hii ni kampuni itakayosimamia Migodi 3 Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu Migodi hii ilikuwa chini ya usimamizi wa kampuni ya Acacia kabla ya kufutwa na Hisa zake kununuliwa na Barrick sasa imezaliwa rasmi kampuni ya Twiga minerals company limited kampuni ambayo serikali ya Tanzania itamiliki Asilimia 16% na kampuni ya Barrick Asilimia 84%....

Mwaka jana, Bunge lilipitisha sheria mbili za madini ambazo pamoja na mambo mengine, zinaipa Serikali umiliki wa asilimia 16% kwenye kila mgodi uliopo au utakaoanzishwa nchini.

lengo la Sheria hii ni kuona Watanzania wananufaika na rasilimari zao na kuona Sekta ya Madini inatoa mchango unaostahili katika pato la Taifa kutoka asilimia 4.8 iliyopo hadi asilimia 10% kama Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano unavyosema.

Sheria mpya ya madini ya mwaka 2017 inakwenda kurudisha uchumi kwa Mwananchi wa Tanzania,

“Sheria mpya ya madini ya mwaka 2017 inataka kurudisha uchumi wa madini kuwa uchumi fungamanishi kwa sekta nyingine. Tulikuwa na Migodi ndani ya nchi ambayo ajira zote na Teknolojia zinapelekwa nje ya nchi kupitia huduma mbalimbali....

Sasa Sheria ya Madini no 5 ya mwaka 2017 ijulikanayo kama The written laws (Miscellaneous Amendments) Act 2017 iliyoanza kutumika 7/7/2017 Sheria hii imeleta mapinduzi katika sekta ya Madini ambapo Sasa

1. Malipo ya Mrabaha yatapanda kutoka Asilimia 4% hadi 6% kwa Madini ya Metali (dhahabu, shaba, fedha)

2. Kuongezeka kwa Malipo ya Mrabaha kutoka Asilimia 5% hadi 6% kwa Madini ya Vito (Tanzanite, Rubby, n.k)

3. Madini yatakaguliwa na kuthaminishwa nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi kwa gharama ya Asilimia 1% ya thamani ya Madini hayo (Clearing fees)

4. Mchimbaji mdogo anayeuza Madini kwa broker au kwa Dealer atakatwa Asilimia 5% ya thamani ya Madini kama withholding tax...

5. Sheria hizi zinatoa fursa kwa serikali kupitia upya mikataba yote ya madini na kutilia mkazo kwa kampuni shughuli za uchakataji madini kufanyika nchini.....

6. Sheria hizi pia zimebainisha wazi kwamba rasilimali madini ni mali ya taifa yatasimamiwa na serikali kwa niaba ya Wananchi, kinyume na ilivyokuwa hapo awali ambapo hakuna sheria iliyokuwa imeweka wazi umiliki wa Madini kwa Taifa...

Sheria Mpya ya Madini pia imetungiwa kanuni na wizara kanuni hizi mpya ambazo, zinatoa kipaumbele si tu kwa taasisi za fedha na huduma za kisheria za Kitanzania lakini pia ajira kwa Watanzania....

7. Kuhusiana na huduma za kifedha, kanuni mpya zinataka makampuni ya madini kufungua akaunti na kuweka fedha zao katika benki za wazawa.

"Benki ya wazawa ni ile inayomilikuwa na wazawa kwa asilimia 100 ama ile ambayo Watanzania wanamiliki hisa nyingi zaidi", mfano CRDB, NMB, DCB, POSTA BANK, n.k

Hii inaziengua benki kadhaa za kigeni kufanya biashara katika sekta ya madini. Baadhi ya benki za kigeni zinazofanya kazi nchini ni pamoja na Stanbic, Barclays, Standard Chartered na ile ya Afrika Kusini ya First National Bank (FNB), KCB n.k

8. Kanuni zinataka pia utoaji wa leseni za uchimbaji madini utoe kipaumbele kwa kampuni za kizawa....

9. Kanuni za Sheria mpya ya Madini zinaelekeza kuwa huduma za chakula na Ulinzi kwa mgodi wowote zinapaswa kutolewa na Watanzania kwa Asilimia 100% na hili wanufaika wakubwa ni sisi Vijana wa kitanzania kanuni inasema itakapobidi kampuni ya kigeni inaweza kutoa huduma hizo lakini ni lazima iingie ubia na Mtanzania....

10. Kanuni mpya pia zinataka, mwenye leseni anapaswa kuwasilisha mpango wake wa utoaji huduma kwa jamii (CSR) kwenye Halmashauri husika ili iuthibitishe mpango huo kabla ya Utekelezaji wake. Tofauti na huko nyuma Utaratibu uliokuwepo wa kampuni ya Madini inajifungia ofisini yenyewe, inakuja na mpango wa kuwajengea shule pasipo Serikali ya kijiji au Wilaya kujua huo utaratibu mfu umefutwa na kanuni hii...

11. Kanuni zinaelekeza kuwepo ajira za staha kwenye Migodi (Decent work) wanufaika wakubwa na hili ni Vijana, pamoja na faida nyingine nyingi zaidi zilizomo kwenye Sheria mpya ya Madini na kanuni zake hizi ni sehemu tu ya faida zilizomo ndani....

Vijana wa Tanzania tuna kila sababu ya kujivunia Rais wetu John Pombe Magufuli kwa namna ambavyo sisi wenyewe tutakuwa wanufaika wa juhudi anazozifanya na vizazi vyetu vijavyo, tuendelee kumuombea Mwenyezi Mungu ampe nguvu Zaidi ili akamilishe Maono yake ya Kuijenga Tanzania Mpya....

Fahami Matsawili.
Mjumbe Wa Baraza kuu Uvccm Taifa.
IMG-20191023-WA0003.jpeg
FB_IMG_1571778437740.jpeg
 
Faida ni nini..Ukishajua utajua maana ya kumiliki hisa...Tufanye wewe ndio mwekezaji je utakubali kugawana faida 50/50 bila kutoa garama za uendeshaji.
 
Hiyo 50/50 ni zile kodi,tozo mbalimbali,CSR etc ndiyo hiyo 50/50.Na bado pia itapata stahiki za 16% kutoka kwa Twiga.

Haiwezekani.

Hamuwezi kugawana faida 50/50 halafu juu ya hapo ukapewa dividends za 16%, utakuwa umetengeneza pesa kuliko mwenye biashara.

16% ni sehemu ya 50 yenu.
 
Ndio maana nikaomba misaada kwa mwenye ufafanuzi kama hujui sio ujinga ukikaa kimya
Kama ulikuwa unaomba msaada wa ufafanuzi maana yake huelewi, sasa kwanini una assert kuwa tumeuziwa mbuzi kwenye gunia? That is a logical fallacy. Ilibidi uombe ufafanuzi, na baada ya ufafanuzi huo, uwe kwenye nafasi ya kusema kuwa tumeuziwa mbuzi kwenye gunia au la!
 
Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa Serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Minerals Corporation.

Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.

======

Baada ya mgogoro uliodumu kwa takribani miaka miwili tangu mwaka 2017, Kampuni ya Barrick na Serikali zimeunda kampuni ya Twiga itakayosimamia migodi mitatu iliyokuwa chini ya kampuni ya Acacia.

Kwenye kampuni hiyo mpya, Barrick itamiliki asilimia 84 ya hisa zote huku Serikali ikiwa na asilimia 16. Utaratibu huo ni utekelezaji wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ‘sasa amezaliwa mtoto mpya baada ya Barrick kukubali kumuua mtoto wake, Acacia.’

Mgogoro kati ya Serikali na kampuni ya Acacia iliyokuwa inasimamia migodi ya Buzwagi, North Mara na Bulanhulu ulianza mwaka 2017 na Rais John Magufuli akaunda tume ya kuchunguza mwenendo wa biashara ya madini.

Tume hiyo ilibaini ukiukwaji wa sheria, utaratibu na kanuni zilizopo hivyo kuikosesha Serikali mapato inayostahili. Kutokana na hilo, Serikali iliipiga faini ya Dola 190 bilioni jambo lililosababisha kuanza kwa mzungumzo baina ya pande hizo mbili.

Bado undani wa makubaliano/mkataba huo haujawekwa wazi hadi Mwanasheria Mkuu wa Serikali apitie mkataba wa makubaliano hadi ifikapo mwezi ujao (Novemba 2019).
Serikali wameshirikiana na Barick. This is end of story
 
Back
Top Bottom