Barrick na Tanzania waunda Kampuni ya ubia iitwayo Twiga Minerals na Serikali itamiliki asilimia 16

Mzee Wa Kale Kabisa

JF-Expert Member
Mar 25, 2018
2,471
2,000
Wewe ndiyo huelewi kabisa!

16% siyo mrabaha bali ni free carried share. Kabla ya hapo tulikuwa na 10% free carried share. Kwa hiyo imeongezeka 6%. Ila kiuhalisia, iwe 10 au 16%, hakuna chochote cha maana. Ungekuwa na uelewa kidogo wa mining industry ningekuelewesha kwa nini nasema hivyo.

Kwa upande wa mrabaha, wakati wa Mkapa tulikuwa na 3%. Wakati wa Kikwete ilipngezwa na kuwa 4%. Sasa tuna 6%. Kwa hiyo imeongezeka 2%.

Kiuhalisia, kwa vurugu zote tulizozifanya kwenye sekta ya madini, tulichokipata kikubwa ni 2% royalty, nothing else.
Elezea tu Mkuu... Tutaokota hata kidogo
 
Mzee Mukaruka

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
713
500
Kama ulikuwa unaomba msaada wa ufafanuzi maana yake huelewi, sasa kwanini una assert kuwa tumeuziwa mbuzi kwenye gunia? That is a logical fallacy. Ilibidi uombe ufafanuzi, na baada ya ufafanuzi huo, uwe kwenye nafasi ya kusema kuwa tumeuziwa mbuzi kwenye gunia au la!
Na baada ya kupewa ufafanuzi anayo nafasi ya kuuliza pale ambapo hakuelewa. Lakini badala ya kufanya hayo anakuja na preconceived conclusions kuwa tumeibiwa mara tumeuziwa sijui mbuzi, sijui kondoo kwenye sijui gunia, sijui ndoo, basi shida moja kwa mbili!
 
NorthJuu

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
396
500
Waziri wa Mambo ya Nje, Prof Palamagamba Kabudi ametangaza leo kuwa Serikali kwa kushirikiana na Barrick Gold Corporation wameunda kampuni ya ubia inayoitwa Twiga Minerals Corporation.

Katika kampuni hiyo Serikali ina hisa asilimia 16 na Barrick asilimia 84.

======

Baada ya mgogoro uliodumu kwa takribani miaka miwili tangu mwaka 2017, Kampuni ya Barrick na Serikali zimeunda kampuni ya Twiga itakayosimamia migodi mitatu iliyokuwa chini ya kampuni ya Acacia.

Kwenye kampuni hiyo mpya, Barrick itamiliki asilimia 84 ya hisa zote huku Serikali ikiwa na asilimia 16. Utaratibu huo ni utekelezaji wa sheria mpya ya madini iliyopitishwa mwaka 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Profesa Palamagamba Kabudi amesema ‘sasa amezaliwa mtoto mpya baada ya Barrick kukubali kumuua mtoto wake, Acacia.’

Mgogoro kati ya Serikali na kampuni ya Acacia iliyokuwa inasimamia migodi ya Buzwagi, North Mara na Bulanhulu ulianza mwaka 2017 na Rais John Magufuli akaunda tume ya kuchunguza mwenendo wa biashara ya madini.

Tume hiyo ilibaini ukiukwaji wa sheria, utaratibu na kanuni zilizopo hivyo kuikosesha Serikali mapato inayostahili. Kutokana na hilo, Serikali iliipiga faini ya Dola 190 bilioni jambo lililosababisha kuanza kwa mzungumzo baina ya pande hizo mbili.

Bado undani wa makubaliano/mkataba huo haujawekwa wazi hadi Mwanasheria Mkuu wa Serikali apitie mkataba wa makubaliano hadi ifikapo mwezi ujao (Novemba 2019).
Wahasibu na wadau wote wa mahesabu, kama kuna closing stock, opening stock na annual dividend, dividend per share, mmoja anamiliki 84% shares, mwingine 16% shares, ni dhahiri kwenye (dividend) hapo ndiyo kuachana kama mbingu na ardhi, hakuna cha "win win situation". Niambie ni mazingira gani wanakula 50/50. Mbuzi mwenye kamba ndefu ndiye ana chance ya kula majani mengi zaidi.
 
The Elephant

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
4,347
2,000
Ongezea na 1% inspection fee (kama madini watayasafrisha nje). Kwa ujumla
1. Royalities = 6%
2. Corporate tax 30%
3. Inspction fee 1%
TOTAL CONTRIBUTION = 37%. Ambapo ktk ubia GOT inachangia "LAND" wakt wao watachangia " TECHNOLOGY na MACHINE/TOOLS.
Hizo corporate tax weka pembeni kwanza kwa sababu inategemea NET Profit, akipata hasara hauna chako hapo uhakika ni asilimia 7 tu
 
toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,848
2,000
Wewe ndiyo huelewi kabisa!

16% siyo mrabaha bali ni free carried share. Kabla ya hapo tulikuwa na 10% free carried share. Kwa hiyo imeongezeka 6%. Ila kiuhalisia, iwe 10 au 16%, hakuna chochote cha maana. Ungekuwa na uelewa kidogo wa mining industry ningekuelewesha kwa nini nasema hivyo.

Kwa upande wa mrabaha, wakati wa Mkapa tulikuwa na 3%. Wakati wa Kikwete ilipngezwa na kuwa 4%. Sasa tuna 6%. Kwa hiyo imeongezeka 2%.

Kiuhalisia, kwa vurugu zote tulizozifanya kwenye sekta ya madini, tulichokipata kikubwa ni 2% royalty, nothing else.
Bora tungekosa tu duuuh 2%
 
toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
3,848
2,000
Yaani uwe na share 16% mwenzako awe na 84 halafu utudanganye ni 50 kwa 50 haiwezekani
 
BUBERWA D.

JF-Expert Member
Apr 22, 2011
2,294
2,000
Na baada ya kupewa ufafanuzi anayo nafasi ya kuuliza pale ambapo hakuelewa. Lakini badala ya kufanya hayo anakuja na preconceived conclusions kuwa tumeibiwa mara tumeuziwa sijui mbuzi, sijui kondoo kwenye sijui gunia, sijui ndoo, basi shida moja kwa mbili!
Hawa ni mzigo kwa Taifa.
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,058
2,000
Waziri husika yuko wapi hapa,mbona wa Mambo nje ?
nani anamuwakilisha raisi katika Mikataba ya madini ikiwa kampuni imesajiliwa ndani ya nchi?
Kulikoni?
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,058
2,000
Wewe ndiyo huelewi kabisa!

16% siyo mrabaha bali ni free carried share. Kabla ya hapo tulikuwa na 10% free carried share. Kwa hiyo imeongezeka 6%. Ila kiuhalisia, iwe 10 au 16%, hakuna chochote cha maana. Ungekuwa na uelewa kidogo wa mining industry ningekuelewesha kwa nini nasema hivyo.

Kwa upande wa mrabaha, wakati wa Mkapa tulikuwa na 3%. Wakati wa Kikwete ilipngezwa na kuwa 4%. Sasa tuna 6%. Kwa hiyo imeongezeka 2%.

Kiuhalisia, kwa vurugu zote tulizozifanya kwenye sekta ya madini, tulichokipata kikubwa ni 2% royalty, nothing else.
WACHA MAYAHUDI WALE VYAO,
MADHALI BADO WAJINGA TUNGALIPO .
AFRIKA SHAMBA LAO.
MUNGU SI MJINGA KUFANYA PUNDA MILIA WENGI BILA MAKUCHA,
NA SIMBA WACHACHE WENYE MAKUCHA NA NGUVU.
WANAKULA WAPENDAPO,JAPO KWA MIKIKI KIDOGO,LAKINI WAO NDO WAFALME WA MWITUNI.
Sisi tukijengewa daraja Baharini,na Uwanja wa Mpira mzuri,na majumba mawili marefu pale Posta inatosha.
Hizo $300 milioni zitaisaidia CCM kwenye uchaguzi 2020 kuwapa raia ili wawape kura,kwisha tutapigiwa vinanda vya mapambio nakuusifu utawala uliopo,maisha yanaendelea,Huku raia wakiendelea kusaga rumba.

NATAMANI ZANZIBAR TUCHIMBE MAFUTA NA GESI ILI NASISI TUTAZAME KAMA TUTAPATA ANGALAU MKIA WA MBUZI KAMA RAIA WA QUWAIT? MAANA SISI TUKO KIDOGO.Raia wote ni 1.5M rahisi sana kugawana hizo $300m kama zingekuwa zetu kila raia angelipata $200 angaalu.
 
Mzee Mukaruka

JF-Expert Member
Jun 18, 2012
713
500
Yaani uwe na share 16% mwenzako awe na 84 halafu utudanganye ni 50 kwa 50 haiwezekani
Nadhani kuna ulazima wa shule juu ya suala la HISA na KUGAWANA FAIDA. Wale wenye uelewa wa masuala haya njooni muokoe jahazi jamani. Kwani wakizidi kusema wale wale itaonekana kama tuna itetea serikali na haya mapatano adhimu iliyoafikiana na Barrick. Jamani saidieni kwenye hili, hata kama ni kutoa ufafanuzi kwa mifano ya umiliki wa HISA hapo Dar-e-s-Salaam Stock Exchange!
 
ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,957
2,000
Nini maana ya ubia kama anayelipa kodi zote ni mmoja?
Ubia maana ya ni mgawanyo wa faida baada ya kodi yaani gawio. Fahamu kuwa kampuni ni kama mtu anayejitegemea. Wenye hisa wanaweka pesa kwake ili azizalishe kwa hiyo hata serikali ikinunua hisa ni lzm iweke pesa. Hapo itaweka 16% ya jumla ya mtaji watakaokubaliana na kutakuwa mjumbe wa serikali kwenye bodi ya hiyo kampuni. Kampuni ikipata faida na kulipa kodi zote albaki inagawanywa serikali 16% na Barrick 84%. Mrabaha ni sehe
 
Katavi yetu

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,205
2,000
Vipi kuhusu kinu cha kuchenjulia makinikia kinajengwa au hakijengwi?

Kabla ya sheria mpya serikali ilikua na hisa asilimia ngapi,mrabaha na kodi ilikua inapata asilimia ngapi?
 
McCarthy

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
507
1,000
Tueleze wewe unayejua kuliko sisi
You've hot no entitlement to command me, bro. Will you pay for the costs of my counsel and consultancy fee? Hapa mjini kila wazo lenye utaalamu ndani yake halitoki bure kwenda kwa mwingine.
 
Katavi yetu

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
1,205
2,000
Serikali imejipanga vipi kuwezesha makampuni ya ndani ambayo ni ya wazawa ili yaweze kutake over hizi oppottunities
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
6,382
2,000
You've hot no entitlement to command me, bro. Will you pay for the costs of my counsel and consultancy fee? Hapa mjini kila wazo lenye utaalamu ndani yake halitoki bure kwenda kwa mwingine.
sorry ms flatterer
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom