Baraza la Sanaa Zanzibar (BASSF) lasitisha shughuli za muziki na burudani kipindi cha Ramadhani

Baraza la Sanaa Zanzibar (BASSF) lasitisha shughuli za muziki na burudani kipindi cha Ramadhani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu Zanzibar limetoa taarifa Kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani linawakumbusha wamiliki wa maeneo ya kumbi za starehe na Burudani, wapigaji wa muziki na Wananchi wote kwa ujumla kwamba Shughuli za upigaji wa muziki kwa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani zinasitishwa ili kuweza kuweka utulivu zaidi wa Ibada katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Soma > Kamisheni ya Utalii Zanzibar: Nguo fupi marufuku kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani

SnapInsta.to_631884840_18053807672694777_7784687508773099861_n.jpg
 
Ujuaji wa Nyerere wa kuaminisha kuwa yeye ndio anajua kila kitu kuliko wengine ndio unaleta hii shida.

Kivitendo Zanzibar ni dola ya kiislamu.
Ukiwa Zanzibar kuuishi uislamu ni jambo la lazima, na sio jambo la kubembelezana tena.
Na ndio mana Ukikutwa unakula chakula hadharani kipindi cha ramadhani lazima ukalale selo.

Kwanini Zanzibar ilizuiliwa na Nyerere kujiunga na O.I.C
 
Zanzibar ni nchi ya kiislam, na miaka hii akina nyerere hawapo imekuwa ikijinasibu kwa uislam bila kificho. Kutwa rais wa zanzibar yupo misikitini na gazeti lao la zanzibar leo linajaza picha kubwa ukurasa wa mbele mwinyi akiwa msikitini akifanya siasa huko! Ni aibu sehemu hiyo ya tanzania kujinasibu kwa uislam huku katiba ya nchi haijaweka wazi kuwa nchi inaongozwa kwa dini ya kiislam
 
Nani wa kukemea udini unaomea na kukua zanzibar? Hii haikubaliki, nchi si jamhuri ya kiislam, haiwezi kukataza watu wasifanye shughuli zao kisa tu mwezi wa ramadhan ambao ni imani tu kama kuamini mawe na masanamu. Huwezi kulazimisha watu kuamini unachoamini, kuabudu unachoabudu. Imani ni suala binafsi aonavyo mtu nafsini mwake. Kitendo cha kuzuia watu wengine wasioamini na kuabudu uislam hakikubaliki
 
Back
Top Bottom