Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

Mkuu Mchambuzi, I hope huta mind, nimemkaribisha rasmi JK katika uzi huu pia nimeuweka ule uzi wako tangulizi.

Baadhi ya hoja zako nitakujibu.
Pasco.

Hakuna tatizo mkuu Pasco, in JamiiForums, "we dare to speak openly."

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Eeeeh mungu tunakuomba uinusuru Tanzania kwa kutokua na viongozi bora zaidi ya yote wamekuwa na ubinafsi na kunijari wenyewe tunajua ya kwamba wewe mungu ni mwenye huruma ila tunapo kukosea unatuadhibu.mawazili walio fanya makisa na wengine kupokea maisha ya watu kuwafukuza au kuwavua madaraka nitofauti sana na ukumu stahiki ambayo walitakiwa wapate ilikutupa nguvu n Imani na utawala huu ambao umekua ni wakibinafsi sana katika kuyatenda yale tunayo yahitaj sisi watanzania..
 
Pasco, na Ruge tena?
Mkuu Swiper, don't under estimate the power of youth!, huyu dogo ndio the brain behind Clouds Media success, imewashika vijama!. Ungeijua ile kampeni ya "Tanzania Tanzania" "Penda Chako, Jenga Kwako" aliohamasisha watu kupenda bidhaa za Tanzania hadi kuweka banda la Tanzania kwenye DITF ya mwaka huu!. Sasa yuko na kampeni ya "Changamkia Fursa!". Chama chochote kinachojipanga kuitawala Tanzania 2015 lazima kiivest on youth!. Huyu ni master mind wa youth mobilization tangu "malaria haikubaliki!", "Tanzania bila Ukimwi inawezekana" etc, japo radio yao inaonekana kama haina maana kwa sababu inaendeshwa bila maadili ya utangazaji, hicho wanachokifanya ndicho vijana wanachokitaka na wamewashika vijana!, 2015 vijana ndio mpango mzima!. Nawashangaa sana jamaa zangu wanamuundia zengwe kijana mwenzao!.
Pasco.
 
liwalo na liwe, naona JK ataamua kumpatia waziri Magufuli uwaziri mkuu ili aifikishe serikali ya ccm 2015. Ataamua kumpatia magufuli kazi hiyo na kumpa nguvu zaidi za kuisimamia serikali. Miaka hiyo miwili itashuhudia ccm kurejesha imani kwa wananchi
 
Wana JF

Naomba mawazo yangu ninayotoa hapa yatafakariwe kwa kina.

Kutokana na visasi na mizigo inavyojionesha katika baraza la mawaziri la sasa namuomba Rais wetu Jakaya Kikwete afanye mabadiliko ya kihistoria mabadiliko ambayo yatamuweka yeye binafsi na serikali yake salama. Imedhihirisha sasa kwamba vyovyote vile Rais hawezi kupata baraza zuri na lenye tija ndani ya CCM peke yake. Kwa sasa hivi kuna vita, minyukano fitina na ghiriba ndani ya CCM.

Sasa hivi mitaani kuna baadhi ya mawaziri na wabunge wamekula mbuzi na bia wakifurahia kujiuzuru kwa Kagasheki. Ukiwasikilza hoja zao ni za ajabu. Mara wasema Kagasheki amewabania vitalu mara jamaaa ana nyodo na mengine mengi hasa wanaojihusisha na nyara za serikali.

Ushauri

Iandikwe historia sasa kwamba tupate mawaziri kutoka vyama vya CCM, CHADEMA, NCCR MAGEUZI, TLP na CUF ili kuepusha labsha na fitina ambazo zinajionyesha ndani ya serikali ya CCM ambazo hazimsaidii mwananchi wa nchi hii.BILA kuandika historia mpya baraza lolote litakaloundwa ndani ya CCM linaweza kuwa baya zaidi kuliko hata la sasa hivi lililopo. Nawasilisha
 
Sioni chama legele kinachoongozwana rais dhaifu na dhalimu pamoja na wabunge wasiojitanbua kama wana weledi wo wote wa kuongoza taifa.

1. Wameondoa mfumo wa serikali ili wao wawe serikali wakati hawana hata mshipa mmoja wa fahamu wa kuendesha serikali. Wamefanya hivyo kwa kukwapua madaraka ya utendaji wa serikali. Wamefanya hivyo kwa teuzi za kishkaji na kisiasa kwenye utendaji wa kitaalamu

2. Wamekiuka haki za kibinadamu (mikono inanuka damu kuanzia JK) kwa kutisha na sasa wajaribu kukalia/kufunika kashfa zisijitokeze.

3. Mawazo yamekuwa mgando ndiyo sababu ya ngonjera zisizo na utekelezaji

4. Bado wanaamini utendaji wa mtu ndani ya utendaji wa mfumo badala ya utendaji wa mfumo ulio na checks and balances

Nitakuwa mtu wa mwisho kukubaliana na mambo ya kuteua watu katika serikali isiyo na utendaji wa kiserikali. Mfano ni rais kuteua watu waliotufikisha hapa kwenye kukiuka haki za msingi za binadamu. Kwangu mimi naamini ana nafasi ya maamuzi mazuri zaidi kupita haya kwa kusimamia Katiba Mpya ambayo ni wazi iko inaelekea down the hill.
 
Umezingatia dini ktk baraza lako ?

Maana humu jf ikionekana dini fulani imepewa cheo kuna vijimaneno vinavyosemwa ...

Nadhani hapo kigezo cha dini hujazingati... Haya tubalancie basi ili watu wa kanisa wafurahi kuwa umeweka usawa maana wakristo hawapendi kuona waislam wakipendelewa wala wakristo wakipendelewa ....
 
Mwigulu Nchemba apewe Wizara ya Elimu- Huyu jamaa amesoma hapa hapa nchini Tanzania kutoka shule ya msingi hadi chuo kikuu tena katika shule za wananchi, hivyo atakuwa msaada kubwa sana katika kutatua matatizo yanayoikabili shule zetu za wananchi (st kayumba)

Stephen Masele(Naibu waziri wa Nishati na Madini anayeshugulikia madini)- apewe wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia aungane na January Makamba katika kuinua sekta hii. Masele ameonyesha uwezo mkubwa katika sekta ya madini hasa katika kuwabana wawekezaji katika sekta kulipa kodi zote stahili katika sekta hii. Kiingia katika wizara hii atahakikisha makampuni ya simu hayakwepi kodi hivyo kuiongezea mapato serikali.
 
Kuimarisha Wizara Ya Maliasili Na Utalii Ange Waweka Wale Miamba Watatu Wa Siasa Za Chama Cha Mapinduzi, Mpina Kama Waziri, Deo Naibu Waziri Utalii Na Ligola Naibu Waziri Maliasili. Kwenye Elimu Kuna Kijana Pale Udsm Anaitwa JOHN ANDONGWISYE, Yuko Vizuri Sana Anauwezo Na Uchungu Kwa Elimu Yetu, Amekwenda Sweaden Kwa Masomo!
 
Kuna tetezi zinaenea kwa kasi ya ajabu hapa mjini kuwa cc ya CCM inampigia Chupuo comrade@mwigulu nchemba awe waziri wa mambo ya ndani kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Nchimbi , je nini maoni yako??
Kuandamana kutaendelea kuwepo ??? mwigulu.JPG
 
Wanabodi,

Baada ya mawaziri wanne kung'oka hii leo, na ile mizigo kutuliwa rasmi, Jee kwenye baraza jipya la mawaziri, nani wengine watapumzishwa na sura mpya zipi zitaingizwa na kwa nini?!.

Watakaipumzishwa ukiachilia wale mizigo, ni pamoja na
  1. Waziri wa Madini-Sababu hawaelewani na nanii!.
  2. Taja wengine....
Watakaobaki ni pamoja na
  1. Waziri wa Tamisemi, -kwa sababu maalum!. (atamhamishia kule!)
  2. Taja wengine waliopaswa kupumshishwa lakini watabakizwa kwa sababu zipi?!.

Promosheni toka naibu nito full
  1. Jan Makamba
  2. Aggrey Mwanri

Na Sura Mpya ni pamoja na
  1. EL, sababu anahitajika sana sasa more than anytime else!
  2. Dr. Asha Rose Migiro-Anaadaliwa ku lobby kura za wanawake!.

Tayari nayajua baadhi ya majina, ila siyataji ili nisiwatibulie.

Pasco.
Imput from Mchambuzi, ikumbukwe hii mada originally ilianzishwa na Mchambuzi hapa [h=1]Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?[/h]
Mkuu Mchambuzi, ingekuwa kuna watu wanaostahili kulipwa kwa michango iliokwenda shule, wewe ni mmoja wao.

Haswa upande wa reasoning power. Hilo la Kilango sikulikumbuka ni kweli kuna watu watachaguliwa kwa sababu tuu ya ku balance uwiano wa uwakilishi. Hili la Deo, Kangi na Zambi wanaweza kuletwa ili tuu kuwa contain!.
Mwanri-atabaki sio kwa sababu ya uwezo wa kutenda bali kusema!. Tamisemi inahitaji watendaji na sio wasemaji!.
-Makamba junior - ndio nyota ing'aayo, ndio kijana wa "king maker" na ndiye yule jamaa yangu anamfagilia njia!. Tatizo la kijana ni dini!, soon mtamshuhudia akimsindikiza mama yake kanisani!, mama Jan ni Mkatoliki!, hivyo atapelekwa MFA kuing'arisha zaidi nyota yake ila pia nakubaliana na wewe anaweza pandishwa pale pale alipo sasa kuwa waziri kamili au kuwa waziri kamili ila mambo ya ndani hapana, hii ni wizara ya muungano, mawaziri lazima wapishane bara na Zanzibar kama ulinzi, kwa vile alianza Zanzibar ndipo akaja bara, this time ni Zanzabar mambo ya ndani, halafu bara Ulinzi, hapa anaweza kuletwa Suluhu au Mbarawa!.
- Ulinzi na JKT kutokana na hali tete ya Ziwa Nyasa na ile "coalition of the willing!", Ulinzi ataleta mjeshi kama Kangi!.
-Membe atang'olewa kutoka wizara ya mambo ya nje ni ili kumzuia asioteshwe ile ndoto, na hawezi kumpeleka fedha huko kutakuwa ni kumuongezea nguvu!.
-Migiro ameletwa strategically just to loo kura za wanawake 2015, she is never a performer, hivyo atapelekwa wanawake na watoto!.
-Muhongo ataondolewa kabisa sambamba na Mgimwa!- Viwanda na Biashara atampa Lazaro, au atampeleka Utalii ili wife pia asaidie kupepesha bendera yetu!
-Dalali Peter Kafumu - Nishati na Madini nakubaliana na wewe.
-Engineer Stella Manyanya atatolewa ukuu wa mkoa na kupewa wizara hii pia ni posible!.
-Anna Kilango atapewa unaibu waziri - mkoa wa kilimanjaro umeishiwa wabunge (ccm) wa kupewa uwaziri kwani chami, magembe, mathayo wameshachafuka; Kilango ataungana na Mwanri kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro kwenye cabine, hii nakukubalia 100% kwa 100% na sababu nyingine pia ni CCM kuendelea ku hold the little grip ya Kaskazini vinginevyo CCM inasafishwa yote!. Hata Ole Medeye atang'olewa na EL anaweza kurudishwa kuwapooza morani!.
-Mwigulu Nchemba atatolewa Lumumba na kupewa unaibu waziri, pengine fedha hili nakubaliana na wewe, ila sio fedha!. Kwa vile fedha ni wizara ya Muungano, ili Mwigulu awe naibu, minister lazima atoke Zanzibar!. Kwa hali ilivyo sasa, we can't trust any Zanzibari na fedha zetu hivyo naibu lazima atoke Zanzibar hivyo aliyepo kuiendelea!.
-Gaudence Kayombo (Mbinga) ataletwa kwenye unaibu kuziba pengo la Nchimbi kama mwakilishi wa wanaruvuma;janista mhagama pia anaweza teuliwa badala ya kayombo iwapo ana degree; wanaweza kuteuliwa wote, Jeanistar ana kadrigrii zile za mchoro mchoro kama Ph.D ya Mama Nagu!, ila hata bila digrii ya ukweli, she is very capable ukiondoa tatizo dogo la mkorogo kama Mwanjelwa na Mlata!.
-Amos Makala - waziri kamili nakubaliana na wewe.
-Makongoro Mahanga - waziri kamili sina uhakika sana maana namuona kama hana any impact!.
-Dr. Ndungulile - Naibu Waziri nakubaliana na wewe, hiki kijamaa ni smart, ila poa kuingingia kifua CCM ndidhi ya nguvu ya CUF kipande ile!.
-Prof Mwandosya - Iwapo afya yake imeimarika, atapewa wizara kamili, hasa wizara ya Maji (haijatengemaa kihivyo)
-Prof Mwandosya asiporudi kwenye wizara kamili, Prof Mwakusya atarudishwa kwenye cabinet-nakubaliana na wewe hii ni possible!.
-Prof Msola - hawezi kurudishwa!, alishakuwepo na kuboronga fulani, Sayansi ikiwa na Elimu ya Juu!. ila pia imethibitika maprofesa ni bure kabisa!. Sarungi wa good akiwa Muhimbili, alipopewa wizara alishindwa!.
wana Iringa wataletewa kijana Deo kama mwakilishi wao kwenye cabinet na sio kurusha makapi ya zamani!.
Haka kakijana ka Dewji kama katakubali, kanaweza kupewa unaubu Viwanda na biashara ila kako tuu buzy!.
Sikumbuki nafasi za rais za uteuzi wa wabunge zimebaki ngapi anaweza kuchukua young blood kama kale ka Jerry au hata Ruge!.
Pasco.


Sioni jipya zaidi ya recycleling!

Hivi tunategemea matokeo tofauti wakati tunarudisha viongozi walewale?

Mie nasubiri 2015,kwa huyu rais aliyepo sitegemei lolote jipya.

I'm very disappointed with him!Its like he totaly a failure!
 
Back
Top Bottom