Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

Lowassa ndiye anafaa kuwa PM. Salama ya JK ni kumrudisha Lowassa kwenye hiyo nafasi.
 
Mwigulu akiwa Waziri Mambo ya Ndani CHADEMA wasahau mikutano ya hadhara na maanadamano virungu kwa sana.
 
hoja sio balance ya wabunge kutokana na "ukabila wao" bali balance ya wabunge kwenye cabinet kutokana na wabunge waliopigiwa "kura" katika sehemu mbalimbali za nchi;

January Makamba ile issue ya kuongoza kampeni ya kupinga kodi ya simu haiwezi kumgharimu?Nimemuona Saleh Pamba anachangia juzi na leo jamaa yupo smart nadhani atakuwepo kwenye cabinet ukizingatia alishawahi kuwa kamishna,
Tatizo cabinet limebadilishwa sana wengi ni backbenchers nadhani kuna uwezekano wa wazee kurudi
 
Hawa nao ni mizigo, Muhongo anajitahidi kutudanganya watanzania lakini ukweli ni kwamba Tanzania bado iko kwenye mgao wa umeme alafu yeye anatuletea personal conflicts zake na Mengi. Hawa wengine matatizo yao mnayajua.

Nawakilisha

Mawaziri wa Elimu na Mawaziri Michezo Nao wafukuzwe kwani utendaji wao umedorora
 
Duh hongera sana CCM yaani mpaka tusiowajua watakua mawaziri?????!!! Mwisho atawekwa hata mwanafamilia
 
 
Nimeshindwa kumwelewa mleta mada! Pengine anamatatizo binafsi.Hata chekechea angeandika vizuri kuliko wewe.Nakama ndivyo wazari kaandika basi hata yeye anamapungufu makubwa,japo hakufanya hivyo unavyo mwakilisha.Think before you write often
 
==> Ur totally sick....hysteria...plus illiteracy.....u don*t deserve even div..V...

=> Scented words...



 
Mkuu Mchambuzi, I hope huta mind, nimemkaribisha rasmi JK katika uzi huu pia nimeuweka ule uzi wako tangulizi.

Baadhi ya hoja zako nitakujibu.
Pasco.
 

mkuu PASCO, kuunda serikali hakuhitaji mambo mengi kama unavyo fikiri! kinachotakiwa ni kuwa na mkakati na nia thabiti ya kuleta maendeleo.kazi ya chama kinacho shinda uchaguzi na kushika dola ni kuisimamia serkali kikamilifu.wafanyakazi serikalini wapo tena wenye maarifa ya kutosha.kinacho kosekana ni usimamizi ili walete TIJA.siku hizi mfanyakazi serikalini hata afanye kosa gani hawezi kufukuzwa kazi labda auwe! jiulize hapo kweli kuna serikali?

siku hizi unaweza kukuta kijana amehitimu chuo kikuu hajui kuandika barua ya kikazi! nini maana yake? Ni kwamba elimu haina usimamizi wa karibu kinacho takiwa ni kuwawajibisha wanaosimamia wamezembea somewhere,hawatakiwi kuonewa huruma hao.kazi ya chama dola ni kuchukua hatua na kuigiza serikali nini cha kufanya.

For your information, Michael satta amechukua serikali wakati chama chake kina umri usio zidi miaka kumi katika siasa,mbona anaiweza Zambia na walau sasa wanaanza kupata political and economical stability.husikii tena bei ya mkate inapanda hovyo! sembuse CHADEMA kina miaka karibu ishirini kwenye active politics tena wana viongozi na makada walio onesha kuwa uwezo wanao.

Mwalimu aliunda serikali akiwa na graduates wachache sana.karibu viongozi wote walikuwa darasa la tano au kidato cha nne lakini aliweza kujenga serikali yenye mwelekeo.wananchi waliiheshimu kwasababu mwalimu aliisimamia serikali yake kikamilifu.kwahiyo kinachotakiwa ni kuwa na mission na vision halafu usimamizi imara.hakuna chama kinacho ingia madarakani kikabadili wafanyakazi wote. wanaoingia ni political administrators basi.wengine watabaki walewale isipo kuwa namna ya kuwasimamia.

PASCO,Tambua kuwa hakuna mahali kwa kufanya mazoezi jinsi ya kushika dola na kufanya tathimini kama mnaweza.indicator kwamba hiki ni chama makini ni jinsi walivyo weza kujijenga na kuwa taasisi inayo aminika ndani na nje ya nchi.kuna vyama vingi tu hapa nchini hata havijulikani kama vipo pamoja na kuwa vina usajili wa kudumu.CHADEMA ya MBOWE,DR SLAA,TUNDU LISSU,MNYIKA,SAUTI YA RADI,MSIGWA,nk mimi nina imani nao sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…