Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

hoja sio balance ya wabunge kutokana na "ukabila wao" bali balance ya wabunge kwenye cabinet kutokana na wabunge waliopigiwa "kura" katika sehemu mbalimbali za nchi;

January Makamba ile issue ya kuongoza kampeni ya kupinga kodi ya simu haiwezi kumgharimu?Nimemuona Saleh Pamba anachangia juzi na leo jamaa yupo smart nadhani atakuwepo kwenye cabinet ukizingatia alishawahi kuwa kamishna,
Tatizo cabinet limebadilishwa sana wengi ni backbenchers nadhani kuna uwezekano wa wazee kurudi
 
Hawa nao ni mizigo, Muhongo anajitahidi kutudanganya watanzania lakini ukweli ni kwamba Tanzania bado iko kwenye mgao wa umeme alafu yeye anatuletea personal conflicts zake na Mengi. Hawa wengine matatizo yao mnayajua.

Nawakilisha

Mawaziri wa Elimu na Mawaziri Michezo Nao wafukuzwe kwani utendaji wao umedorora
 
Duh hongera sana CCM yaani mpaka tusiowajua watakua mawaziri?????!!! Mwisho atawekwa hata mwanafamilia
 
Kutoka Kwa Pasco wa JF
Jamiiforums
Mtandaoni.

Kwenda kwa
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ofisi ya Rais Ikulu
S.L.P 9120

DAR ES SALAAM
Simu : 0222116898
Simu : 02222116900/6
Barua pepe : ikulu@ikulu.go.tz

Mhe. Rais/ Mtukufu Rais.

YAH: TUMEJITOLEA KUKUSAIDIA KUKUSHAURI BURE KUHUSU BARAZA LAKO JIPYA LA MAWAZIRI.

Barua hii ya wazi kwako ni kwa mujibu wa Ibara ya 18-1 Katiba ya JMT, inayosema na hapa ninanukuu
Haki ya Uhuru wa Mawazo
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati." ambayo inakwenda sambamba na sheria ya Uhuru wa Maoni Inara ya 6 ya Sheria Na.15 ya mwaka 1984.


Kwa heshima na taadhima, nikiwa raia mwema wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwenye mapenzi mema na nchi yangu, napenda kuchukua fursa hii, kukuandikia barua rasmi ya wazi, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ya kukuomba kwa unyenyekevu mkuu, uzisike sauti zetu za ushauri kwako kwa lengo la kukusaidia kuliunda upya baraza lako la mawaziri!.

Ushauri wenyewe ni HUU na HUU!

Mhe.Rais/ Mtukufu Rais, huu ni ushauri tuu, ukiamua kuutumia, uutumie, ukiamua kuuacha uache, hata kama uliishaamua kuyatumia baadhi ya majina kwenye mapendekezo yetu haya kabla hata sisi hatuja yapendekeza, hivyo uko huru kuendelea kuyatumia, au yote, au baadhi wala hatutajidai kuwa ni sisi ndio tulio kushauri!, au kama vipi, unaona ukiendelea kuwatumia utaonekana umeaunda baraza lako jipya kwa mujibu wa ushauri wa jf, hivyoi kuishushia hadhi taasisi yako ya urais, then uko free usitumie jina lolote kati ya haya, yaani usilitumie hata jina moja kati ya yote yaliyopendekezwa humu ili tusikuingilie kabisa katika mamlaka yako ya uteuzi.

Asante.

Pasco

Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida mwenye umri wa zaidi ya miaka 18, asiye mwanachama wa chama chochote cha siasa, ambaye ni mpiga kura, mwaka 2005 alipiga kura, mwaka 2010 alipiga kura na mwaka 2015 atapiga kura, kwa vile kura ni siri, hasemi alimpigia nani, ila kama Mtanzania, analipa kodi ambazo ndizo zinazomlipa mshahara rais wetu!.



Nimeshindwa kumwelewa mleta mada! Pengine anamatatizo binafsi.Hata chekechea angeandika vizuri kuliko wewe.Nakama ndivyo wazari kaandika basi hata yeye anamapungufu makubwa,japo hakufanya hivyo unavyo mwakilisha.Think before you write often

 
Nimeshindwa kumwelewa mleta mada! Pengine anamatatizo binafsi.Hata chekechea angeandika vizuri kuliko wewe.Nakama ndivyo wazari kaandika basi hata yeye anamapungufu makubwa,japo hakufanya hivyo unavyo mwakilisha.Think before you write often
 
==> Ur totally sick....hysteria...plus illiteracy.....u don*t deserve even div..V...

=> Scented words...



Kutoka Kwa Pasco wa JF
Jamiiforums
Mtandaoni.

Kwenda kwa
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ofisi ya Rais Ikulu
S.L.P 9120

DAR ES SALAAM
Simu : 0222116898
Simu : 02222116900/6
Barua pepe : ikulu@ikulu.go.tz

Mhe. Rais/ Mtukufu Rais.

YAH: TUMEJITOLEA KUKUSAIDIA KUKUSHAURI BURE KUHUSU BARAZA LAKO JIPYA LA MAWAZIRI.

Barua hii ya wazi kwako ni kwa mujibu wa Ibara ya 18-1 Katiba ya JMT, inayosema na hapa ninanukuu
Haki ya Uhuru wa Mawazo
18.-(1) Bila ya kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta, kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati." ambayo inakwenda sambamba na sheria ya Uhuru wa Maoni Inara ya 6 ya Sheria Na.15 ya mwaka 1984.


Kwa heshima na taadhima, nikiwa raia mwema wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mwenye mapenzi mema na nchi yangu, napenda kuchukua fursa hii, kukuandikia barua rasmi ya wazi, Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, ya kukuomba kwa unyenyekevu mkuu, uzisike sauti zetu za ushauri kwako kwa lengo la kukusaidia kuliunda upya baraza lako la mawaziri!.

Ushauri wenyewe ni HUU na HUU!

Mhe.Rais/ Mtukufu Rais, huu ni ushauri tuu, ukiamua kuutumia, uutumie, ukiamua kuuacha uache, hata kama uliishaamua kuyatumia baadhi ya majina kwenye mapendekezo yetu haya kabla hata sisi hatuja yapendekeza, hivyo uko huru kuendelea kuyatumia, au yote, au baadhi wala hatutajidai kuwa ni sisi ndio tulio kushauri!, au kama vipi, unaona ukiendelea kuwatumia utaonekana umeaunda baraza lako jipya kwa mujibu wa ushauri wa jf, hivyoi kuishushia hadhi taasisi yako ya urais, then uko free usitumie jina lolote kati ya haya, yaani usilitumie hata jina moja kati ya yote yaliyopendekezwa humu ili tusikuingilie kabisa katika mamlaka yako ya uteuzi.

Asante.

Pasco

Pasco wa jf, ni Mtanzania wa kawaida mwenye umri wa zaidi ya miaka 18, asiye mwanachama wa chama chochote cha siasa, ambaye ni mpiga kura, mwaka 2005 alipiga kura, mwaka 2010 alipiga kura na mwaka 2015 atapiga kura, kwa vile kura ni siri, hasemi alimpigia nani, ila kama Mtanzania, analipa kodi ambazo ndizo zinazomlipa mshahara rais wetu!.





 
Mkuu Pasco:

Hii ni kufuatana na bandiko lako #117 . Naungana na wewe katika hoja zako za msingi, lakini ningependa kuchangia kama ifuatavyo:

Kwanza - bila ya kuuma uma, nadhani unakubaliana na mimi kwamba baada ya Mkapa kung'atuka, utawala wa nchi umekuwa ni utawala wa 'economy of affection' wa kutumua vigezo vya ndugu, jamaa, rafiki, mwenzetu, kuliko uteuzi based on 'merit'. Lakini muhimu zaidi, huko tuendako, the silent policy ni kujengea mazingira watoto na wajukuu waje kukamata nchi na wao, and this applies to both ikulu ya CCM au Chadema. Hii ni kwa sababu uongozi wa kisiasa sio wito tena au utumishi wa umma bali uongozi sasa umekuwa ni sehemu ya maisha binafsi ya mtu. Kwa maana hii, unapomtaja mtu kama January Makamba ambae kwa ukweli hes fit, ni lazima kuangalia, je, wengine wanajipangeje na watoto na wajukuu zao? Nadhani utakubaliana na mimi kwamba January out shines many in line, na ni kwa maintiki hii, kawekwa kwenye wizara ambayo haina impact kubwa katika maisha ya kila siku ya wananchi walio wengi. Kwa mfano, sekta ya mawasiliano is almost self regulated kupitia TCRA, hivyo ni vigumu kwa waziri katika wizara hii kustaajabisha ya Musa and win the public. Mkuu Pasco, hakuna kijana mwenye elimu, uwezo, msimamo, and rational ambae atapewa nafasi katika serikali ya sasa kwa sababu nilizojadili awali kwamba kufanya hivyo kutaharibu "calculations za the economy of affection".

Sababu yangu kumtaja January kwenda Unaibu Mambo ya Ndani au Uwaziri Kamili hapo hapo ni hiyo hiyo - kwamba pale, pamoja na ukubwa na uzito wa wizara, waziri husika hana much influence kwani IGP, Magereza etc zinasimama zenyewe kama taasisi. Ni kwa mantiki hii, Lau Masha kupelekwa mambo ya ndani wasn't a threat, na hata Nchimbi. Kwa maana hii, January Makamba kupewa wizara zenye mashiko na ukaribu na umma itakuwa ngumu kwani hes brilliant, and his performance itavuruga mikakati ya maandalizi ya vijana "wanaohitajika" na wenye nchi.

Kuhusu wizara ya ulinzi na JKT, katibu mkuu aliyepo sasa is very brilliant, na pia ni mtu mwenye vigezo unavyovijadili, kwahiyo hayo unayoyasema ataya handle kiutendaji, huku uwaziri ambao ndio face ya wizara ikihitaji mwanadiplomasia;

Kuhusu wizara za muungano to alternate baina ya wazanzibari na watanganyika, nakubaliana na wewe lakini hili halitokei wakati wote kwa sababu its a silent policy, hivyo mamlaka ya uteuzi inaweza fanya itakavyo kukidhi matakwa lengwa. Kwa mfano, Wizara ya Afya sio ya muungano, lakini mzanzibari ndiye waziri pale; Same applies to Wizara ya Sayansi, Tekinolijoa na mawasiliano.

Kuhusu Muhongo kwamba anakwenda na maji - kwanini unafikiri hivyo? Je ni kwa sababu ameingia katika malumbano na mchangiaji wa ule mradi/mfuko? Kwa mtazamo wangu, Muhongo ataondoka Nishati na Madini lakini hatoondoka kwenye baraza la mawaziri. Pamoja na mapungufu yake mengi, anaipa CCM mileage fulani katika kada fulani fulani ndani ya jamii.

Mwigulu - huyu sidhani kama watamuacha aendelee na nafasi yake ya pale Lumumba kutokana na mtafaruku alionao na chadema. Kwa mtazamo wangu pengine finyu, hali imefikia pabaya sana, na ifike mahala mamlaka ya uteuzi itumie busara kulimaliza hili, hivyo kwa vile wanamhitaji, kuna umuhimu wa kumpa unaibu waziri kwenye wizara ambayo haitampa nafasi ya kuendeleza yanayojiri sasa. Ni kweli kwamba wizara ya fedha ina issue ya muungano, na hoja yangu juu ya unaibu wa mwigulu fedha ipo based kwenye assumption kwamba manaibu mawaziri fedha wataendelea kuwa wawili. Moja ya wizara ambazo akipelekwa hatokuwa na means za kuendeleza siasa zake ni wizara ya fedha (kuendana na elimu yake ya Uchumi), kama sio kwenda kwa January Makamba (Mawasiliano) ambayo ina characteristics nilizojadili hapo juu. Isitoshe, Mwigulu alishasema kwenye vyombo vya habari kwamba CCM yeye keshachagua upande (urais 2015) na nadhani unajua implications zake...

Kuhusu Makongoro Mahanga - huyu ni msomi mzuri tu (ukiachilia ile PhD), na ni mtendaji mzuri akipewa sehemu inayohitaji kichwa kizuri, suala ambalo halijatokea bado. Isitoshe, nadhani unajua kwamba huyu yupo kambi yako, kwahiyo atawekwa sehemu za ajabu ajabu tu ili asing'are. Sababu yangu kumtaja kupanda kuwa waziri kamili ni kwamba - Mkoa wa DSM haujawahi kuwa na waziri kamili kwa muda sasa (wa mwisho alikuwa ni Charles Keenja, ubungo 1995 - 2005 na Rita Mlaki, kawe (1995 - 2005). Katika pita pita zangu nimewasikia wana CCM wengi wa majimbo ya DSM wakilalamika kwamba hawana mawaziri, na kuelekea 2015, wanataka wagombea ambao watakuwa na sifa za kuteuliwa moja kwa moja kuwa waziri. Assumption hapa ni kwamba majimbo husika yatachukuliwa na CCM, na pia ikulu itabakia CCM.

Kuhusu Lowassa na Uwaziri - naunga mkono hoja, pamoja na mapungufu yake ya hapa na pale, Lowassa anahitajika sana kuweka mambo sawa ndani ya serikali kiutendaji. Mwaka 2008, ilitamkwa kwamba yaliyomkuta Lowassa ilikuwa ni 'ajali ya kisiasa', je, majeraha ya ajali hayo hayajapona tu kwa miaka mitano? Au alipata donda dugu?

Mwisho ni kuhusiana na swali lako juu ya nafasi ngapi za ubunge wa kuteuliwa na rais zimebakia. Nafasi hizo ni mbili, na nimependa sana kusoma majina uliyoyataja - Silaa na Ruge. Katika miezi hii kumi na saba kabla ya uteuzi wa mgombea urais (CCM) for 2015 elections, kwa kweli lolote linawezekana.
Mkuu Mchambuzi, I hope huta mind, nimemkaribisha rasmi JK katika uzi huu pia nimeuweka ule uzi wako tangulizi.

Baadhi ya hoja zako nitakujibu.
Pasco.
 
Mkuu Samaritan, kiukweli Chadema ina watu very inteligent na wengine ni ma intelectual wenye impacable ability, ila kiukweli kabisa sioni any systematic approach ya kutaka kushika dola 2015!. Kila nikiuliza humu, huambiwa huishia kubezwa hadi kutukanwa!.

Nimetokea kuwafahamu baadhi yao kwa karibu na kuhudhuria kampeni zao, kuna baadhi walioshinda ubunge kwa sababu tuu CCM imechokwa!, lakini hawana ability, capability wa intergrity yoyote iliyowafanya washinde!.

Nilipowaambia hawajipanga, nilishauri waje na plan watafanya nini tofauti na CCM, they have nothing!, no plan, no strategy, wanategemea kura za walioichoka CCM!, huku CCM chovu ikijivua lawama kuhusika na madudu ya serikali yake!, inawarudia wananchi sio tuu kuwapa pole kwa madhila ya serikali mbovu, bali pia kukubali makosa na kuahidi kuyashughulikia!. Na masikini Watanzania waliowengi, hawana kumbukumbu ya ahadi ngapi zimetekelezwa, 2015 CCM itakuja na track records ya tuliahidi hili, tumetekeleza hili, ila pia licha ya kutoahidi kuhusu katiba, tumewaletea zawadi mzuri na yenye thamani kuliko chochote kwa Watanzania, ni katiba mpya!, ukijumlisha na "safety net project" iliyotengewa TZS bilioni 400 kuzigawa hard cash kwa familia masikini!, 2015 ni aCCM tena!.

Chadema wako bize kukijenga chama kwa kubomoa misingi na kukata mizizi mikuu, wakijiaminisha machipukizi yao kama kina Lema, nao watageuka mizizi kama Zitto, hivyo hakitatikisika!.

Sisi wengine kiukweli kabisa hatuna vyama, ila tunaitaka Tanzania yenye neema, CCM has failed us miaka nenda miaka rudi, hivyo Chadema kinaonekana kama ndilo tuumaini pekee la ukombozi!, kazi yetu ni kuliambia tumaini hili, this is the way, follow the right way, wenyewe wanajijua na wanajiamini njia pia wanazijua, hawakubali kuambiwa lolote wala kusikia lolote hivyo itakapofika 2015 wakashindwa, akina sisi sio tuu tutawakumbusha bali pia tutawazomea kwa kushindwa kwa upumbavu wao wa kukosa maarifa!.

Kati ya wanajf wote, japo Mchambuzi ni CCM, hakuna aliyewapa nondo nzuri za ushindi waziwazi kama Mchambuzi, ila kwa vile ni CCM, sijua hata kama wanasoma michango yake. Labda kwa vile Mzee Mwanakijiji na Nguruvi 3 wameishatake sides, na wanapeleka ushauri jikoni direct, sijui ila Chadema ina kila sababu ya kushinda uchaguzi wa 2015, pia nia wanayo tatizo ni uwezo!, kukubali hawana uwezo huo ili wasaidiwe hawataki!, imebaki wakicheza tuu makida makina huku wakichezea shilingi yao choo kwa " bura yao nema" kubadili na rehani!.
Pasco

mkuu PASCO, kuunda serikali hakuhitaji mambo mengi kama unavyo fikiri! kinachotakiwa ni kuwa na mkakati na nia thabiti ya kuleta maendeleo.kazi ya chama kinacho shinda uchaguzi na kushika dola ni kuisimamia serkali kikamilifu.wafanyakazi serikalini wapo tena wenye maarifa ya kutosha.kinacho kosekana ni usimamizi ili walete TIJA.siku hizi mfanyakazi serikalini hata afanye kosa gani hawezi kufukuzwa kazi labda auwe! jiulize hapo kweli kuna serikali?

siku hizi unaweza kukuta kijana amehitimu chuo kikuu hajui kuandika barua ya kikazi! nini maana yake? Ni kwamba elimu haina usimamizi wa karibu kinacho takiwa ni kuwawajibisha wanaosimamia wamezembea somewhere,hawatakiwi kuonewa huruma hao.kazi ya chama dola ni kuchukua hatua na kuigiza serikali nini cha kufanya.

For your information, Michael satta amechukua serikali wakati chama chake kina umri usio zidi miaka kumi katika siasa,mbona anaiweza Zambia na walau sasa wanaanza kupata political and economical stability.husikii tena bei ya mkate inapanda hovyo! sembuse CHADEMA kina miaka karibu ishirini kwenye active politics tena wana viongozi na makada walio onesha kuwa uwezo wanao.

Mwalimu aliunda serikali akiwa na graduates wachache sana.karibu viongozi wote walikuwa darasa la tano au kidato cha nne lakini aliweza kujenga serikali yenye mwelekeo.wananchi waliiheshimu kwasababu mwalimu aliisimamia serikali yake kikamilifu.kwahiyo kinachotakiwa ni kuwa na mission na vision halafu usimamizi imara.hakuna chama kinacho ingia madarakani kikabadili wafanyakazi wote. wanaoingia ni political administrators basi.wengine watabaki walewale isipo kuwa namna ya kuwasimamia.

PASCO,Tambua kuwa hakuna mahali kwa kufanya mazoezi jinsi ya kushika dola na kufanya tathimini kama mnaweza.indicator kwamba hiki ni chama makini ni jinsi walivyo weza kujijenga na kuwa taasisi inayo aminika ndani na nje ya nchi.kuna vyama vingi tu hapa nchini hata havijulikani kama vipo pamoja na kuwa vina usajili wa kudumu.CHADEMA ya MBOWE,DR SLAA,TUNDU LISSU,MNYIKA,SAUTI YA RADI,MSIGWA,nk mimi nina imani nao sana.
 
21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom