Baraza la Mawaziri: Nani atoke, Nani abaki, Nani aingie?

Lembeli naona anafaa sana kuwa waziri wa mambo ya ndani au kangi
huyu anaemiliki huu mjengo mkubwa huko kusini inabidi atoswe kukinusuru chama
attachment.php

Mkuu si kweli hamiliki hili jengo.Achana na tetesi.Nina uhakika 100%
 
Unamjua malima au unamsikia??Unajua kwanin alitolewa pale nishati? Yule mtu hafai. Some of us tulipewa kazi ya kumfuatilia mpaka nje na safari zake.
Hana tatizo, ukiondoa kusafiri na bulk cash na silaha za vita, hana tatizo jingine lolote!, kama ni issue za "blanketi" la baridi awapo safarini, waheshimiwa wote hujifunika, huku wengine wakibeba mablangeti yao toka nyumbani!, kama kosa lake ni kutumia mablangeti ya huko huko anakofikia tena kwa kujitafutia mwenyewe, then he is better off kwa sababu, kwanza anasaidia kuinua uchumi wa hapo anapofikia, wakati wale wabebao, wanatia hasara kusafiri na mizigo mingi hivyo kuongeza uzito!.

Najua tatizo lenu nyinyi kina Amini usiamini, kwa vile mko huko kwenye bold, mlitaka mpewe kibarua cha kuwa mnawatufutia waheshimiwa mabrangeti "yenu yale" akidai ati lazima wajifunike mabrangeti yaliyokuwa "approved" kitendo cha yeye kujichagulia blangeti kumefanya kazi yenu ya kufuatilia watu kuwa ngumu!, hivyo kumuundia zengwe huko kwenu!. Kwa vile mambo za kuzuia baridi kwa blangeti pia ndio zake mukulu wabangoi, then jamaa lazima atabaki na haswa kwa kukizingatia kile kibalaghashia!.
Pasco.
 
Mwigulu Nchemba atapewa wizara ya mambo ya ndani!!!! Ahhh'aaaaa. Kwa JK kila kitu kinawezekana.Itapangwa timu ya kuwatokomeza viongozi was upinzani hasa CHADEMA
 
Muungwana Pasco...umeniwahi kupost hii topic...TANESCO walizima ghafla MWANGA.

Kwa kuangalia nyakati na majira na mwelekeo wa uchaguzi KISAYANSI 2015
, wafuatao ni baadhi ya watakao bidhiwa KAZI ya kuwatumikia wananchi...

1. AS Migiro --- Mambo ya Nje au Elimu
2. Mwanri ----TAMISEMI
3. J Makamba --- N-Nje au M/ndani
4. Deo Fulikonjombe ---
5. S Masele -- Nishati na Madini akitolewa yule Prof MROPOKAJI

Wadau nawasilisha kwa kuanzia.

NB: PINDA HATOKI hadi JK amalize kipindi chake ili ku-stabilize SERIKALI

Kwa mtazamo wangu:

-Mwanri-nakubaliana na wewe;
-Makamba junior - nakubaliana na wewe kuwa naibu nje au ndani, lakini pia anaweza pandishwa pale pale alipo sasa kuwa waziri kamili au kuwa waziri kamili mambo ya ndani;
-Prof Mbarawa - Ulinzi na JKT
-Membe kutoka wizara ya mambo ya nje ni ngumu, atamaliza na JK; Kama atatoka, basi anaenda fedha kumpisha migiro nje;
-Migiro ataenda fedha iwapo membe atabakia nje;
-Muhongo - Viwanda na Biashara;
-Dalali Peter Kafumu - Nishati na Madini;
-Engineer Stella Manyanya atatolewa ukuu wa mkoa na kupewa wizara;
-Anna Kilango atapewa unaibu waziri - mkoa wa kilimanjaro umeishiwa wabunge (ccm) wa kupewa uwaziri kwani chami, magembe, mathayo wameshachafuka; Kilango ataungana na Mwanri kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro kwenye cabinet;
-Mwigulu Nchemba atatolewa Lumumba na kupewa unaibu waziri, pengine fedha;
-Gaudence Kayombo (Mbinga) ataletwa kwenye unaibu kuziba pengo la Nchimbi kama mwakilishi wa wanaruvuma;janista mhagama pia anaweza teuliwa badala ya kayombo iwapo ana degree;
-Amos Makala - waziri kamili;
-Makongoro Mahanga - waziri kamili;
-Nyalandu - waziri kamili.
-Dr. Ndungulile - Naibu Waziri.
-Prof Mwandosya - Iwapo afya yake imeimarika, atapewa wizara kamili, hasa wizara ya Maji;
-Prof Mwandosya asiporudi kwenye wizara kamili, Prof Mwakusya atarudishwa kwenye cabinet;
-Prof Msola - Elimu (kuziba pengo la waziri wa fedha kama mwakilishi wa wana iringa kwenye cabinet);
-Filikunjombe - hawezi kupewa nafasi kwani ataharibia wahusika calculations zao za kuandaa vijana wao kwa sasa na baadae;



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Mkuu si kweli hamiliki hili jengo.Achana na tetesi.Nina uhakika 100%
Kwani hata angekuwa ndio mmiliki, kwani siku hizi kiongozi kumiliki mali ni kosa?!, si inategemea tuu umezipataje!. Kama ni umiliki wa mahoteli tuu, hebu nenda pale Bwaga, ulizia a`liyeuziwa lilie jengo la kihistoria lililokuwa soko la watumwa na sasa ameligeuza ni hoteli!.

Jamaa hawezi toswa kwa sababu pia ni dam dam!, atasogezwa tuu ili kumpunguza impact ya safari ya kuelekea 2015.
Pasco.
 
Sio mmoja, tuna wanajamvi watatu humu ambao ni wabunge wa CCM, verified na wote watatu wanaweza chaguliwa manaibu yule mmoja anaweza kuwa full!.

Dr. Kigwa is capable kama JK ataacha kusikiliza umbea, fitna, zengwe, siasa za maji taka kwa propaganda ganda chafu ndani ya CCM, atamteu Dr. Kigwa ndani ya timu mpya.

Dr. Mary Mwanjelwa anaweza kuteuliwa, japo udakitari wake sio wa kivile sana, lakini Sugu, ameisumbua sana serikali pale Mbeya, huyu dada ndio tishio, hivyo atapewa tuu ili kumuongezea nguvu za kumgoa Sugu pale Mbeya!.

Mwigulu Mchemba, japo he is always a joker, anaelimu ya ukweli na anauwezo wa ukweli wa uwaziri.

Pasco

Mwigulu Nchemba tena!? Kweli hapo Rais atakuwa amechemka
 
yaani we paskali usipomtaja yule muasisi wa kampuni ya kufua umeme ya mfukoni huwa unahisi bandiko lako halina mashiko
 
Kwa mtazamo wangu:

-Mwanri-nakubaliana na wewe;
-Makamba junior - nakubaliana na wewe kuwa naibu nje au ndani, lakini pia anaweza pandishwa pale pale alipo sasa kuwa waziri kamili au kuwa waziri kamili mambo ya ndani;
-Prof Mbarawa - Ulinzi na JKT
-Membe kutoka wizara ya mambo ya nje ni ngumu, atamaliza na JK; Kama atatoka, basi anaenda fedha kumpisha migiro nje;
-Migiro ataenda fedha iwapo membe atabakia nje;
-Muhongo - Viwanda na Biashara;
-Dalali Peter Kafumu - Nishati na Madini;
-Engineer Stella Manyanya atatolewa ukuu wa mkoa na kupewa wizara;
-Anna Kilango atapewa unaibu waziri - mkoa wa kilimanjaro umeishiwa wabunge (ccm) wa kupewa uwaziri kwani chami, magembe, mathayo wameshachafuka; Kilango ataungana na Mwanri kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro kwenye cabinet;
-Mwigulu Nchemba atatolewa Lumumba na kupewa unaibu waziri, pengine fedha;
-Gaudence Kayombo (Mbinga) ataletwa kwenye unaibu kuziba pengo la Nchimbi kama mwakilishi wa wanaruvuma;janista mhagama pia anaweza teuliwa badala ya kayombo iwapo ana degree;
-Amos Makala - waziri kamili;
-Makongoro Mahanga - waziri kamili;
-Nyalandu - waziri kamili.
-Dr. Ndungulile - Naibu Waziri.
-Prof Mwandosya - Iwapo afya yake imeimarika, atapewa wizara kamili, hasa wizara ya Maji;
-Prof Mwandosya asiporudi kwenye wizara kamili, Prof Mwakusya atarudishwa kwenye cabinet;
-Prof Msola - Elimu (kuziba pengo la waziri wa fedha kama mwakilishi wa wana iringa kwenye cabinet);
-Filikunjombe - hawezi kupewa nafasi kwani ataharibia wahusika calculations zao za kuandaa vijana wao kwa sasa na baadae;
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Mkuu Mchambuzi, ingekuwa kuna watu wanaostahili kulipwa kwa michango iliokwenda shule, wewe ni mmoja wao.

Haswa upande wa reasoning power. Hilo la Kilango sikulikumbuka ni kweli kuna watu watachaguliwa kwa sababu tuu ya ku balance uwiano wa uwakilishi. Hili la Deo, Kangi na Zambi wanaweza kuletwa ili tuu kuwa contain!.
Mwanri-atabaki sio kwa sababu ya uwezo wa kutenda bali kusema!. Tamisemi inahitaji watendaji na sio wasemaji!.
-Makamba junior - ndio nyota ing'aayo, ndio kijana wa "king maker" na ndiye yule jamaa yangu anamfagilia njia!. Tatizo la kijana ni dini!, soon mtamshuhudia akimsindikiza mama yake kanisani!, mama Jan ni Mkatoliki!, hivyo atapelekwa MFA kuing'arisha zaidi nyota yake ila pia nakubaliana na wewe anaweza pandishwa pale pale alipo sasa kuwa waziri kamili au kuwa waziri kamili ila mambo ya ndani hapana, hii ni wizara ya muungano, mawaziri lazima wapishane bara na Zanzibar kama ulinzi, kwa vile alianza Zanzibar ndipo akaja bara, this time ni Zanzabar mambo ya ndani, halafu bara Ulinzi, hapa anaweza kuletwa Suluhu au Mbarawa!.
- Ulinzi na JKT kutokana na hali tete ya Ziwa Nyasa na ile "coalition of the willing!", Ulinzi ataleta mjeshi kama Kangi!.
-Membe atang'olewa kutoka wizara ya mambo ya nje ni ili kumzuia asioteshwe ile ndoto, na hawezi kumpeleka fedha huko kutakuwa ni kumuongezea nguvu!.
-Migiro ameletwa strategically just to loo kura za wanawake 2015, she is never a performer, hivyo atapelekwa wanawake na watoto!.
-Muhongo ataondolewa kabisa sambamba na Mgimwa!- Viwanda na Biashara atampa Lazaro, au atampeleka Utalii ili wife pia asaidie kupepesha bendera yetu!
-Dalali Peter Kafumu - Nishati na Madini nakubaliana na wewe.
-Engineer Stella Manyanya atatolewa ukuu wa mkoa na kupewa wizara hii pia ni posible!.
-Anna Kilango atapewa unaibu waziri - mkoa wa kilimanjaro umeishiwa wabunge (ccm) wa kupewa uwaziri kwani chami, magembe, mathayo wameshachafuka; Kilango ataungana na Mwanri kuwakilisha mkoa wa Kilimanjaro kwenye cabine, hii nakukubalia 100% kwa 100% na sababu nyingine pia ni CCM kuendelea ku hold the little grip ya Kaskazini vinginevyo CCM inasafishwa yote!. Hata Ole Medeye atang'olewa na EL anaweza kurudishwa kuwapooza morani!.
-Mwigulu Nchemba atatolewa Lumumba na kupewa unaibu waziri, pengine fedha hili nakubaliana na wewe, ila sio fedha!. Kwa vile fedha ni wizara ya Muungano, ili Mwigulu awe naibu, minister lazima atoke Zanzibar!. Kwa hali ilivyo sasa, we can't trust any Zanzibari na fedha zetu hivyo naibu lazima atoke Zanzibar hivyo aliyepo kuiendelea!.
-Gaudence Kayombo (Mbinga) ataletwa kwenye unaibu kuziba pengo la Nchimbi kama mwakilishi wa wanaruvuma;janista mhagama pia anaweza teuliwa badala ya kayombo iwapo ana degree; wanaweza kuteuliwa wote, Jeanistar ana kadrigrii zile za mchoro mchoro kama Ph.D ya Mama Nagu!, ila hata bila digrii ya ukweli, she is very capable ukiondoa tatizo dogo la mkorogo kama Mwanjelwa na Mlata!.
-Amos Makala - waziri kamili nakubaliana na wewe.
-Makongoro Mahanga - waziri kamili sina uhakika sana maana namuona kama hana any impact!.
-Dr. Ndungulile - Naibu Waziri nakubaliana na wewe, hiki kijamaa ni smart, ila poa kuingingia kifua CCM ndidhi ya nguvu ya CUF kipande ile!.
-Prof Mwandosya - Iwapo afya yake imeimarika, atapewa wizara kamili, hasa wizara ya Maji (haijatengemaa kihivyo)
-Prof Mwandosya asiporudi kwenye wizara kamili, Prof Mwakusya atarudishwa kwenye cabinet-nakubaliana na wewe hii ni possible!.
-Prof Msola - hawezi kurudishwa!, alishakuwepo na kuboronga fulani, Sayansi ikiwa na Elimu ya Juu!. ila pia imethibitika maprofesa ni bure kabisa!. Sarungi wa good akiwa Muhimbili, alipopewa wizara alishindwa!.
wana Iringa wataletewa kijana Deo kama mwakilishi wao kwenye cabinet na sio kurusha makapi ya zamani!.
Haka kakijana ka Dewji kama katakubali, kanaweza kupewa unaubu Viwanda na biashara ila kako tuu buzy!.
Sikumbuki nafasi za rais za uteuzi wa wabunge zimebaki ngapi anaweza kuchukua young blood kama kale ka Jerry au hata Ruge!.
Pasco.
 
=> PM - Dr. Harrison Mwakyembe..

=> Mambo ya nje.....Membe..

=> Nishati & Madini...Prof. Muhongo (no changes)
huyu anafaaa sana....he knows exactly wht he is
doing, highest intellectual standard...

=> MALI ASILI NA UTALII....KAGASHEKI....atarudishwa
tu na Rais.....hakuna anayeweza wizara hii kama
KAGASHEKI....hili hata Rais na wananchi wanajua

=> TAMISEMI ...Aggrey Mwanri

=> UJENZI....Dr. Magufuli...

=> Transport....Dr. Shabaan Mwinjaka... ( Permanent
Secretary wa Wizara kwa sasa )


=> Kilimo ... Kigoma Malima..

=> UTUMISHI....baadae ntaleta

=> FEDHA...Waziri Dr. Mgimwa....Naibu...?? Sada out..

=> Wanawake, jinsia na watoto....Asha Rose..

=> WATAKAO UPOTEZA UWAZIRI NI HAWA....Kawambwa...Maghembe....Mkuchika...CelineKombani...Hawa Ghasia....Mulugo ( Elimu ) ...
 
1.Waziri wa mambo ya ndani- Mwigulu Nchemba.
2. Waziri wa maliasiri na utalii- Asha rose Migiro na Zambi akiwa naibu wake
3. Waziri wa mifugo- Mh. Laizer
4. Waziri wa Ulinzi- Vita Kawawa
 
Watanzania tumekuwa wagumu sana linapokuja swala la kuwajibika likitokea tatizo katika eneo lako la kazi. Tunashuhudia viongozi wengi duniani wakiwajibika kwa makosa madogo sana ukilinganisha na makosa yanayotokea hapa nnchini. Ivi dr nchimbi na nahodha ivi hamkuona kabisa sababu ya kuwajibika pamoja na madhara yote hayo yaliyosababishwa kwa wanachi? Tumezoea siasa lakini linapokuja swala la maisha ya binadamu kudhulumiwa nilitegemea mjihuzuru bila kulazimishwa na kujitwalia heshima kwa watanzania. Lakini imekuwa kinyume kabisa na hivyo mnahesabika mmefukuzwa kazi. Kagasheki nakukubali sana kwa kuwa ww hujafukuzwa kazi ila ulikubali mwenye kuachia ngazi kabla uamuzi wa kufukuzwa haujatangazwa.
 
Hawa nao ni mizigo, Muhongo anajitahidi kutudanganya watanzania lakini ukweli ni kwamba Tanzania bado iko kwenye mgao wa umeme alafu yeye anatuletea personal conflicts zake na Mengi. Hawa wengine matatizo yao mnayajua.

Nawakilisha
 
WAZIRI wa mambo ya ndani MWIGULU?
KWELI busara hekima na maarifa vitakuwa vinaongozwa na ulimbukeni
 
kweli kama inaweza kuwa, ili migiro apige pesa kwenye utalii ya kujianda na urais
 
Back
Top Bottom