Baraza la Mawaziri lakutana kikao cha kwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la Mawaziri lakutana kikao cha kwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Nov 29, 2010.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna taarifa kwamba Baraza la Mawaziri limekutana leo kwa mara ya kwanza. Tusubiri tuone yatakayojiri.

  -------
  UPDATE:

  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Novemba 29, 2010, amekutana rasmi kwa mara ya kwanza na Baraza la Mawaziri lake jipya pamoja na Naibu Mawaziri na kuwapa maelekezo ya awali ya nini anakitarajia kutoka kwa wateule wake hao.

  Mawaziri wote 29 na Naibu Mawaziri wote 21 ambao Rais Kikwete aliwaapisha rasmi kushika nyadhifa zao katika sherehe iliyofanyika Jumamosi iliyopita, Novemba 27, 2010, wamehudhuria mkutano huo kwenye Chumba cha Baraza la Mawaziri, Ikulu, Dar es Salaam.

  Katika mkutano huo uliochukua kiasi cha saa tatu, Rais alianza kwa kuwaeleza mawaziri kuwa katika kipindi hiki cha pili cha uongozi wake hakutakuwepo na muda wa kupoteza, na wala hatakuwa tayari kukubali maelezo ya kwa nini utekelezaji wa majukumu ya msingi umeshindikana.

  Kwa mara nyingine amewapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri hao akisisitiza: “Mnastahili pongezi hasa ukizingatia ukweli kwamba nyinyi mmebahatika kuteuliwa kutoka kwenye orodha ndefu ya wabunge wengi wenye sifa za kushika nafasi mlizo nazo. Nimewateua kwa imani kuwa pamoja nanyi, tutatimiza matumaini ya wananchi wa Tanzania waliokichagua Chama cha Mapinduzi kiendelee kuongoza nchi yetu.”

  Ameongeza: “Ni imani yangu kuwa kwa mshikamano na ushirikiano wetu kama timu moja ya ushindi, tutatekeleza majukumu yote kwa uadilifu, uaminifu na ufanisi wa hali ya juu. Ufanisi wa Waziri ama Naibu Waziri katika utekelezaji wa majukumu yake unategemea sana ufahamu na uelewa wake wa masuala muhimu yanayohusu Nchi, Serikali na Wizara anayoiongoza.”

  Katika mkutano huo ambao ameuelezea kama wa Utangulizi wakati inaandaliwa Semina Elekezi, Rais Kikwete amewaelezea wateule wake maana ya Baraza la Mawaziri na majukumu yake, na kutaka kila Waziri ahakikishe anatayarisha kalenda yake ya masuala muhimu ambayo anataka yajadiliwe na Baraza la Mawaziri kwa mwaka.

  Rais Kikwete pia amewaeleza wateule wake kuhusu wajibu wa Mawaziri katika Bunge akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila waziri kuhudhuria vikao vyote vya Bunge, na kuwa ndani ya Bunge mawaziri wote wa Serikali lazima wawajibike kwa pamoja.

  “Ni muhimu ieleweke kuwa kama ilivyo kwa maamuzi ya Baraza la Mawaziri, uwajibikaji wa Mawaziri Bungeni ni wa Pamoja. Kwa hiyo, Hoja ya Serikali Bungeni ni Hoja ya Mawaziri Wote na siyo Waziri anayewasilisha hoja tu,” amesema Rais Kikwete.

  Rais pia amewakumbusha wateule wake kuhusu uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) katika kuongoza nchi, akisisitiza kuwa uwajibikaji huo unaelezwa kwa ufasaha katika Hati Maalum (Instrument) ya Majukumu ya kila Wizara.

  Kuhusu uhusiano kati ya Waziri na Rais, na kati ya Waziri na Waziri Mkuu, Rais amesema kuwa pamoja na kwamba shughuli zote za utendaji Serikalini hutekelezwa kwa niaba ya Rais, lazima mawaziri wakumbuke kuwa Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali.

  Rais Kikwete pia ametaka kujengeka mahusiano mazuri kati ya Waziri na Naibu Waziri wake akisisitiza: “Jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba uhusiano mzuri baina ya viongozi hawa ni nguzo muhimu katika mafanikio ya Wizara. Kwa hiyo, ili kuepuka migongano katika utekelezaji ni muhimu mipaka ya kazi za Waziri na Naibu Waziri ikaheshimika na pia ni wajibu wa Waziri kumpangia kazi Naibu Waziri katika Wizara husika.

  Katika mkutano huo, Rais Kikwete pia amezungumzia uhusiano kati ya Waziri na Katibu Mkuu; uhusiano kati ya Waziri wa Nchi Asiyekuwa na Portfolio na Katibu Mkuu; uhusiano kati ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu, na uhusiano kati ya Waziri na Waziri wa Sekta Nyingine.

  Rais Kikwete pia amefafanua kuhusu uhusiano kati ya Wizara na Wadau Wengine; uhusiano baina ya Wizara, Mikoa na Halmashauri; uhusiano na Taasisi Zilizo Chini ya Wizara; uhusiano na Wasaidizi wa Mawaziri pamoja na utekelezaji wa Maagizo ya Viongozi wa Kitaifa.

  Rais Kikwete pia amewaeleza Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu nyaraka muhimu ambazo wanapaswa kukabidhiwa na kuzipitia watakapofika kwenye nafasi zao mpya za kazi. Nyaraka hizo ni pamoja na Taarifa ya Makabidhiano ya Ofisi, Katiba, Ilani ya Chama Tawala, Dira ya Taifa, na Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA).

  Aidha, Rais Kikwete amewaeleza wateule wake kuhusu umuhimu wao kufahamu Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu, Mikakati, Mipangomkakati, Mpango na Bajeti ya Wizara, Mpango wa Kazi wa Wizara na Masharti ya Kazi ya Waziri.

  Rais Kikwete vile vile amekumbusha Mawaziri na Naibu Mawaziri wake kuwa suala la vita dhidi ya rushwa ni suala la kikatiba na kuwataka kuhakikisha kuwa Mpango wa Pili wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa (NACSAP-11) unatekelezwa.

  Pia amewataka Mawaziri kusimamia mapato ya Serikali yasiyotokana na kodi na kudhibiti matumizi ya Serikali.
  Rais Kikwete pia amewataka viongozi hao kuzingatia maadili ya uongozi ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria za nchi, kuheshimu sheria katika shughuli na mambo yao binafsi na pia kutunza siri za Serikali kwa mujibu wa kiapo chao.

  Rais Kikwete pia amesisitiza umuhimu wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuwasiliana na wananchi kwa maana ya kueleza mafanikio ya Serikali na mipango ya Serikali katika kushughulikia matatizo ya wananchi.

  Amewataka kuvitumia kikamilifu Vitengo vya Mawasiliano ya Serikali katika wizara zao ambavyo ndivyo vyenye jukumu la kutoa taarifa kuhusu Wizara inavyotelekeza majukumu yake.

  “Uzoefu unaonyesha kuwa Mawaziri wengi ni wazito kufanya mawasiliano na wananchi hata pale ambako Wizara imefanya mambo mengi mazuri. Hivyo, Mawaziri muwe mstari wa mbele kuelezea mafanikio ya utendaji wa Serikali katika Wizara zetu,” ameelekeza Rais Kikwete na kuongeza:

  “Lazima ujengwe utamaduni wa kudumu wa kuwasiliana na wananchi wote ambao ndio waajiri wetu kupitia kura zao. Mawaziri wote tumieni Vitengo vyenu vya Mawasiliano na vyombo vya habari kwa ustadi ipasavyo,” amefafanua Rais Kikwete.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  29 Novemba, 2010
   
 2. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ok.
   
 3. chobu

  chobu JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa hata mimi hiyo nimeipata!!!!!!!!!!
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nisaidieni hivi manaibu waziri ni wajumbe wa baraza la mawaziri?
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Thanx kwa taarifa, mwanaJF ndani ya kikao, tunaomba minitisi za kikao.
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Nov 29, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  hakuna la maana wanaenda kunywa chai tu na sambusa huko..hakuna la maana lolote watakalo ongea hawa
   
 7. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  well said. ni introductory meeting. Ni keki, sambusa, shampeni, soda, maji etc. nathing more
   
 8. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone: 255-22-2114512, 2116539
  E-mail: press@ikulu.go.tz
  Website: Mawasiliano Ikulu
  Fax: 255-22-2113425  PRESIDENT’S OFFICE,
  THE STATE HOUSE,
  P.O. BOX 9120,
  DAR ES SALAAM.
  Tanzania.  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  RAIS Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Novemba 29, 2010, amekutana rasmi kwa mara ya kwanza na Baraza la Mawaziri lake jipya pamoja na Naibu Mawaziri na kuwapa maelekezo ya awali ya nini anakitarajia kutoka kwa wateule wake hao.

  Mawaziri wote 29 na Naibu Mawaziri wote 21 ambao Rais Kikwete aliwaapisha rasmi kushika nyadhifa zao katika sherehe iliyofanyika Jumamosi iliyopita, Novemba 27, 2010, wamehudhuria mkutano huo kwenye Chumba cha Baraza la Mawaziri, Ikulu, Dar es Salaam.

  Katika mkutano huo uliochukua kiasi cha saa tatu, Rais alianza kwa kuwaeleza mawaziri kuwa katika kipindi hiki cha pili cha uongozi wake hakutakuwepo na muda wa kupoteza, na wala hatakuwa tayari kukubali maelezo ya kwa nini utekelezaji wa majukumu ya msingi umeshindikana.

  Kwa mara nyingine amewapongeza Mawaziri na Naibu Mawaziri hao akisisitiza: “Mnastahili pongezi hasa ukizingatia ukweli kwamba nyinyi mmebahatika kuteuliwa kutoka kwenye orodha ndefu ya wabunge wengi wenye sifa za kushika nafasi mlizo nazo. Nimewateua kwa imani kuwa pamoja nanyi, tutatimiza matumaini ya wananchi wa Tanzania waliokichagua Chama cha Mapinduzi kiendelee kuongoza nchi yetu.”

  Ameongeza: “Ni imani yangu kuwa kwa mshikamano na ushirikiano wetu kama timu moja ya ushindi, tutatekeleza majukumu yote kwa uadilifu, uaminifu na ufanisi wa hali ya juu. Ufanisi wa Waziri ama Naibu Waziri katika utekelezaji wa majukumu yake unategemea sana ufahamu na uelewa wake wa masuala muhimu yanayohusu Nchi, Serikali na Wizara anayoiongoza.”

  Katika mkutano huo ambao ameuelezea kama wa Utangulizi wakati inaandaliwa Semina Elekezi, Rais Kikwete amewaelezea wateule wake maana ya Baraza la Mawaziri na majukumu yake, na kutaka kila Waziri ahakikishe anatayarisha kalenda yake ya masuala muhimu ambayo anataka yajadiliwe na Baraza la Mawaziri kwa mwaka.

  Rais Kikwete pia amewaeleza wateule wake kuhusu wajibu wa Mawaziri katika Bunge akisisitiza kuwa ni wajibu wa kila waziri kuhudhuria vikao vyote vya Bunge, na kuwa ndani ya Bunge mawaziri wote wa Serikali lazima wawajibike kwa pamoja.

  “Ni muhimu ieleweke kuwa kama ilivyo kwa maamuzi ya Baraza la Mawaziri, uwajibikaji wa Mawaziri Bungeni ni wa Pamoja. Kwa hiyo, Hoja ya Serikali Bungeni ni Hoja ya Mawaziri Wote na siyo Waziri anayewasilisha hoja tu,” amesema Rais Kikwete.

  Rais pia amewakumbusha wateule wake kuhusu uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility) katika kuongoza nchi, akisisitiza kuwa uwajibikaji huo unaelezwa kwa ufasaha katika Hati Maalum (Instrument) ya Majukumu ya kila Wizara.

  Kuhusu uhusiano kati ya Waziri na Rais, na kati ya Waziri na Waziri Mkuu, Rais amesema kuwa pamoja na kwamba shughuli zote za utendaji Serikalini hutekelezwa kwa niaba ya Rais, lazima mawaziri wakumbuke kuwa Waziri Mkuu ndiye msimamizi wa shughuli za kila siku za Serikali.

  Rais Kikwete pia ametaka kujengeka mahusiano mazuri kati ya Waziri na Naibu Waziri wake akisisitiza: “Jambo la msingi la kuzingatia ni kwamba uhusiano mzuri baina ya viongozi hawa ni nguzo muhimu katika mafanikio ya Wizara. Kwa hiyo, ili kuepuka migongano katika utekelezaji ni muhimu mipaka ya kazi za Waziri na Naibu Waziri ikaheshimika na pia ni wajibu wa Waziri kumpangia kazi Naibu Waziri katika Wizara husika.

  Katika mkutano huo, Rais Kikwete pia amezungumzia uhusiano kati ya Waziri na Katibu Mkuu; uhusiano kati ya Waziri wa Nchi Asiyekuwa na Portfolio na Katibu Mkuu; uhusiano kati ya Naibu Waziri na Katibu Mkuu, na uhusiano kati ya Waziri na Waziri wa Sekta Nyingine.

  Rais Kikwete pia amefafanua kuhusu uhusiano kati ya Wizara na Wadau Wengine; uhusiano baina ya Wizara, Mikoa na Halmashauri; uhusiano na Taasisi Zilizo Chini ya Wizara; uhusiano na Wasaidizi wa Mawaziri pamoja na utekelezaji wa Maagizo ya Viongozi wa Kitaifa.
  Rais Kikwete pia amewaeleza Mawaziri na Naibu Mawaziri kuhusu nyaraka muhimu ambazo wanapaswa kukabidhiwa na kuzipitia watakapofika kwenye nafasi zao mpya za kazi. Nyaraka hizo ni pamoja na Taarifa ya Makabidhiano ya Ofisi, Katiba, Ilani ya Chama Tawala, Dira ya Taifa, na Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini (MKUKUTA).

  Aidha, Rais Kikwete amewaeleza wateule wake kuhusu umuhimu wao kufahamu Sera, Sheria, Kanuni, Taratibu, Mikakati, Mipangomkakati, Mpango na Bajeti ya Wizara, Mpango wa Kazi wa Wizara na Masharti ya Kazi ya Waziri.

  Rais Kikwete vile vile amekumbusha Mawaziri na Naibu Mawaziri wake kuwa suala la vita dhidi ya rushwa ni suala la kikatiba na kuwataka kuhakikisha kuwa Mpango wa Pili wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa (NACSAP-11) unatekelezwa.

  Pia amewataka Mawaziri kusimamia mapato ya Serikali yasiyotokana na kodi na kudhibiti matumizi ya Serikali.
  Rais Kikwete pia amewataka viongozi hao kuzingatia maadili ya uongozi ikiwa ni pamoja na kusimamia sheria za nchi, kuheshimu sheria katika shughuli na mambo yao binafsi na pia kutunza siri za Serikali kwa mujibu wa kiapo chao.

  Rais Kikwete pia amesisitiza umuhimu wa Mawaziri na Naibu Mawaziri kuwasiliana na wananchi kwa maana ya kueleza mafanikio ya Serikali na mipango ya Serikali katika kushughulikia matatizo ya wananchi.

  Amewataka kuvitumia kikamilifu Vitengo vya Mawasiliano ya Serikali katika wizara zao ambavyo ndivyo vyenye jukumu la kutoa taarifa kuhusu Wizara inavyotelekeza majukumu yake.

  “Uzoefu unaonyesha kuwa Mawaziri wengi ni wazito kufanya mawasiliano na wananchi hata pale ambako Wizara imefanya mambo mengi mazuri. Hivyo, Mawaziri muwe mstari wa mbele kuelezea mafanikio ya utendaji wa Serikali katika Wizara zetu,” ameelekeza Rais Kikwete na kuongeza:

  “Lazima ujengwe utamaduni wa kudumu wa kuwasiliana na wananchi wote ambao ndio waajiri wetu kupitia kura zao. Mawaziri wote tumieni Vitengo vyenu vya Mawasiliano na vyombo vya habari kwa ustadi ipasavyo,” amefafanua Rais Kikwete.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
  Ikulu,
  DAR ES SALAAM.

  29 Novemba, 2010
   
 9. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #9
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Hivi ni kwa nini waandishi hawakuwemo?
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hawakuwepo wapi kaka ? Vikao vya baraza la mawaziri ni siri. Hata hiyo habari iliyotolewa kwenye public ni just tip of iceberg kilichozungumzwa.

  Hapo ndipo wanatakiwa waandishi wadadisi ili kuwaonjesha wanachi kile kilichotokea na hawakuambiwa. Sasa kama hakuna chombo cha habari au mwandishi aliyejua kuwa tarehe 29 NOv kulikuwa na kikao cha CABINET.... ndio unaweza kujua uwezo wa waandishi wetu.

  SIRI- KALI.
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  hapo kwenye bold. hilo ni kosa lingine na matumizi mabaya ya fedha za serikali. naona kikwete hajajifunza makosa aliyoyafanya mwaka 2005 ambapo aliidhinisha fedha za umma kuwafanyia semina elekezi wateule wake halafu delivery ikawa inadequate. au atuthibitishie kwamba fedha ya semina elekezi itatoka mfukoni mwake kwani hakuna bajeti yake kwenye jedwali la bajeti ya serikali iliyopitishwa na bunge.

  Kikwete ana maneno mazuri ila matendo ndo yanamuumbua. mie bado sana kumwamini kwani ameshaanza kwa bad leg tegemee penalt kupigwa kwa dochi safari hii.
   
 12. M

  Mtu wa Mungu JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Bila shaka mkwere atakuwa amewatahadharisha mawaziri hawa kumkaba barabara kuzuia magoli ya kufungwa na Tundu Lissu na team yake mjengoni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mikakati ya kujiandaa kwenda Ngurudoto nini ? wakae vikao vya siri ila ukweli upo pale pale watu wawajibike na si porojo !
   
 14. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Shida sio kumuamini JK. Ipeni muda serikali mpya tuone itafanya nini. Tatizo watu mnataka matokeo wakati ndio kwanza dakika 47 second half.lol.. Tusiiumbue serikali changa kama hii. Tuipe 100 days kwanza alafu tuone upepo unaelekea wapi...
   
 15. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  JF pia ina waandishi na ni chombo cha habari
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  KUNA MTU ALICOMMENT KAMA WEWE 2005 HALAFU HAKUKOMMENT TENA 2010. tone la kwanza nalo ni sehemu ya mvua
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Apo anapotaka bungeni wawe wamoja nadhani anataka kuwanyamazisha baadhi ya watu apo!
   
 18. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Manaibu waziri hawapo kwenye cabinet lakini kwa kuwa hicho ni kikao cha kwanza nadhani rais aliona ni vema awakusanye wote na kuwaeleza hicho alichowaeleza. kwa hiyo, katika kipengele cha mahudhurio kwenye proceedings za kikao cha leo, mawaziri wanaorodhozeshwa kama cabinet members na manaibu waziri kama wajumbe waalikwa.
   
 19. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #19
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Semina elekezi za nini kama sio kumaliza pesa tu kwa mambo yasiyo ya msingi? wale ambao walifanya hizo semina elekezi mwaka ule kwa bilion kadhaa kule ngurdoto ndo tulipata nini? sitaki kusikia uji...
   
 20. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Yaani SEMINA ELEKEZI tena?
   
Loading...