Wacha1
JF-Expert Member
- Dec 21, 2009
- 16,681
- 8,233
Ulitaka wewe ndio uwe mshauri wake? Kila mtu ana kazi yake mwacheni JPM afanye kazi yake, baada ya miezi miwili ya kampeni nchi nzima bado unataka akurupuke, lazima ajiridhishe maana amepewa dhamana kubwa kuwaweka Mawaziri wenye uwezo wa kuwavusha Watanzania.Kuna jambo sio la kawaida linaendelea kwa sasa. Baraza la Mawaziri kwa Serikali yeyote ndio timu ya nchi katika utawala na chombo muhimu sana katika maendeleo ya nchi.
Lakini jambo la ajabu ni kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 Rais Magufuli amechukua zaidi ya wiki tatu hajataja baraza lake na tofauti na zamani jambo hilo lilipokuwa la muhimu, sasa hivi hakuna hata mwenye kufuatilia au kushauri nani awe nani katika baraza.
Je, kukosekana msisimko huo ni ishara kuwa baraza chini ya JPM huwa ni muhuri tuu? Au ni upotevu wa pesa kwani hata wasipokuwepo hakuna tofauti?