Baraza la Mawaziri la Rais Mgufuli mbona Raia Wamelipotezea?

Tena Mimi namshauri Rais Dk. Magufuli asiliteue hadi hata baada ya miaka Miwili hivi kwani Makatibu Wakuu wapo na Nchi itaenda vyema vile vile.
Makatibu wetu ni Wakuu wanaoteuliwa na Rais aliye madarakani siyo Wakudumu (Permanent) ambao hubaki kwenye nafasi zao hata Serikali ikibadilika ikaja ya Chama kingine. Rais baada ya kuteua Mawaziri anateua Makatibu Wakuu na watendaji wengine mpaka Makatibu Tarafa ndo maana Rasimu ya Warioba ilipendekeza apunguziwe madaraka ili ateue wa karibu yake tu aweze kufuatilia utendaji kazi wao. Hii ingesaidia asilale na majalada ya Watendaji wake!
 
Hayo ndo maoni sahihi ila ungeongezea ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Baraza ni mzigo tu kwa walipa kodi na maisha yanaweza kuendelea kama kawaida bila wao mpaka Uchafuzi mwingine. Ni karibu mwezi sasa wananchi hawajui kama Mwenyekiti mwenye jukumu la kuunda Baraza lake yupo Chamwino, Dar es Salaam au Chato. We don't miss them, we can do without them!
Uko sahihi kabisa wao wanakula mema ya nchi huku raia tunapambana na Hali zetu na hamna unafuu wowote tunaoupata kimaisha twasogeza tu siku za kuishi
 
Kuna jambo sio la kawaida linaendelea kwa sasa. Baraza la Mawaziri kwa serikali yeyote ndio timu ya nchi katika utawala na chombo muhimu sana katika maendeleo ya nchi.

Lakini jambo la ajabu ni kuwa baada ya uchaguzi Mkuu wa 2020 Rais JPM amechukua zaidi ya wiki tatu hajataja baraza lake na tofauti na zamani jambo hilo lilipokuwa la muhimu, sasa hivi hakuna hata mwenye kufuatilia au kushauri nani awe nani katika baraza.

Je, kukosekana msisimko huo ni ishara kuwa baraza chini ya JPM huwa ni muhuri tuu? Au ni upotevu wa pesa kwani hata wasipokuwepo hakuna tofauti?
Mbona alishasema hatateua mawaziri mapema. Hivyo watz wanajua mkuu!
 
Tena Mimi namshauri Rais Dk. Magufuli asiliteue hadi hata baada ya miaka Miwili hivi kwani Makatibu Wakuu wapo na Nchi itaenda vyema vile vile.
Nchi haiendeshwi kwa mhemko au upepo unaendaje, Bali sheria na katiba.
Uwepo wa mawaziri na utendaji wao uko kikatiba lazima ufuatwe. Na yapo maamuzi ya kuendesha nchi lazima yafanyike kwa pamoja ndani ya baraza LA mawaziri, jee hayo yanafanyikaje kwa sasa? Au ndio kwamba nchi iko katika control ya MTU mmoja?
 
Kwani baraza la mawaziri linatusaidia nini, mbona tunafanya kazi zetu bila shida tu?
Nadhani ikipita tafiti ya nchi IPI imejaa mafala au inaongoza duniani lazima TZ ichukue uongozi kutokana na watu wa aina hii
 
Mpango katubu mwenyewe juzi wakati anaapishwa kuna umaskini kufuru hapa tanzania sasa hao mawaziri ni mzigo tuu kuongeza gharam za nchi..wabunge pia ni mzigo tuu 350+ hizo hela zote za nn akati tungeweka tu mbunge mmoja kila mkoa angetosha...hatuwezi kutajirika kama uongozi unatumia karibu nusu ya bajeti ya nchi kwajili ya mishahara na posho yan nonsense utafikiri hakuna wachumi wasomi hii nnchi hovyo kabisa
 
Kuna jambo sio la kawaida linaendelea kwa sasa. Baraza la Mawaziri kwa Serikali yeyote ndio timu ya nchi katika utawala na chombo muhimu sana katika maendeleo ya nchi.

Lakini jambo la ajabu ni kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 Rais Magufuli amechukua zaidi ya wiki tatu hajataja baraza lake na tofauti na zamani jambo hilo lilipokuwa la muhimu, sasa hivi hakuna hata mwenye kufuatilia au kushauri nani awe nani katika baraza.

Je, kukosekana msisimko huo ni ishara kuwa baraza chini ya JPM huwa ni muhuri tuu? Au ni upotevu wa pesa kwani hata wasipokuwepo hakuna tofauti?
Ingia shambani ulime mvua zinanyesha.Ya serikali mwachie rais.Accounting Officers wa wizara ni Katibu Mkuu waziri n mwanasiasa. Muda wa siasa umekwisha sasa ni Kazi tuuu.
 
Kuna jambo sio la kawaida linaendelea kwa sasa. Baraza la Mawaziri kwa Serikali yeyote ndio timu ya nchi katika utawala na chombo muhimu sana katika maendeleo ya nchi.

Lakini jambo la ajabu ni kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 Rais Magufuli amechukua zaidi ya wiki tatu hajataja baraza lake na tofauti na zamani jambo hilo lilipokuwa la muhimu, sasa hivi hakuna hata mwenye kufuatilia au kushauri nani awe nani katika baraza.

Je, kukosekana msisimko huo ni ishara kuwa baraza chini ya JPM huwa ni muhuri tuu? Au ni upotevu wa pesa kwani hata wasipokuwepo hakuna tofauti?
Watu wanajua Magufuli atakuwa Waziri wa Wizara zote, hao mawaziri watakuwa vikaragosi tu.
 
Kuna jambo sio la kawaida linaendelea kwa sasa. Baraza la Mawaziri kwa Serikali yeyote ndio timu ya nchi katika utawala na chombo muhimu sana katika maendeleo ya nchi.

Lakini jambo la ajabu ni kuwa baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2020 Rais Magufuli amechukua zaidi ya wiki tatu hajataja baraza lake na tofauti na zamani jambo hilo lilipokuwa la muhimu, sasa hivi hakuna hata mwenye kufuatilia au kushauri nani awe nani katika baraza.

Je, kukosekana msisimko huo ni ishara kuwa baraza chini ya JPM huwa ni muhuri tuu? Au ni upotevu wa pesa kwani hata wasipokuwepo hakuna tofauti?

Ngoja atengeneze blue print na makatibu wakuu kwanza, mawaziri wakija wanaelekezwa cha kufanya
 
Hakuna haraka.

1. Hujui Baraza la Sasa ni la muhimu Sana KWA ajili ya uchaguzi wa 2025? Hasa nafasi ya Waziri mkuu ajaye?

2. Hujui wabunge wote ni wa CCM Sasa kuchagua ni kaazi Sana. wako wengi...

3. Hujui karibu wote waliomaliza wamefanya vizuri.......Sasa ni Kazi kuwaacha. Mf. Ummy. Ndalichako. Jafo. Kalemani. Bashungwa. Lukuvi. Mbarawa. etc

Nafasi wazi ni wizara kama

1. Waziri michezo..utamaduni na sanaa
2. Mambo ya ndani.
3. Ulinzi.

Nyingine warudi tu wale wale
 
Mm baada ya uchaguzi sitaki kusikia kinacho endelea ama kinacho ongelewa coz hakuna haki
 
Ninavyosemaga hapa kuwa Watanzania ni magoigoi huwa sitanii.Nakuhakikishia hata kama Magufuli ataendesha hii nchi kwa mwaka mzima bila baraza la mawaziri wala hutasikia chochote kutoka kwa wananchi.Yaani wananchi kwao kila kitu ni sawa tu,kiwe kina manufaa kwa nchi,kiwe hakina manufaa kwa nchi au kiwe cha kuliangamiza Taifa kwao ni sawa tu.Ni magoigoi haswa!
Hata Watanzania wakiongea au kulalamika nani atawasikiliza?Na hata wakisikilizwa nani ataamua kwa mapenzi yao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom