Baraza la Mawaziri Kutangazwa Leo...Tetesi za Wanaotajwa Sura Mpya...

Nasikiliza Clouds sasa hivi kwamba Baraza La Mawaziri huenda likatajwa muda wowote leo hii na baadhi ya wanaotajwa katika sura mpya ni David Mwakyusa, Anne Kilango, Jenista Mhagama, Pindi Chana, Abdallah Kigoda, na Dalali Kafumu

My Take: staili ya JK si kama ya Nkapa, maana hata tetesi za kuvunjwa kwa Baraza zilishauwa hewani.. ngoja 2one

Mkuu tendea haki uanachama wako hapa JF.. Hcho kipindi hata mimi nakisikiliza, hakuna aliyewataja hao.. Au we umesikia wapi? Au umesikiliza redio kwa sekunde kadhaa na kusikia hayo majina basi ukadhani ndio wanaotajwa tajwa.. Be smart mkuu sikiliza kwa makini ndo ulete uzi.. Usikurupuke!

Si kila wakati tuanzishe thread kama hatuna sensitive and proven issues especialy wen we post abt current poltcal situation in tz.. We better organize ourselves first, otherwise let's fall into cht chat forum.
 
Nasikiliza Clouds sasa hivi kwamba Baraza La Mawaziri huenda likatajwa muda wowote leo hii na baadhi ya wanaotajwa katika sura mpya ni David Mwakyusa, Anne Kilango, Jenista Mhagama, Pindi Chana, Abdallah Kigoda, na Dalali Kafumu

My Take: staili ya JK si kama ya Nkapa, maana hata tetesi za kuvunjwa kwa Baraza zilishauwa hewani.. ngoja 2one

Duh , hivi hamjui nyie wakati mwakyusa yupo wizara ya afya aliingiza madawa na kusaidia watu kutolipa kodi! na ndio chanzo cha yeye kutemwa! ni mlafi na hana lolote jipya! yaani kama JK atamrudisha nitamuona wa ajabu! ana madudu mengi aliyafanya wakati yupo wizara ya afya.

Anne Kilango, huyu ni FISADI NAMBARI WANI! nani aiejua, alileta kidomo domo sana wakati ule mumewe alipotemwa kwenye urais, akatolea hasira zake zote bungeni kwa kupiga kelele! na alishaanza kujitangaza kwamba yeye ni FIRST LADY, nani asiejua kule dodoma wakati wa kuchagua mgombea urais na akashushuka baada ya jina la mumewe kutopitishwa , na juzi mbona hatukumuona katika vote of no confidence ! hapa nooo! tena BIG nooo!

Jenista Muhagama ! ni FISADI PIA ! hawa wote ndio wanaoendekeza posho! kwanza nashangaa kwanini posho HAZIFUTWI? itautwe njia ambayo mtu kugombea Ubunge iwe ni kazi ya kujitolea ambayo watalipwa mishara na hizi posho zifutwe halafu tuwaone ! hii nchi inatia kichefu chefu kwa kweli!

sioni hata mmoja anaefaa... huyu MAgufuli kakma ndio PM si ATATUCHARAZA VIBOKO njiani huyu ! no no no !
 
Watanzania tusirudie kumpata Rais wetu ajae kwa namna tulivyompata JMK. Tangu 2005 alipochaguliwa amelazimika kuunda Cabinet ya matapeli, wezi, wahuni, fisadi akawa Waziri Mkuu, fisadi mwingine akawa mwekahazina wa CCM,..., akajaribu kuibadili Cabinet hii mwaka 2008. Akawapandisha vibaka wengi akina Ngeleja, Malima, Mkullo, Maige,....,
Sasa atajaribu tena kuunda Baraza lingine labda aibadili ile Tume ya Katiba ndio iwe Cabinet yake mpya!
 
Musa Azzan Zungu, waziri wa ulinzi.

Mohamed Dewji, waziri wa biashara na viwanda.

Majimarefu, waziri wa afya.

Omar Nundu, aendelee kufichuwa madudu.
 
Nasikiliza Clouds sasa hivi kwamba Baraza La Mawaziri huenda likatajwa muda wowote leo hii na baadhi ya wanaotajwa katika sura mpya ni David Mwakyusa, Anne Kilango, Jenista Mhagama, Pindi Chana, Abdallah Kigoda, na Dalali Kafumu

My Take: staili ya JK si kama ya Nkapa, maana hata tetesi za kuvunjwa kwa Baraza zilishauwa hewani.. ngoja 2one
Kwa hiyo, hiyo ndiyo Cream ya ccm iliyobaki? hahaha...Mnahatari...
 
Ukiangalia kati ya Wabunge wa CCM waliopo, ambao yapasa Mawaziri watoke humo hutaona yeyeto afaaye na usishangae Prof Majimarefu (mtambikaji wa CCM), Mwigulu Nchemba (mwagamwaga/mtoa rushwa) na Ayeshi ndio wakateuliwa kuwa Mawaziri.
Hapo ndipo yale mapendekezo kuwa Wabunge wasiwe Mawaziri linapota umuhimu.
 
Musa Azzan Zungu, waziri wa ulinzi.

Mohamed Dewji, waziri wa biashara na viwanda.

Majimarefu, waziri wa afya.

Omar Nundu, aendelee kufichuwa madudu.

Hapo utaona JK amechagua bonge la cabinet!
Huwa sishangai jinsi unavyoiteteaga CCM na serikali yake.
 
Ha ha ha haa, Mwigulu? Huyu anayeshindwa hata kujieleza hapa JF? Kama ndo hivyo bora baraza libaki hilohilo lililopo tu. Naona CCM ishaishiwa man power hivi sasa. Mtaji mzuri upo CHADEMA kuliko hata CCM kwenyewe. Sioni kipya katika orodha hiyo. Eti hadi Kilango, mnafiki huyo?
Mwigulu!!! wake za watu HAZINA na wizarani kaeni mkao wa kula. Waume zenu watajinyonga!!! kwa KIDUME cha mbegu kukabithiwa rungu!!
 
Hii ktk lugha ya bible tunaiita kuweka mvinyo mpya kwenye majagi/maprastic ya zamani!
Watu wanaweza kuwa wapya ila mfumo na chama ni kile kile
 
Nasikiliza Clouds sasa hivi kwamba Baraza La Mawaziri huenda likatajwa muda wowote leo hii na baadhi ya wanaotajwa katika sura mpya ni David Mwakyusa, Anne Kilango, Jenista Mhagama, Pindi Chana, Abdallah Kigoda, na Dalali Kafumu

My Take: staili ya JK si kama ya Nkapa, maana hata tetesi za kuvunjwa kwa Baraza zilishauwa hewani.. ngoja 2one
Hivi huyu Abdalla Kigoda huwa ana nguvu gani kwenye siasa za TZ????maana huyu jamaa amekuwepo tangu enzi za Mkpa...infact sera mbovu za ubinafsishaji zinazopigiwa kelele leo ziliasisiwa na huyu jamaa wakati akiwa tume ya mipango na kina Ngasongwa enzi za Mkapa......actually huyu jamaa naye alikula EPA.........leo hii bado tunasikia anataka kurudishwa kwenye uwaziri!!!...hivi TZ imelaaniwa!!!!!!...hata mtu asiyemjua Kigoda personally anaweza kujua mambo yake kwenye mitandao.......maana uozo wake wajulikana sana......hawa ndio waasisi wa EPA.....leo hii jamaa tunasikia tetesi anataka kurudi kweli????.....ebu msomeni hapa..Abdallah Omar Kigoda - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Katika Bunge la Sasa, Kikwete ana kama watu 70 tu anaoweza kuwachagua kwenye baraza lake la mawaziri iwapo utawatoa

1. Wabunge wa kuteulia na Rais, viti maalum vya wanwake na wa Baraza la Wawakilishi

2. Wabunge CCM kutoka Zanzibar

3. Wabunge wa vyama vya Upinzani

3. Wabunge waliopo kwenye baraza la Mawaziri la Sasa

4. Wabunge waliokuwemo kwenye Mabaraza yaliyopita na

5. Wabunge aina ya Professa Maji Marefu na Lusinde


Kikwete hana choice, maana wabunge tuliowachaguwa wananchi kuwaingiza bungeni hawakidhi sifa za kuwa mawaziri

*Katiba mpya impe madaraka Rais ya kuchagua watu nje ya Bunge kushika nyadhifa hizo

Nimeipenda hii;
imekaa kichambuzi!
 
wenzetu mna moyo kweli; wanaondolewa wana CCM wanarudishwa wana CCM, sera zile zile, chama kile kile, ilani ile ile, watu wale wale! Kama Kigoda akirudishwa si alishakuwemo humo? I'm really indifferent kwa vyovyote watakavyofanya!

Kweli mzee wetu, UPUMBAVU ni kufanya kitu kilekile kwa njia ileile na style ileile huku ukitegemea matokeo tofauti

 
Huyo kigoda sitaki hata kumsikia wakimrudishe tena kweli tutajua ccm wameishiwa watu.Alipiga pesa sana enzi za ubinafsishaji enzi za mkapa na ndo alikuwa postermaster wake kumpelekea pesa mzee tena leo wamrudishe.
'


Kigoda kwa sifa hiyo tu kuna possibility kubwa sana akaukwaaa uwaziri wa fedha

"
Kigoda, Basil Pesambili, Juma Ngasongwa, Rostam Aziz, Lowassa the then PM and others are said to be behind EPA scam under which Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania's ruling party stole billions of shillings from the central bank to finance its elections that saw Jakaya Kikwete win"
 
serikali itakuwa ile ile na madudu yale yale,,,, na ninasema hili kwa kuwa tatizo si aina ya watu watakaoteuliwa kuwa mawaziri bali ni mfumo uliopo ambao unaruhusu mianya mingi ya rushwa na kutowajibika.. na kwa mtazamo wangu tusitegemee mapya kutoka baraza jipya hata wakiwekwa wapya wote,,,, tutapata baraza lenye kuwajibika kama mfu wa uongozi ndani wa CCM na serikali....
 
Back
Top Bottom