Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Kumbuka akina Komu na Selasini walihamia NCCR lakini Mambo yakawa magumu, na Kuna tetesi Selasini anaweza kurudi chadema. Pia kumbuka kwamba hata ACT tayari Kuna watu huko wamejipanga na Wana vyeo huwezi kwenda huko tu ukapewa nafasi na ukawa na usahwishi Kama ulio kuwa nao chadema.
Salama yao kurudi ccm ingawa huko nako jiwe ndio alikuwa anagawa vyeo kwa mamluki nowadays wenye chama wamekaza
Mpaka dakitari wa mihogo anamaliza hou Media ili asikike kuwa yupo lkn wapiii watawala waliopo wamemkazia
watu wakumbuke walikotoka na waheshimu bila chadema nani alimjua Slaa .. Zitto au Halima na wasaka fursa wenzie
 
Ndugu elewa kwamba walikata Rufaa kupinga kufukuzwa uanachama. Ndio maana ilibidi baraza kuu likae na kujadili Rufaa yao na baadae kutoa maamuzi.
Kikao kinapaswa kuketi baada ya mda ganiii, pindi kipatapo barua ya rufaa??
 
HALIMA MDEE NA WENZAKE 18 WAFUKUZWA RASMI CHADEMA

Baraza Kuu la #CHADEMA limezitupilia mbali Rufaa za Halima Mdee na wenzake 18 wakipinga kufukuzwa uanachama na Kamati Kuu ya chama hicho kwa kukubali kwenda kuapishwa na kuwa wabunge wa Viti Maalumu bila baraka za chama
======
UPDATE:

View attachment 2221145

Halima Mdee: Kilichofanyika ni Uhuni, hata Mbowe (Freeman) mwenyewe anajua

John Mrema: Baada ya uamuzi wa Baraza Kuu, Katibu Mkuu ataandika barua kumuarifu Spika kuwa suala lao limehitimishwa; tutamwachia spika afanye uamuzi kama alivyosema anasubiri Rufaa zao
=======

Matokeo ni kama ifuatavyo;

Kanda ya Victoria (Wajumbe 44)
-Wanaokubalia wavuliwe uwanachama 42
-Wasiokubali 1
-Wasiofungamana na Upande wowote 1
Jumla kura 44

Kanda ya Nyasa (Wajumbe 57)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 57
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 57

Kanda ya Unguja (Wajumbe 22)

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 19
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 1
Jumla ya Kura 22

Kanda ya Pemba 15
-Wanaokubali wavuliwe uanachama 12
-Wasiokubali 1
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 15

Kanda ya Kusini 32

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 32
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 32

Kanda ya Pwani 47

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 45
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 2
Jumla ya Kura 47

Kanda ya Kati 44

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 44
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 44

Kanda ya Serengeti Wajumbe 41

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 41
-Wasiokubalina 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 41

Kanda ya Magharib Wajumbe 37

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 37
Wasiokubali 0
Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 37

Kanda ya Kaskazini Wajumbe 61

-Wanaokubali wavuliwe uanachama 61
-Wasiokubali 0
-Wasifungamana na Upande wowote 0
Jumla ya Kura 61

Kura 352 zimekubaliana na Kamati Kuu na kura 5 ndo zimepingana na maamuzi ya Kamati Kuu
This is CHADEMA..Mungu zidi kukibariki hiki chama..
 
Walivuna walichopanda walikuwa wanapewa kiburi na mwendazake na Ndugai leo wako wapi?
 
Inapendeza wadada wakienda ACT ili ulaji wao uendelee! for me wahuni at work!

sijawahi kuwaona kama chama bali genge flani tu la kusaka "mawe" mjini.

ni kawaida ukikulia Chuga kupata hela ni must ila tumia njia yoyote. Yaani the end justify the means!

ukiwa na akili peleka mtoto wako akulie kule Chuga utashangaa akikua anavyopenda pesa kuzidi Bwana Makengeza!!
 
Watamkuta Kibatala kwenye geti la Kisutu.
Hata wakienda mahakamani ni kusogeza muda tu,ni bora kukaa pembeni kuheshimu maamuzi ya chama.Labda kuna siku wakasamehewa kabla ya 2025 wakajipanga upya kuwania nafasi za uongozi.
Lakini pammoja na hayo wamekitumikia chama,na kupitia vikwazo vingi,kusweka ndani mara kwa mara na kufunguliwa kesi za kubumba.
 
Acha kupanikiii. Mahakama inazingatia sheria. Hivyo lazima katiba ya chadema ichukuliwe na kisha isomwe ilikubaini kama kama haki inafuatwa kwa mjibu wa katiba ya chadema. Na muache kupaniki kabisaa
Yaani mwenyekiti atoke kuongea na mkuu wa muhimili uliojichimbia zaidi then eti mahakama?
 
Hata wakienda mahakamani ni kusogeza muda tu,ni bora kukaa pembeni kuheshimu maamuzi ya chama.Labda kuna siku wakasamehewa kabla ya 2025 wakajipanga upya kuwania nafasi za uongozi.
Lakini pammoja na hayo wamekitumikia chama,na kupitia vikwazo vingi,kusweka ndani mara kwa mara na kufunguliwa kesi za kubumba.
Acheni kuwakandamiza kwa kuwatishia wanasheria wenu kandamizi dhidi ya akinamama. Kwenda mahakamani ni haki yao. Acheni kuwatisha, etiwatulie mbeleni mtawasamehe kwa kosa lipi mpaka waombe msamahaa. Tunataka sheria ichunguze na itoe hakiii
 
Back
Top Bottom