Baraza Kuu la CHADEMA laridhia kufukuzwa kwa Halima Mdee na wenzake 18. Asilimia 97.6 waafikiana na maamuzi

Bunge ndo litaamua....sheria za Tanzania zina gaps nyingi. Hapo Tulia Mwansasu ashapata kipengele cha kuwalinda kabla hata ya hilo Baraza lao kukaa
Na awalinde tu, mbowe anasema alimtafutia mdee kazi, Je vipi hao wengine 18 nao aliwatafutia kazi?
Chama cha kibaguzi Sana!
 
View attachment 2221957

Uwezi kuwa na taratibu za kufukuza watu kinyume na sheria, hayo mambo yote ya kwenye vyama vya siasa sijui katiba zao zinasema nini ni taratibu za utekelezaji wa sheria tu kwa mtindo wao.

Sasa kwenye misconduct taratibu za kufukuzana kwa mtu anaetaka haki itendeke inabidi awepo na neutral party kwenye kusikiliza pande mbili. In this instance labda the neutral party ni wawakilishi kutoka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa washirikishwe kusikiliza accusation za pande mbili.

Lakini kwenye dismissal process ambazo jaji mwenyekiti wa chama, prosecutors mwenyekiti wa chama na genge lake la wahuni na jurors wapo mfukoni kwa mwenyekiti; uende au usiende kwenye dispute resolution kama hiyo matokeo yapo wazi.

Sasa kama ni victim either ukubali kama Membe au upambanie haki yako mahakamani kama Zitto.

Binafsi naona unyanyasaji wa hakina mama nchi hii umekithiri ni kwenda mahakamani tu.
Yaani walivyofukuzwa Membe na Sophia hizi insha hamkuandika kabisa, nchi hii ni ccm pekee mwenye haki ya kufukuza wanachama wake lakini sio vyama vingine
 
Wabaki na kuomba uanachama upya, Watanzania na hususani Wana CDM watawaelewa wakiomba radhi kufuatia siasa za chuki visasi Mwendazake.
Nyinyi chuki mmeshatengeneza juu Yao, hamna namna mtawasamehe, mwenzenu yeriko pamoja na malisa walianza kwa kuwananga hata kabla ya kikao kuitishwa Leo anawalaumu kwa kutoomba msamaha walipipewa nafasi ( luckily they are all so intelligent, wanajua huwezi gonga hodi sememu ambayo unajua watu hawapo ).
Unafiki unaanzia hapo,
 
Bila shaka wewe ni mume wa Halima
 
Mkuu Matola , kwenye uteuzi wa wabunge WA viti maalum, kila chama kina utaratibu wake wa ndani, kwa Chadema ni CC ya Chadema kwanza kwa kila mjumbe kuleta watu wake, ndio maana ulikuta mtu anamleta mwanae wa kike, na mke wa mtoto wake wa kiume hivyo bungeni wako Baba, mtoto na mkwe!. Lisu na Zitto wakaleta dada zao!. Wajumbe wengine wake zao na kwa baadhi ya viongozi wakaleta hadi vidumu vyao!, ambavyo havichangii hoja yoyote mule Bungeni zaidi ya kutoa tuu zile huduma za kibinaadamu!.

Majina hayo huwasilishwa NEC 30 days kabla ya uchaguzi in order of preference.
Baada ya uchaguzi, NEC hufanya calibration ya kura za urais na kukokotoa idadi ya viti maalum kutoka kila chama na kuwaandikia barua vyama vi confirm uteuzi. Chadema responded kwa barua halali, yenye headed paper ya Chadema na signature ya office bearers.

NEC ikafanya uteuzi na kumpa Spika majina. Katibu Mkuu, JJ.Mnyika, huyu ni Nyerere type, hakuleta jina la ndugu yake yoyote, mke au kidumu, akashangaa barua hiyo ya uteuzi imeandikwa na nani na kusainiwa na nani wakati yeye ndiye KM na hakuandika!. Akaliamsha!. Ukweli barua ya uteuzi ipo ni bonafide genuine, ina bonafide genuine headed paper ya Chadema, ina bonafide genuine signature ya office bearers, hivyo hakuna forgery yoyote ndio maana hawakuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike!. Na kikao cha Baraza Kuu, hakikufanya and due diligence yoyote kujiridhisha CC did the right thing zaidi ya kuyabariki maamuzi ya CC ya Chadema.

Chadema ina katiba yake yenye miongozo yote ya nidhamu, kwanini haikufutwa?. Ule ni Ukangaroo!.

Kama ilivyo kwa Zitto as NKM na Halima Mdee as Mwenyekiti wa Bawacha, hawa wanachaguliwa na Baraza Kuu, ndilo mamlaka yake ya nidhamu, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtiimua Zitto na sasa Halima?!. Huu ni Ukangaroo!.

Kiukweli karma imekuwa iki washughulikia Chadema collectively as chama na kuwashughulikia viongozi wake individually!. Why now add an insult to an injury?.

Karma is real!.
P
Sikutegemea kama hili linaweza kuwa andiko lako, Paskali hivi ni kweli hujui viti maalum cdm vinapatikanaje? Kuhusu ndugu au wapenzi kuwa bungeni ni cdm ndio waanzilishi? Ccm haikuwahi kutokea familia kuwa bungeni? Zito alikuwa anatembea na mtoto wa bulembo mbona hamkuandika haya? Bulembo na mwanae walikuwa bungeni mbona ulikaa kimya? Acha unafiki kaka ukweli unaujua nafsini kwako
 
Jikite kwenye hoja, mbowe amekiri kumuita mdee na bulaya na kumuahidi kumtafutia kazi mdee, vipi hao wengine 18?
Wapi iliandikwa lazima awatafutie kazi wote? Kama hizo kazi wenye sifa walikuwa hao tu kwanini aite wengine?
 
Sikutegemea kama hili linaweza kuwa andiko lako, Paskali hivi ni kweli hujui viti maalum cdm vinapatikanaje? Kuhusu ndugu au wapenzi kuwa bungeni ni cdm ndio waanzilishi? Ccm haikuwahi kutokea familia kuwa bungeni? Zito alikuwa anatembea na mtoto wa bulembo mbona hamkuandika haya? Bulembo na mwanae walikuwa bungeni mbona ulikaa kimya? Acha unafiki kaka ukweli unaujua nafsini kwako
Ukitaka kwenda vizuri na wanafki na mandumilakuwili unakwenda nao taraatiibuu, mpaka wanaingia king wenyewe, usiwe na haraka niachie mimi huyu.
 
Mkuu Matola , kwenye uteuzi wa wabunge WA viti maalum, kila chama kina utaratibu wake wa ndani, kwa Chadema ni CC ya Chadema kwanza kwa kila mjumbe kuleta watu wake, ndio maana ulikuta mtu anamleta mwanae wa kike, na mke wa mtoto wake wa kiume hivyo bungeni wako Baba, mtoto na mkwe!. Lisu na Zitto wakaleta dada zao!. Wajumbe wengine wake zao na kwa baadhi ya viongozi wakaleta hadi vidumu vyao!, ambavyo havichangii hoja yoyote mule Bungeni zaidi ya kutoa tuu zile huduma za kibinaadamu!.

Majina hayo huwasilishwa NEC 30 days kabla ya uchaguzi in order of preference.
Baada ya uchaguzi, NEC hufanya calibration ya kura za urais na kukokotoa idadi ya viti maalum kutoka kila chama na kuwaandikia barua vyama vi confirm uteuzi. Chadema responded kwa barua halali, yenye headed paper ya Chadema na signature ya office bearers.

NEC ikafanya uteuzi na kumpa Spika majina. Katibu Mkuu, JJ.Mnyika, huyu ni Nyerere type, hakuleta jina la ndugu yake yoyote, mke au kidumu, akashangaa barua hiyo ya uteuzi imeandikwa na nani na kusainiwa na nani wakati yeye ndiye KM na hakuandika!. Akaliamsha!. Ukweli barua ya uteuzi ipo ni bonafide genuine, ina bonafide genuine headed paper ya Chadema, ina bonafide genuine signature ya office bearers, hivyo hakuna forgery yoyote ndio maana hawakuripoti polisi ili uchunguzi wa kijinai ufanyike!. Na kikao cha Baraza Kuu, hakikufanya and due diligence yoyote kujiridhisha CC did the right thing zaidi ya kuyabariki maamuzi ya CC ya Chadema.

Chadema ina katiba yake yenye miongozo yote ya nidhamu, kwanini haikufutwa?. Ule ni Ukangaroo!.

Kama ilivyo kwa Zitto as NKM na Halima Mdee as Mwenyekiti wa Bawacha, hawa wanachaguliwa na Baraza Kuu, ndilo mamlaka yake ya nidhamu, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtiimua Zitto na sasa Halima?!. Huu ni Ukangaroo!.

Kiukweli karma imekuwa iki washughulikia Chadema collectively as chama na kuwashughulikia viongozi wake individually!. Why now add an insult to an injury?.

Karma is real!.
P
Nataka twende taratibu ili tuelewane, sitoandika magazeti hapa ila maswali machache tu naomba majibu.

Je ni kweli vijana hawa Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee na Joseph Mbilinyi Sugu ni product za Mbowe?

Wakati unanijibu swali hilo hapo juu naomba unijibu Nusrat Hanje alikuwa jela ana kesi isiyokuwa na dhamana alitoka vipi jela straight kwenda kwenye garage ya bunge kuapishwa?

Na wakati unajibu hayo maswali mawili hapo juu nakukumbusha tu Halima mdee alikuwa mgombea wa jimbo na mwenyekiti wa Bawacha alikuwa lazima apate uteuzi asingetumika.

Kama huelewi nakukumbusha viti maalum chadema walikuwa wakisubiri mrejesho wa majimbo uko vipi ili waliogombea majimboni na kushindwa pia wapewe kipaumbele.

Mimi nilianza kuwa na mashaka na wewe na hiden ajenda zako tangu siku ya msiba wa Regia Mtema R.I.P, nadhani unakumbuka au tuseme yule alikuwa Pasco?
 
Mdogo mdogo ndio mwendo, tutafika kiuhakika zaidi.
Je ni kweli vijana hawa Zitto Kabwe, John Mnyika, Halima Mdee na Joseph Mbilinyi Sugu ni product za Mbowe?
Hao watatu ukimuondoa Sugu, wote walikuwa UDSM pamoja, hivyo it's true, wamejiunga Chadema enzi za Mbowe, Zitto toka mama yake ni Chadema, Zitto na Halima Mdee ni madenti wa chuo, mambo ya madenti utakuwa unayajua. Sugu alivutiwa na Zitto.
Wakati unanijibu swali hilo hapo juu naomba unijibu Nusrat Hanje alikuwa jela ana kesi isiyokuwa na dhamana alitoka vipi jela straight kwenda kwenye garage ya bunge kuapishwa?
Aliachiwa kwa nolle, akatoka akaapishwa. Mtu kuwa mahabusu hakuzuii uteuzi.
Na wakati unajibu hayo maswali mawili hapo juu nakukumbusha tu Halima mdee alikuwa mgombea wa jimbo na mwenyekiti wa Bawacha alikuwa lazima apate uteuzi asingetumika.
Uteuzi gani tena wakati barua ya uteuzi kutoka Chadema kwenda NEC iliyopitisha majina yao ipo!.
Kama huelewi nakukumbusha viti maalum chadema walikuwa wakisubiri mrejesho wa majimbo uko vipi ili waliogombea majimboni na kushindwa pia wapewe kipaumbele.
Wakisubiri kwa Nani?!. Barua yao ya uteuzi ni legit, bonafide genuine!.
Mimi nilianza kuwa na mashaka na wewe na hiden ajenda zako tangu siku ya msiba wa Regia Mtema R.I.P, nadhani unakumbuka au tuseme yule alikuwa Pasco?
Pasco wa JF, ni jina la enzi zile za ujana, sasa ni Mzee Paskali. Pasco ana hidden agenda gani na Chadema, mimi masikini wa Mungu?!.
Na mimi naomba nikuulize swali moja.
Kwa mujibu wa katiba ya Chadema, mamlaka ya nidhamu ya M/Kiti wa Bawacha na NKM ni Baraza Kuu, CC ya Chadema, ilipowafuta uanachama, imewafuta kwa mamlaka gani?!.
P
P
 
Kila Nikiwafikiria WABUNGE 19 walivyokuwa na MAPENZI Makubwa na CHADEMA Nashindwa kuelewa nini kiliwapata mpaka wakafikia hayo MAAMUZI.Nikifikiria MATESO waliyoyapata wakati Wakienda Kumtoa MBOWE Gerezani ya Kupigwa na ASKARI wa MAGUFULI na kupelekea kuvunja Mikono na pia Kupora UBUNGE wao SIKUTARAJIA kama Wangeweza kukaa Meza moja na MAGUFULI na kukubali KUKISALITI CHAMA CHAO kwa MALIPO ya UBUNGE
Ndio maana NAULIZA ni NANI ALIWAROGA hawa WADADA?
1652327090551.jpg

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom