Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...

Baraza Jipya la Mawaziri hili hapa...

sarakasi zinaendelea maana wengi humo sio waadilifu. mtaona watakavyotenda
 
Mh! HUyo Nchimbi eti kapewa wizara ya habari na michezo, anajua nini kuhusu habari yule jamaa?
 
Wanabodi,

Hatimaye Baraza jipya la Mawaziri ndio lianza kutangazwa sasa live kupitia TBC!
Endelea kufuatilia...

UPDATES:

  • Wizara ya maji imeunganishwa na Kilimo - Itakuwa Wizara ya Kilimo na umwagiliaji!
  • Kazi ajira na vijana - kitengo cha vijana kimehamishiwa michezo na utamaduni
  • Uwezeshaji wa wananchi (Baraza la uwezeshaji) - Ilikuwa wizara ya fedha, imebidi kuipunguzia Hazina mzigo huu na kulielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu
  • Waziri wa TAMISEMI atakuwa na manaibu wawili
  • Wizara ya Miundo Mbinu imepunguzwa, imegawanyika kuwa na Wizara ya Ujenzi (barabara na viwanja vya ndege) & Wizara ya Uchukuzi - Reli, bandari na usafiri wa majini
  • Magufuli atachukua wizara ya Ujenzi na msaidizi wake ni Mwakyembe
  • Sitta atakuwa waziri wa Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki
  • Membe ataendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje
  • Ngeleja ataendelea kubaki wizara ya Nishati na Madini
  • Wizara ya Mambo ya Ndani atakuwepo Nahodha akishirikiana na Kagasheki
  • Anna Tibaijuka atakuwa waziri wa Wizara ya Ardhi na Makazi
  • Hakuna jina la Januari Makamba wala Lowassa kama wengi walivyokuwa wakishuku
WIZARA NA MAWAZIRI WAKE:
Umekosea, Wizara ya maji inabaki pekee yake ila umwagiliaji inaenda Kilimo, kutakuwa na Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji
 
Naona hesabu za fasta fasta zinaonyesha tutahitajika kununua ma shangingi 87 kwa ajili ya mawaziri, manaibu na makatibu wakuu. leave alone wakurugenzi, so tukiagiza kama 200 hivi yatatosha!!! zidisha mara milioni 100 kwa kila shangingi!!! mafuta na service!! hatujafilisika tu???
 
Nimeipenda wizara moja tu yenye Mhe. John Magufuli na Harrison Mwakyembe. Nawaamini hawa watu
 
Back
Top Bottom