NIONGEZEENI WENGINE BASI....!?
- Magreth Sitta
- Mwakyusa
- Magembe Amepata kilimo
- etc
Ila kwenye ardhi kuwekewa muhaya tutapata kweli viwanja?Hongera raisi kikwete kwa kutupa raha kwa hili,umafanya jambo la busara wizara kwa mtu anayefaa..
Wanabodi,
Hatimaye Baraza jipya la Mawaziri ndio lianza kutangazwa sasa live kupitia TBC!
Endelea kufuatilia...
UPDATES:
WIZARA NA MAWAZIRI WAKE:
- Wizara ya maji imeunganishwa na Kilimo - Itakuwa Wizara ya Kilimo na umwagiliaji!
- Kazi ajira na vijana - kitengo cha vijana kimehamishiwa michezo na utamaduni
- Uwezeshaji wa wananchi (Baraza la uwezeshaji) - Ilikuwa wizara ya fedha, imebidi kuipunguzia Hazina mzigo huu na kulielekeza Ofisi ya Waziri Mkuu
- Waziri wa TAMISEMI atakuwa na manaibu wawili
- Wizara ya Miundo Mbinu imepunguzwa, imegawanyika kuwa na Wizara ya Ujenzi (barabara na viwanja vya ndege) & Wizara ya Uchukuzi - Reli, bandari na usafiri wa majini
- Magufuli atachukua wizara ya Ujenzi na msaidizi wake ni Mwakyembe
- Sitta atakuwa waziri wa Wizara ya ushirikiano wa Afrika Mashariki
- Membe ataendelea kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje
- Ngeleja ataendelea kubaki wizara ya Nishati na Madini
- Wizara ya Mambo ya Ndani atakuwepo Nahodha akishirikiana na Kagasheki
- Anna Tibaijuka atakuwa waziri wa Wizara ya Ardhi na Makazi
- Hakuna jina la Januari Makamba wala Lowassa kama wengi walivyokuwa wakishuku