Barakoa 😷 Kujilinda na COVID-19 zauzwa Tshs. 2000 na Bila kuivaa huingii lango la Hospitali kwenda kupata matibabu

Ugonjwa wa Corona Virus au Covid-19 inazidi kuleta madhara na kusababisha vifo mbali mbali duniani na hapa nchini.

Bila shaka nchi yetu ndo miongoni mwao nchi chache barani Afrika ambazo zimechukua tahadhari kadhaa bila kufungia wananchi wake ndani (Lockdown) na kuacha wananchi waendelee kufanya shughuli za uzalishaji huku wakihadhari.

Kutokana na hali kuonekana kuanza kuwa mbaya kutokana na idadi kubwa ya watu wanaotangazwa kwa sasa, Hospitali na vituo vya afya zimeanza kutoruhusu wagonjwa kuingia Getini la Hospitali bila kuwa wamevaa Barakoa. Hili ni jambo la kupongezwa na la maana sana kujilinda na maabukizi.

Hata hivyo, hali ya barakoa moja kuuzwa Tshs 2000 imekuwa kidogo changamoto kwa wagonjwa hasa walala hoi. Je hakuna uwezekano bei ikapungua angalau ikauzwa kwa rejareja tshs 500? Kwa kweli hili nalo ni janga.

Hakuna mtu anayependa kuugua huu ugonjwa au kuambukiza wengine huu ugonjwa. Sasa kama vifaa vya kujikinga vitakuwa bei ghali je wananchi wa hali ya chini watamudu?

Tunakoelekea, itakuwa kwamba huwezi ingia sokoni bila kuvaa barakoa nalo ni jambo jema sana na kama watendaji wanaliona mapema na kianze maana masikini nako japokuwa tunanawa mikono basi watu tuvae na barakoa kujilinda kikamilifu. Iwe lazima kwa muuzaji na mteja kuvaa barakoa.

Barakoa inashauliwa kuvalia kwa masaa 4 mfululizo na baada ya hapo itolewe na mtu avae nyingine. Je kama zitakuwa zinauzwa Aghali je wananchi watamudu?

Leo hii pale St. Joseph Hospital Mjini moshi, kuna watu walikuwa wamekwama kuingia mlangoni mwa geti la hospitali kwa kukosa 2000 ya barakoa.

Si kila aende hospitali anaumwa, wengine huwapelekea chakula ndugu zao wagonjwa waliolazwa. Sasa kama mtu alikuwa amejiandaa na nauli halafu anakuta stop getini ya kotoingia bila kuvaa barakoa hapo huwa mtihani.

Kama mama amempeleka mtoto kwenye matibabu, hapa inamlazimu kununua barakoa Mbili : ya kwake (mama) na mtoto pia.Kwa hali hiyo mama atagharamia sh 4000. Hii gharama hakuitegemea kabisa!

My takes.

Barakoa zigawe bure au zipungue bei na zivaliwe na kila mtu sehemu ya mkusanyiko.

Kwa sasa si muda wa Hospitali na maeneo ya public ya mkusanyiko kufanya biashara za hizi Barakoa kama ilivyo kwenye Hospitali ya St. Joseph Mjini Moshi. Wazitoe kama huduma na kama inagalimu basi zitolewe kwa bei nafuu sana.
Nunueni barakoa za kitambaa ambazo zinafulika. Ukiwa nazo mbili au tatu zinatosha. Unafua na kubadilisha kila siku..na bei yake ndo hiyo hiyo elfu mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unavaa barakoa, unaenda kushika sehem yenye kirusi unajifikicha macho kidogo, tayari umekwisha!

Tuvaeni ma helmet tu yale ya pikipiki yenye kufunika kichwa kizima
 
Nimeenda hospitali leo pale Mnazi Mmoja hakuna kuchekiwa wala nini zaidi ya kupuliziwa maji yenye dawa tu .

You'd think a hospital of all places wangekua strict ila waapi . Si Madokta wala manesi waliovaa hizo mask
Wewe mbona haupo strict nyumban kwako?
 
Ila tungekuwa na huduma bora za afya ika sasa ni Mungu tu!
Hapana kwenye barakoa tusingewaza hio kitu kwanza kwenye afya msisitizo huwa dawa zaidi kisha vifaa vingine vinafatia, just imagine nchi kama marekani inafikia hatua ya kuteka barakoa za nchi nyingine. Je walizonazo hazitoshi?maskini sie tusingeweza
 
Hizo barakoa za kutoa bure kwa watu takribani millioni 40 watazipata wapi?

..siyo lazima ziwe milioni 40.

..hivi serikali haina uwezo wa kutoa barakoa kwa polisi, bodaboda, wachuuzi wa sokoni, mama ntilie, etc etc?

..kama tunaweza kutoa chanjo mbalimbali kwanini tushindwe kutoa barakoa?
 
1.umeandika kanakwamba ni utaratibu wa hospitali zote nchini kumbe ni kwenye hiyo hospitali ya Moshi pekee (tena ya mtakatifu-siyo ya umma)

2.barakoa ni vyema zivaliwe na wagonjwa tu au kama na wengine basi kwenye maeneo hatarishi

3.usiione watu wajinga kusema msivae barakoa hovyohovyo kwani endapo mkiamua wote mvae itakuwa kama fashion na si kinga tena na ndo tutapukutika kama kuku wenye kideli maana umakini utakosekana pia itakuwa ngumu kutofautisha wagonjwa na wasio wagonjwa

Sent using Jamii Forums mobile app

1. Hata hospitali za umma wametoa maagizo hakuna mtu kuingia maeneo yao bila barakoa.

2. Barakoa ni nzuri na zinahitajika wakati huu. Zingekuwa hazina msaada basi madaktari na wauguzi wasingekuwa wanazitumia.

3. Katika hali iliyopo sasa hivi, ili covid19 isisambae, wenye ugonjwa, na wasio na ugonjwa, wanatakiwa wavae barakoa.

4. Barakoa zikiwa fashion au utamaduni wetu itakuwa vizuri zaidi. Hata tukiendelea na utaratibu wa sasa wa kuosha mikono itakuwa jambo jema vilevile. Tutafanikiwa kupunguza magonjwa mengi yanayosambaa kwa pumzi, au yanayosambaa kupitia mikono michafu.
 
Ugonjwa wa Corona Virus au Covid-19 unazidi kuleta madhara na kusababisha vifo mbali mbali duniani na hapa nchini.

Bila shaka nchi yetu ndo miongoni mwao nchi chache barani Afrika ambazo zimechukua tahadhari kadhaa bila kufungia wananchi wake ndani (Lockdown) na kuacha wananchi waendelee kufanya shughuli za uzalishaji huku wakihadhari. Hili ni jambo ambalo sisi watanzania tunalipongeza sana tena sana.

Kutokana na hali kuonekana kuanza kuwa mbaya kutokana na idadi kubwa ya watu wanaotangazwa kwa sasa, Hospitali na vituo vya afya zimeanza kutoruhusu wagonjwa kuingia Getini la Hospitali bila kuwa wamevaa Barakoa. Hili ni jambo la kupongezwa na la maana sana kujilinda na maabukizi.

Hata hivyo, hali ya barakoa moja kuuzwa Tshs 2000 imekuwa kidogo changamoto kwa wagonjwa hasa walala hoi. Je hakuna uwezekano bei ikapungua angalau ikauzwa kwa rejareja tshs 500 au tsh 1000.

Hakuna mtu anayependa kuugua huu ugonjwa au kuambukiza wengine huu ugonjwa. Sasa kama vifaa vya kujikinga vitakuwa bei ghali je wananchi wa hali ya chini watamudu?

Tunakoelekea, itakuwa kwamba huwezi ingia sokoni bila kuvaa barakoa nalo ni jambo jema sana na kama watendaji wanaliona basi mapema lianze maana masokoni nako japokuwa tunanawa mikono hatuko salama 100%.Basi watu tuvae barakoa kujilinda kikamilifu na iwe lazima kwa muuzaji na mteja wote tuvae barakoa.

Inasemekana barakoa moja inashauliwa kuvalia kwa masaa 4 mfululizo na baada ya hapo itolewe na mtu avae nyingine. Je kama zitakuwa zinauzwa Aghali je wananchi watamudu?

Si kila anende hospitali anaumwa, wengine huwapelekea chakula ndugu zao wagonjwa waliolazwa. Sasa kama mtu alikuwa amejiandaa na nauli halafu anakuta stop getini ya kotoingia bila kuvaa barakoa hapo huwa mtihani.

Kama mama amempeleka mtoto kwenye matibabu, hapa inamlazimu kununua barakoa Mbili : ya kwake (mama) na mtoto pia.Kwa hali hiyo mama atagharamia sh 4000.

My takes.

Barakoa zigawe bure au zipungue bei na zivaliwe na kila mtu sehemu ya mkusanyiko.

Kwa sasa si muda wa Hospitali na maeneo ya public ya mkusanyiko kufanya biashara za hizi Barako. Wazitoe kama huduma na kama inagalimu basi zitolewe kwa bei nafuu sana.
Serikali Ina viwanda 4999
Ikiwemo vya nguo kwann isitutengenezee barakoa na itupe
Bureee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom