75% ya Wagonjwa wa Saratani wanaofika Hospitali kwa ajili ya matibabu wanakuwa wamechelewa

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Katika kuwafanya Wananchi wengi kuwa na ufahamu kuhusu Ugonjwa wa Saratani na kuwapa elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto hiyo ya kiafya, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road inaendelea na mchakato wa kutembelea mikoa tofauti kutoa elimu na mafunzo kuhusu ugonjwa huo.

Meneja wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma, Dkt. Maguha Stephano anaeleza kuwa mchakato huo ni sehemu ya taasisi yao kuelimisha jamii kutokana na kuonekana kuna dhana tofauti kuhusu Saratani.

Amesema kuna watu wanaamini unapoenda hospitalini kufanyiwa vipimo kama vile Ocean Road kuhusu Saratani ndio mwanzo wa kupata ugonjwa huo, kitu ambacho si kweli, huku wengine wakiwa na ufahamu mdogo na wengine kutojua kabisa kuhusu changamoto ya kiafya ya aina hiyo.
92ea4e60-329d-4773-b429-60c44e293b6b.jpg

Saratani ya Tezi Dume inavyopimwa

Dkt. Maguha Stephano anafafanua: Taasisi ya Ocean Road huwa tunatoa huduma mkoba zinazohusisha matibabu ya Saratani pamoja na uchunguzi, ni huduma za kibingwa ambazo badala ya kufanyika kwenye taasisi yetu pekee tunazunguka na kuzitoa katika Hospitali za Rufaa mikoani pamoja na zile za Kanda.

Kuna wenye uhitaji ambao hawana uwezo wa kufika Dar es Salaam au hawana uelewa kwa ukaribu kuhusu Saratani, hivyo hii ni nafasi yao.

Wakati huu tupo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na sehemu ya huduma tunayoitoa ni elimu pamoja na uchunguzi wa awali na kuwajengea uwezo madaktari wa Geita na mikoa inayozunguka kuhusu Saratani.

Lengo ni kuongeza mwamko wa watu kujitokeza kupata vipimo pamoja na madaktari kuwa na uwezo wa kubaini dalili za awali za Saratani ili kuwawezesha kuwapa rufaa mapema Wagonjwa kwenda katika vituo vinavyohusika na Saratani.
8d8e8fda-79f4-424a-9f5e-d1d28b89e201.jpg
Wagonjwa wanachelewa
Takwimu zinaoneshwa zaidi ya Asilimia 75 ya Wagonjwa wanaofika Ocean Road kwa ajili ya matibabu ya Saratani wanafika wakiwa wamechelewa.

Wanafika wakiwa katika hatua ya tatu au ya nne ya Saratani, hali ambayo inakuwa ni changamoto katika kupata matibabu.

Pia kumekuwa na dhana nyingi potofu kuhusu taasisi yetu hali inayowafanya baadhi kuogopa kujitokeza kufanya vipimo au kutibiwa.

Wapo wanaoamini kuwa ukitibiwa kwa mionzi basi unajitengenezea mazingira ya kupata Saratani jambo ambalo si la kweli kwa kuwa kuna watu wametibiwa Saratani ya matiti, mlango wa kizazi na walipona miaka mingi iliyopita.
59d9bdc6-c2d2-48c2-8965-0afcac5e1922.jpg
Changamoto mikoani
Tukiwa Geita ndani ya siku ya kwanza tumehudumia takribani Watu 200, wengi wakiwa hawajawahi kufanya hata uchunguzi wa Saratani na uelewa wao ni mdogo.

Tukitoka Geita tunatarajia kwenda Mara kuanzia Juni 9 hadi 12 (2023) tutakuwepo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

Saratani inawaumiza watu wazima zaidi
Saratani inawaathiri watu wa rika zote bila kujali jinsia lakini watu wazima wapo katika hali hatarishi zaidi ya kupata Saratani kutokana na umri.

Umri unavyosonga mbele ndivyo ambavyo uwezekano wa kupata Saratani pia unakuwa mkubwa kutokana na asili ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Saratani unatokana na mabadiliko ya chembechembe hai za mwili ambazo zinabadilia taratibu, mfano Saratani ya Mlango wa Kizazi mabadiliko yake ndani ya mwili yanaweza kutokea ndani ya kipindi cha miaka 10 hadi 20, ndio mtu anaanza kupata dalili za wazi.
61fbe9c8-c028-4d90-8877-a62bab498b85.jpg
Wanaume na Saratani ya Tezi Dume
Mfano wa Saratani ya Tezi Dume, Wanaume ambao wana umri wa miaka 50 na kuendelea wapo hatarini zaidi kuliko vijana wadogo.

Kawaida Mwanaume anapofikisha umri wa miaka 40 na kuendelea Tezi Dume yake huwa inaongezeka ukubwa pia kama mabadiliko yalianza kabla ya hapo, ndipo mabadiliko ya chembechembe hai yanapoongezeka kwa kasi.

Saratani ni ugonjwa unaotokana na chembechembe hai mwilini ambazo zinabadilika, nyingine zinakuwa nyingine zinakufa.
c06adac5-365f-4d63-a45e-3a50944bde6b.jpg
Matumizi ya Tumbaku ni hatari
Mojawapo ya kihatarishi cha Saratani ni matumizi ya tumbaku, zile kemikali zinachangia mabadiliko ya uzalishaji na umri wa kuishi wa chembechembe hai.

Saratani ina visababishi tofauti kulingana na saratani husika pia inaweza kutokea kwa kurithi, ukosefu wa mazoezi, unene uliopitiliza, mtindo wa maisha, ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi, matumizi ya mafuta kupita kiasi.
c6ef8f4c-968b-4816-8b0b-5ecf4f2ab6d6.jpg
Madaktari bingwa Ocean Road
Kwa sasa madaktari bingwa wa saratani wapo wamebobea na wanatoa huduma ambazo zamani ilikuwa lazima uende Ulaya ndio unaweza kuzipata

Tuna mashine ya PET-CT Scan ambayo inagundua saratani katika hatua za awali kabisa kuliko mashine nyingine, ni ya kisasa, ndio maana tunasisitiza watu kuwawahisha wagonjwa mapema kwa ajili ya matibabu.

Pia mashine hiyo inafatilia mwenendo wa matibabu kwa wagonjwa waliokshapata matibabu, tayari ipo Ocean Road na inamaliziwa usimikwaji wake na muda wowote itaanza kufanya kazi.

Dhana kuwa Kanda ya Ziwa ina wagonjwa wengi
Kwa Taasisi ya Ocean Road tuna wagonjwa wengi ambao wanatoka maenoe tofauti nchini, dhana hiyo ya kuwa Kanda ya Ziwa ilikuwepo lakini nadhani sio ya Kisanyansi zaidi.

Ilionekana Watu wa Kanda ya Ziwa wengi walikuwa wakifika Dar es Salaam wakiwa hawana ndugu, hivyo wanalazimika kulazwa, ikawa rahisi kuwajua lakini kwa sasa huduma zimesambaa sehemu nyingi nchini ikiwemo Bugando ambapo pia wagonjwa wanaelekea huko.
 
Katika kuwafanya Wananchi wengi kuwa na ufahamu kuhusu Ugonjwa wa Saratani na kuwapa elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto hiyo ya kiafya, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road inaendelea na mchakato wa kutembelea mikoa tofauti kutoa elimu na mafunzo kuhusu ugonjwa huo.

Meneja wa Kitengo cha Uchunguzi wa Saratani na Elimu kwa Umma, Dkt. Maguha Stephano anaeleza kuwa mchakato huo ni sehemu ya taasisi yao kuelimisha jamii kutokana na kuonekana kuna dhana tofauti kuhusu Saratani.

Amesema kuna watu wanaamini unapoenda hospitalini kufanyiwa vipimo kama vile Ocean Road kuhusu Saratani ndio mwanzo wa kupata ugonjwa huo, kitu ambacho si kweli, huku wengine wakiwa na ufahamu mdogo na wengine kutojua kabisa kuhusu changamoto ya kiafya ya aina hiyo.
View attachment 2648715
Saratani ya Tezi Dume inavyopimwa

Dkt. Maguha Stephano anafafanua: Taasisi ya Ocean Road huwa tunatoa huduma mkoba zinazohusisha matibabu ya Saratani pamoja na uchunguzi, ni huduma za kibingwa ambazo badala ya kufanyika kwenye taasisi yetu pekee tunazunguka na kuzitoa katika Hospitali za Rufaa mikoani pamoja na zile za Kanda.

Kuna wenye uhitaji ambao hawana uwezo wa kufika Dar es Salaam au hawana uelewa kwa ukaribu kuhusu Saratani, hivyo hii ni nafasi yao.

Wakati huu tupo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita na sehemu ya huduma tunayoitoa ni elimu pamoja na uchunguzi wa awali na kuwajengea uwezo madaktari wa Geita na mikoa inayozunguka kuhusu Saratani.

Lengo ni kuongeza mwamko wa watu kujitokeza kupata vipimo pamoja na madaktari kuwa na uwezo wa kubaini dalili za awali za Saratani ili kuwawezesha kuwapa rufaa mapema Wagonjwa kwenda katika vituo vinavyohusika na Saratani.
Wagonjwa wanachelewa
Takwimu zinaoneshwa zaidi ya Asilimia 75 ya Wagonjwa wanaofika Ocean Road kwa ajili ya matibabu ya Saratani wanafika wakiwa wamechelewa.

Wanafika wakiwa katika hatua ya tatu au ya nne ya Saratani, hali ambayo inakuwa ni changamoto katika kupata matibabu.

Pia kumekuwa na dhana nyingi potofu kuhusu taasisi yetu hali inayowafanya baadhi kuogopa kujitokeza kufanya vipimo au kutibiwa.

Wapo wanaoamini kuwa ukitibiwa kwa mionzi basi unajitengenezea mazingira ya kupata Saratani jambo ambalo si la kweli kwa kuwa kuna watu wametibiwa Saratani ya matiti, mlango wa kizazi na walipona miaka mingi iliyopita.
Changamoto mikoani
Tukiwa Geita ndani ya siku ya kwanza tumehudumia takribani Watu 200, wengi wakiwa hawajawahi kufanya hata uchunguzi wa Saratani na uelewa wao ni mdogo.

Tukitoka Geita tunatarajia kwenda Mara kuanzia Juni 9 hadi 12 (2023) tutakuwepo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

Saratani inawaumiza watu wazima zaidi
Saratani inawaathiri watu wa rika zote bila kujali jinsia lakini watu wazima wapo katika hali hatarishi zaidi ya kupata Saratani kutokana na umri.

Umri unavyosonga mbele ndivyo ambavyo uwezekano wa kupata Saratani pia unakuwa mkubwa kutokana na asili ya ugonjwa huo.

Ugonjwa wa Saratani unatokana na mabadiliko ya chembechembe hai za mwili ambazo zinabadilia taratibu, mfano Saratani ya Mlango wa Kizazi mabadiliko yake ndani ya mwili yanaweza kutokea ndani ya kipindi cha miaka 10 hadi 20, ndio mtu anaanza kupata dalili za wazi.
Wanaume na Saratani ya Tezi Dume
Mfano wa Saratani ya Tezi Dume, Wanaume ambao wana umri wa miaka 50 na kuendelea wapo hatarini zaidi kuliko vijana wadogo.

Kawaida Mwanaume anapofikisha umri wa miaka 40 na kuendelea Tezi Dume yake huwa inaongezeka ukubwa pia kama mabadiliko yalianza kabla ya hapo, ndipo mabadiliko ya chembechembe hai yanapoongezeka kwa kasi.

Saratani ni ugonjwa unaotokana na chembechembe hai mwilini ambazo zinabadilika, nyingine zinakuwa nyingine zinakufa.
Matumizi ya Tumbaku ni hatari
Mojawapo ya kihatarishi cha Saratani ni matumizi ya tumbaku, zile kemikali zinachangia mabadiliko ya uzalishaji na umri wa kuishi wa chembechembe hai.

Saratani ina visababishi tofauti kulingana na saratani husika pia inaweza kutokea kwa kurithi, ukosefu wa mazoezi, unene uliopitiliza, mtindo wa maisha, ulaji wa nyama nyekundu kupita kiasi, matumizi ya mafuta kupita kiasi.
Madaktari bingwa Ocean Road
Kwa sasa madaktari bingwa wa saratani wapo wamebobea na wanatoa huduma ambazo zamani ilikuwa lazima uende Ulaya ndio unaweza kuzipata

Tuna mashine ya PET-CT Scan ambayo inagundua saratani katika hatua za awali kabisa kuliko mashine nyingine, ni ya kisasa, ndio maana tunasisitiza watu kuwawahisha wagonjwa mapema kwa ajili ya matibabu.

Pia mashine hiyo inafatilia mwenendo wa matibabu kwa wagonjwa waliokshapata matibabu, tayari ipo Ocean Road na inamaliziwa usimikwaji wake na muda wowote itaanza kufanya kazi.

Dhana kuwa Kanda ya Ziwa ina wagonjwa wengi
Kwa Taasisi ya Ocean Road tuna wagonjwa wengi ambao wanatoka maenoe tofauti nchini, dhana hiyo ya kuwa Kanda ya Ziwa ilikuwepo lakini nadhani sio ya Kisanyansi zaidi.

Ilionekana Watu wa Kanda ya Ziwa wengi walikuwa wakifika Dar es Salaam wakiwa hawana ndugu, hivyo wanalazimika kulazwa, ikawa rahisi kuwajua lakini kwa sasa huduma zimesambaa sehemu nyingi nchini ikiwemo Bugando ambapo pia wagonjwa wanaelekea huko.
Mje na huku Mbeya, tunahitaji huduma hiyo pia, changamoto za Saratani zipo lakini bado ufahamu ni mdogo.
 
Shida kubwa Tz ni watu hawaweki muda kwenye kujielemisha.

Watu hawajali
 
Back
Top Bottom