#COVID19 RC Mtaka: Wasiovaa barakoa marufuku kwenda kuwaona wagonjwa hospitali zote za Dodoma

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, amewataka wananchi wanaokwenda kuwaona wagonjwa katika hospitali hizo kuhakikisha wanavaa barakoa kwa lengo la kujikinga wao na wagonjwa dhidi ya ugonjwa wa Corona ama sivyo wasiruhusiwe.

Ametoa tahadhari hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliojionea mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni inayosambazwa katika wodi mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

RC Mtaka ametoa amri ya kutowaruhusu watu wote wanaokwenda kuwafariji wagonjwa ama kuwapelekea chakula wasiovaa barakoa katika hospitali za binafsi na za serikali mkoani humo.

"Mganga Mkuu wa Mkoa amesema kuwa wanaokwenda kumuona mgonjwa wasizidi watu watatu, sisi wa mkoa tumeyapokea lakini nyongeza yake ni ukitaka kwenda kumuona mgonjwa, kumpelekea chakula bila kuvaa barakoa hatutakuruhusu, ili uruhusiwe kumuona kwenye zahanati, kituo cha afya, hospitali ya serikali au ya binafsi tunawaomba mvae barakoa kwa faida yako na mgonjwa pia," amesisitiza RC Mtaka.

Pia ameweka msisitizo kwa maeneo yote ya biashara na yenye mikusanyiko mikubwa, sokoni, minada na stendi kila mmoja achukue tahadhari kwa kuvaa barakoa na kunawa maji tiririka ama kujipaka sanitaiza.

Amewashauri watu wote wanaojihisi kuwa na dalili za ugonjwa wa corona wasibahatishe kuhusu tiba bali waende kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali kupimwa ili kuwa na uhakika.

Vilevile amezitaka daladala kupakia 'level seat' na bodaboda kuzingatia sheria ya kupakia abiria mmoja ili kuepukana na maambukizi ya ugonjwa huo.

RC Mtaka, amekiri uwepo wa wagonjwa wa corona mkoani humo na kwamba wanajitosheleza kuwahudumia kwa vile hakuna msongamano.
 
Watuambie tu kama barakoa inazuia covid tuanze kutembea na packet zake za kutosha kila sehemu.
 
Back
Top Bottom