Michaelmakene
JF-Expert Member
- Aug 7, 2019
- 236
- 322
.... hongera ndg umetoa elimu njema Sana nazani wahusika wakilifanyia kazi inaweza saidia sana....lengo kuu ni kuondoa maambukizi mapya na kuendana na hali ya vipato vya wananchi.....Je ni lazima wagonjwa wanunue mask kutoka kwao?
Sehemu nyingi nchi zingine sasa hivi ni lazima kuvaa mask au kufunika mdomo na pua kwa njia yoyote ya kitambaa hili kupata uduma. Kama mtu hana mask maalum, wanatumia kilemba, kitambaa chochote kufunika pua na mdomo.
Kwahio ni muhimu kuruhusu raia watumie kitambaa chochote kuziba pua na mdomo hili kupunguza usumbufu. Kanga za zamani mtu anaweza kutumia kukata na kukunja mara tatu akafunika mdomo na pua kama hana hela ya kununua mask. Muhimu ni kuhakikisha kitambaa ni kisafi.
Tuache uvivu wa kufikiri kwamba kila kitu hatuwezi au hakiwezekani. Kuna mitambala mibovu majumbani mengine mnatumia kupigia deki lakini mnashindwa kutumia kuziba midomo na pua kujikinga na hili janga.
Huu ugonjwa upo na uamaliza watu. Ni muhimu kuchukua hatua mapema kuliko kusubiri hapo baadae hali ikiwa mbaya.