Barabara ya Njia 4 Kibaha - Morogoro itakuwa na Tozo

Yaani wewe unajufuniaga nguo kumbe hujui kitu
Unatia huruma
Jo kuna wakati nadhani zinakufyatuka kidogo
Barabara ya zamani Picha ya ndege mpaka kwa Mfipa madaraja yameshaanza kujengwa
Barabara ya Tamko Mapinga kuna shida na mkandarasi anayetajwa kama Mayanga Construction maana hajajenga hata km 5 tangu 2018
Hiyo ya Kibaha Morogoro iko kwenye maandalizi tangu May
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Super idea. Fanyeni hivyo hivyo hata kwa ujenzi wa viwanja vya michezo.
 
Yani nikipewa madaraka nitakuwa Magufuli x 10 yake sicheki na boya. Kazi tu!

Maadui zangu ni wajinga wajinga wezi na mafisadi ndio ntawanyoosha. Hukumu ni shaba tu hamna kingine. Ukikutwa umedokoa hela na ushahidi ukapatikana jua ni shaba moja kwa moja.
Nchi za europe watu waliuana sana kimtindo huo plus kulishwa uzalendo ule wa kupenda nchi yako ipige hatua na ndio maana wenzetu wamefika pale,mimi nishakaa nchi 1 hivi nyumba kama ya 3 alikua anaishi waziri wao wa mazingira,aisee yule anaishi uswazi tu na kiford chake anadrive mwenyewe na yuko peace,huku kwetu mtu akipata cheo familia first
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEOW
Ni mpango mzuri, ila isiwe na matuta na zebra crossings, kuwe na vivuko vya juu vya wavuka barabara kwa miguu na speed limit isishuke chini ya 80km.
Barabara ya Kimara -Kibaha, japo ni ya nyia 4 bado haijapunguza mda wa kusafiri, hivyo sioni manufaa yake.
 
Walipoweka mataa na mizebra kibao ndio walipo haribu! Barabara ni ya highway ila haina tofauti na barabara ya mjini kati. Kimsingi alitakiwa asionekane mtu hata mmoja akikatiza barabarani, ile gharama ya kujaza mataa wangeweka vivuko vya juu kama cha buguruni kile.

Sielewi sijui hao wanaopanga mipango ya barabara wanawazaga kwa kutumia nini!
 
Jo kuna wakati nadhani zinakufyatuka kidogo
Barabara ya zamani Picha ya ndege mpaka kwa Mfipa madaraja yameshaanza kujengwa
Barabara ya Tamko Mapinga kuna shida na mkandarasi anayetajwa kama Mayanga Construction maana hajajenga hata km 5 tangu 2018
Hiyo ya Kibaha Morogoro iko kwenye maandalizi tangu May

Mshana kwanza elewa kuwa swali la jamaa ni la kutafuta kiki kwani inasemekana kuwa Mwendazake alirest in pisi akiwa ameshatenga kule Hazina fund ya barabara ya Kibaha (Mailimoja) mpaka Mlandizi, Brbr ya Mapinga hhaitakaa iishe sababu humo kuna wenzetu - wengi tu, Mlandizi - Chalinze - Morogoro nafikiria ni project ya kufikirika kama utakumbuka kuna express way ambayo iliongelewa mpaka bungeni na ilifanyiwa mpaka survey ambayo ilikuwa inaanzia Bandarini - Tazara - Kibamba - Kibaha ikapita mkongeni karibu na kwa Askofu Mwingira - Mlandizi hadi Msoga iungane na ile ya Bagamoyo, brbr hii walisema itakuwa ya kulipia lakini imeishia kwenye makaratasi, pia kumbuka kuna bwana mmoja na wenzake hivi karibuni walisema njia nne ni mpaka Tunduma...cha muhimu zaidi kumbuka kuwa 2025 is at corner!
 
cha muhimu zaidi kumbuka kuwa 2025 is at corner! nimekupata vema
 
Kwa mtanzamo wangu naona Sawa Tu kwasababu serikali hawataingiza pesa zao kwenye mradi kitakachofanyika ni kutangaza tender na atakayeshinda atatengeneza barabara na ikikamilika ataanza kutoza pesa ili hela yake irudi(shida itakuja Kwa huyu mzabuni anaweza kupiga pesa Kwa miaka mingi huku akitoza hela nyingi Kwa gari moja)..
Serikali ingekuwa ina Akili timamu wangetia hela wenyewe Tu
Yani kulikoni huyo mzabuni bora serikali ichukue tozo yenyewe. Sababu gharama ya kusafiria barabara kwa hizo kilometre inaweza kuwa ndefu kichizi. Ila bora ilimradi isiwe na matrafiki tu ambao ni kero namba 1
 
Mshana kwanza elewa kuwa swali la jamaa ni la kutafuta kiki kwani inasemekana kuwa Mwendazake alirest in pisi akiwa ameshatenga kule Hazina fund ya barabara ya Kibaha (Mailimoja) mpaka Mlandizi, Brbr ya Mapinga hhaitakaa iishe sababu humo kuna wenzetu - wengi tu, Mlandizi - Chalinze - Morogoro nafikiria ni project ya kufikirika kama utakumbuka kuna express way ambayo iliongelewa mpaka bungeni na ilifanyiwa mpaka survey ambayo ilikuwa inaanzia Bandarini - Tazara - Kibamba - Kibaha ikapita mkongeni karibu na kwa Askofu Mwingira - Mlandizi hadi Msoga iungane na ile ya Bagamoyo, brbr hii walisema itakuwa ya kulipia lakini imeishia kwenye makaratasi, pia kumbuka kuna bwana mmoja na wenzake hivi karibuni walisema njia nne ni mpaka Tunduma...cha muhimu zaidi kumbuka kuwa 2025 is at corner!
Hio 2025 bila machafuko wataendelea kuishi Ikulu na 2030 still watarithishana vijiti.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Na hili pia nawaomba ndugu zangu mkaliangalieee!!!
 
Ndiyo yatakuwa yaleyale ya DART...

Yani hiyo barabara mpaka waje wairudishe ni mpaka pale hiyo barabara ichakae kwanza.

Hawataikabidhi kwa muda kwa visingizio vya hapa na pale hasa "Bado Hatujarudisha Chetu"..

Na hapo tenda ndiyo utakuta kuna mkono wa mkubwa mmoja.

Yani inshort ni kwamba hapa tayari kuna mkubwa kashaichukua hii tenda.

RIP JPM, ULISEMA TUTAKUKUMBUKA KWA MAZURI NA KWELI YANATIMIA.
Wavivu kama wewe mliokuwa mnafurahia kuitwa wanyonge mtazungukia Selous mkienda Morogoro. Road toll zipo kila mahali Duniani hata kwenda Kigamboni
 
Hapa misugusugu karibu na kiwanda cha sabuni nice one zaid ya km 2 toka main road nilikuwa najenga kakibanda kangu kule nimepigwa stop kujenga tuliambiwa kuna barabara ya "mwendo kasi" itapita labda ndio hii, dah wanipe pesa zangu nikaangalie ustaarabu mwingine dah
 
Super idea. Fanyeni hivyo hivyo hata kwa ujenzi wa viwanja vya michezo.
Kweli kabisa, kwa mfumo huu tunaweza kupata barabara mbadala nyingi hasa mijini na kufanikiwa kupunguza misongamano ya magari. Tanzania sio kuwa tuna magari mengi, barabara ndio hatuna za kutosha na zilizopo ni finyu na zina design mbaya ya kizamani hasa kwenye makutano(four ways). Mlifika Botswana siku za karibuni mtaelewa ninachoongea. Kuna Junctions zina barabara 8, wanaenda kulia na kushoto, wana barabara zao ,hawajipangi kwenye barabaza za wanaoenda moja kwa moja.
 
Ndani ya miaka 10 mwendazake angekuwepo njia ingefika Tunduma bila hata kutozwa hata tsh.100! Katika kila litre ya mafuta kuna hela ya kuboresha barabara, Tarura wanakusanya za maegesho. Hizo hela zote zinaenda wapi?

Magari yako million ngapi nchini?
Mzilankende Kuna Alifanya Mazuri Hawa Wa Sasa Sijui Wanakwama Wapi
 
Jo kuna wakati nadhani zinakufyatuka kidogo
Barabara ya zamani Picha ya ndege mpaka kwa Mfipa madaraja yameshaanza kujengwa
Barabara ya Tamko Mapinga kuna shida na mkandarasi anayetajwa kama Mayanga Construction maana hajajenga hata km 5 tangu 2018
Hiyo ya Kibaha Morogoro iko kwenye maandalizi tangu May
Kwahiyo hii ya kibaha to Morogoro ipo kwel mkuu au ni Siasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Toza
Tozea
Tozana
Tozesha
Tozeshea
Tozanisha
Tozanishana
 
Back
Top Bottom