KWA NCHI KAMA YETU ILIYOUZA RASILIMALI ZAKE ZOTE KWA WAZUNGU SI RAHISI KUWANYALI WAFANYABIASHARA.
Bwana King Kong, mimi nashangaa kitu kimoja, tunakosoa kwamba nchi haijali wafanyabiashara, lakini Magufuli akitoa kauli mhemko ya
"Mimi ni Rais wa masikini" huwa tunaona poa, tunashangilia, why?
Hakuna hata mtu aliyewahi kumpinga (hata wapinzani) Magufuli kwamba hey, Mr. President, wewe sio Rais wa masikini peke yao, wala hukuchaguliwa na masikini peke yao, kama alivyodai juzi Unguja. Tanzania hakuna "exit poles" za kutathmini nani kamvotia nani.
Wapinzani wanaogopa kupinga kauli ya "Mimi ni Rais wa masikini" wasije wakaonekana ni out of touch, bourgeoisie class wanaoetetea matajiri wenzao.
Lakini hao matajiri ambao Magufuli hawajali ni mimi na wewe tunaomiliki laptop moja, una afford kukaa baa ku order bia tatu, sahani ya nyama na bar maid mmoja, una kiwanja Dar-es-Salaam, una Toyota Carina, una ki agency cha M-Pesa na mitikasi mingine legal lakini isiyoelezeka in 30 seconds, una vitoto viwili una unga unga kuvipeleka English Medium school, kwa Tanzania wewe ni tajiri mchafu! Na haufiti kwenye definition ya kundi la watu ambao Magufuli anawajali.
I wish Watanzania wangelijua hili. Wasingekuwa wanakubali na kushangilia Rais akisema yeye ni Rais wa masikini. Wengi sana, wahangaikaji na wabangaizaji wengi mno tunaachwa nje ya hiyo definition, sembuse li kampuni linalo import makontena ya unga wa ngano? Ndio watalijali?