Tina
JF-Expert Member
- Jul 9, 2007
- 572
- 584
- Thread starter
- #21
YAH: HOJA ZA WENYEVITI NA MAKATIBU KWA KATIBU MKUU DOWUTA
UTANGULIZI:
1.0 Rejea mazungumzo kati yako na Wenyeviti na Makatibu wa Matawi kwa nyakati mbalimbali kuhusiana na hali ya itemdaji kazi katika Bandari zetu kufuatia mikakati ya nchi zenye Bandari shindani na Bandari zetu na zile nchi zinazotumia Bandari za Tanzania, viongozi wa Matawi waliona busara kukutana nawe ili kuyabainisha matatizo ambayo yanaweza kuathiri Taasisi yetu na nchi kwa ujumla.
Aidha hofu waliyonayo Wanachama/Wafanyakazi kuhusu mustakabali wa nafasi zao za ajira.
2.0 Hivyo Wenyeviti na Makatibu katika kikao chao maalum kilichokutana leo tarehe 6/9/2013 katika Ofisi ya tawi la DOWUTA Makao Makuu kilipokea taarifa mbalimbali kitoka kwa Matawi yote ya TPA.
3.0 Baada ya kupokea taarifa hizo viongozi wa Matawi walibaini hali ya kiwanda kuwa sio nzuri hivyo masuala makuu yafuatayo yafanyiwe kazi haraka ili kuondoa hali ya sintofahamu kwa Wafanyakazi. Masuala hayo muhimu ni kama ifuatavyo:-
(1) Hofu ya DOWUTA kwa Bandari kupoteza shehena /Biashara kutokana na Mkataba uliofingwa hivi karibuni kati ya Nchi za Kenya Uganda na Rwanda kujenga Reli ya pamoja kutoka Mombasa hadi Kigali na kukamilika ujenzi wa Reli kutoka Bandari ya Lobito (Angola) hadi mpaka wa Nchi ya Zambia hali ambayo itazuia au kupunguza shehena kupitia Bandari zetu.
(2) Kukwama kwa utekelezaji wa maslahi ya Wafanyakazi ambayo tumekubaliana kwenye mabaraza halali ambayo yapo kishera.
(3) Kutofanyika kwa vikao vya ajira na nidhamu kwa muda mrefu hivyo kuathiri utendaji wa kazi na kuwanyima haki Wafanyakazi wanaotuhumiwa na wanaostahili kupandishwa madaraja.
Tunawasilisha kwa majadiliano
WENYEVITI NA MAKATIBU