Bandari anayojenga Marekani Gaza si ya misaada, bali ni bandari ya kifo cha Palestina pamoja na maslahi ya Marekani na ulinzi wa Israel

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,186
10,922
Wanaharakati wanaopigania haki za wapalestina wametoa uchambuzi ukifafanua juu ya uharamu wa bandari inayoendelea kujengwa na Marekani eneo la Gaza kwa kisingizio cha kupeleka misaada.

Mshangano wa mwanzo wa wanaharakati hao ni kuwa Marekani imepeleka malori na mashine nzito za ujenzi zipatazo 30 kwa muda mfupi kubeba kifusi na kujaza bahari ili kufikia eneo la kutia nanga meli kubwa za mizigo.

Kwanza kifusi hicho kimejaa maiti za watu waliangukiwa na majumba wakati Israel ikipiga kwa mabomu mazito ambao haikuwezekana kuokolewa na watu wao.

Wakati Israel ilipoporomosha majengo hayo walizuia njia zote za uokozi ikiwemo kuziripua gari za kubebea wagonjwa na buldoza zilizotumiwa na wapalestina kuwafikia watu hao. Huku ndugu wakisikia vilio vya watu waot hawakuweza kufanya chochote na hatimae masaa 72 yalitimia bila kupata usaidizi ambao ungeweza kuokoa maisha yao.

Marekani siku hizo kumbe wangeweza kupeleka zana nzito za kuondoa vifusi kwa muda mfupi kutoka visiwa vya Cyprus na hawakufanya hivyo.Barabara ndefu inayojengwa kufikia gati hilo imepewa jina la njia ya vifo.

Eneo linapojengwa gati hilo ni eneo kubwa na muhimu kwa wapalestina wa Gaza ambapo waliweza kutumia kwa mapumziko na shughuli za uvuvi. Kuanzia sasa inakisiwa itakuwa ni kambi kubwa ya kijeshi ambayo itazuiwa kwa wapalestina kufika na kutumia kwa shughuli yoyote ile.

Meli kubwa zitakazotia nanga hapo zitakuwa zikiwahamasisha wapalestina kuhama na kupelekwa nchi nyengine kuishi kwa kudumu na kuipa nafasi Israel kujitanua kutoka ukingo wa magharibi mpaka bahari ya mediterraneon yote.

Askari 2000 wanaotumika kujenga eneo hilo baada ya muda mfupi wataongezeka na kufikia hata 20,000 ikiwa ni kituo kikubwa cha kijeshi cha kuilinda bahari ya Mediteranean kwa maslahi ya Israel na Marekani yenyewe.
 
Niliwahi kusema siku za nyuma hii vita tusiiangalie kwa macho ya juu juu kuna kitu kikubwa zaidi kimejificha nyuma ya tunayoyaona kwa macho ya kawaida, wakati Natanyahu anarudimadarakani kuna mahala nilisoma walisema mpango wa kumrudisha madarakani una madhara makubwa sana kwa wa Palestina na Gaza kwa ujumla siku za usoni.
 
Wanaharakati wanaopigania haki za wapalestina wametoa uchambuzi ukifafanua juu ya uharamu wa bandari inayoendelea kujengwa na Marekani eneo la Gaza kwa kisingizio cha kupeleka misaada.

Mshangano wa mwanzo wa wanaharakati hao ni kuwa Marekani imepeleka malori na mashine nzito za ujenzi zipatazo 30 kwa muda mfupi kubeba kifusi na kujaza bahari ili kufikia eneo la kutia nanga meli kubwa za mizigo.

Kwanza kifusi hicho kimejaa maiti za watu waliangukiwa na majumba wakati Israel ikipiga kwa mabomu mazito ambao haikuwezekana kuokolewa na watu wao.

Wakati Israel ilipoporomosha majengo hayo walizuia njia zote za uokozi ikiwemo kuziripua gari za kubebea wagonjwa na buldoza zilizotumiwa na wapalestina kuwafikia watu hao. Huku ndugu wakisikia vilio vya watu waot hawakuweza kufanya chochote na hatimae masaa 72 yalitimia bila kupata usaidizi ambao ungeweza kuokoa maisha yao.

Marekani siku hizo kumbe wangeweza kupeleka zana nzito za kuondoa vifusi kwa muda mfupi kutoka visiwa vya Cyprus na hawakufanya hivyo.Barabara ndefu inayojengwa kufikia gati hilo imepewa jina la njia ya vifo.

Eneo linapojengwa gati hilo ni eneo kubwa na muhimu kwa wapalestina wa Gaza ambapo waliweza kutumia kwa mapumziko na shughuli za uvuvi. Kuanzia sasa inakisiwa itakuwa ni kambi kubwa ya kijeshi ambayo itazuiwa kwa wapalestina kufika na kutumia kwa shughuli yoyote ile.

Meli kubwa zitakazotia nanga hapo zitakuwa zikiwahamasisha wapalestina kuhama na kupelekwa nchi nyengine kuishi kwa kudumu na kuipa nafasi Israel kujitanua kutoka ukingo wa magharibi mpaka bahari ya mediterraneon yote.

Askari 2000 wanaotumika kujenga eneo hilo baada ya muda mfupi wataongezeka na kufikia hata 20,000 ikiwa ni kituo kikubwa cha kijeshi cha kuilinda bahari ya Mediteranean kwa maslahi ya Israel na Marekani yenyewe.
Akireport Alwaz kutoka al-Taqiyya news room
 
Nyie watu wanafiki Sana mwanzoni ulikuwa ukisema waisraeli wanapigika vilivyo pale Gaza kumbe sasa hivi imekuwa wapalestina ndo wapigwa kipigo cha mbwa Koko?
 
Safi sana kwa kulijua hilo, nyie lazima mpumuliwe masikioni ndio msikie, Marekani iwekeze kabisa hayo maeneo, ijenge bandari na isimamishe kambi kubwa ya kijeshi.
 
Back
Top Bottom