Gaza ni Marekani dhidi ya Palestina si Israel na HAMAS

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,879
35,878
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu. Ikumbukwe;

1. Israel anajinasibu kupambana na HAMAS akisema hana taabu na wapalestina huku wahanga wakiwa wapalestina; hadi West Bank ambako hakuna HAMAS.

3. Kila vita vinapotaka kusimama, maafisa wazito wazito wa Marekani huenda Israel na vita hurundima upya kwa kasi mpya na ari mpya punde tu wanene hao wanapoondoka:

IMG_20231221_073031~2.jpg

2. Vita viliwaka moto Kwa kasi zaidi baada ya kusimama, siku moja tu baada ya waziri Blinken kuzuru Israel.

3. #2 hapo ikumbukwe Blinken alisema wanapenda vita iendelee, ila waone vifo vya raia vinapungua (japo kidogo) siyo vita kusimama

4. Baada ya Israeli kuuwa mateka wake Israel, nia ya kurejea mezani iliimatika Hadi UN: UNSC ikaitishwa kwa azimio la kusitisha vita:

UNSC kusimamisha vita Gaza

5. Kama safari ile, safari hii wanene wengine wakaelekea Israel; na alipoondoka tu mnene huyo wa Pentagon, vita vilivyokuwa vimeanza kupoa kuonesha dalili ya kufikia mwisho mwema vikarindima tena, kasi mpya, ari mpya na nguvu zaidi:

Vita Gaza katika mwelekeo mwema, busara inapoanza kurejea

6. Bwana Lloyd Austin akaitangazia dunia kuwa Sasa vita itakuwa 'more surgical," whatever that means, na eti kuwa haitakuwa "shoot to kill" ila "think first before shooting" eti wasiuwe mateka wengine kama wale kama watatokea tena.

7 Tokea hapo Marekani amekuwa anajivuta miguu na kura UNSC tokea jumatatu Kkla siku ati mpaka aridhike; hadi wa leo.

8. Mawaziri wote wawili hawa na ma spy masters wao kila wakifika Israel hushiriki kwenye vikao vya baraza la vita kama wajumbe kamili.

9. #8 hapo yawezekana hushiriki siku zote kupitia teknolojia.

10. Marekani hataki suluhu, hana haja na mateka mengine yote ni mbwembwe kumnyorosha mpalestina, bila shaka lengo kuu akimtafuta Iran ajichanganye.

11. #10 hapo ndiyo maana kaleta manowari zake pale na ana madege yake juu bega kwa bega katika operation hii.

12. Sasa hivi Blinken kafichama, kimya hasikiki; mnafiki mkubwa!

13. Hadi dunia itakapo mstukia beberu mkuu mwenye vita yake na Iran huyu, bado tupo tupo sana!
 
Wanaoneshana ubabe
Watu wakishiba ndio shida yao bora wakae njaa
Hata home watoto wakishiba watakusumbua wakiwa na njaawanatulia na usikivu unakuwa mkubwa
 
Palestina ianzishe uhusiano na North Korea pamoja na Russia kupitia Wagner, hawa wengine akina Iran waogawaoga tu...

Nilitegemea kuwaona Hizbollah wakilianzisha upande mwingine kama support kwa Palestina huku na kufanya vita isiyoiasha..

Taleban na wale Chechniya huwa wana wapiganaji wenye uvumilivu na uwezo wa kudumu vitani kwa muda mrefu sana ambacho ni kitu USA na Israel hawataki kukiona..

Iran angetumia influence yake na Urusi, kupitisha wataleban na wachechniya wapite Iran to syria and Lebanon wakae upande wa Hizbollah tushuhudie mtanange wa chini kwa chini..
 
1. Unayo hoja nzito taabu Russia anashindwa kusimama wima kiuadilifu kwa kumwonea Ukraine.

2. Asingekuwa na lake Ukraine hapa ndipo palikuwa pa kuonyesha uongozi wa dunia. Dunia yote Ingemwunga mkono.

3. Angalia kura hii:

Israel na Marekani wapewa za uso UNGA
 
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu. Ikumbukwe;

1. Israel anajinasibu kupambana na HAMAS akisema hana taabu na wapalestina huku wahanga wakiwa wapalestina; hadi West Bank ambako hakuna HAMAS.

3. Kila vita vinapotaka kusimama, maafisa wazito wazito wa Marekani huenda Israel na vita hurundima upya kwa kasi mpya na ari mpya punde tu wanene hao wanapoondoka:

View attachment 2848731

2. Vita viliwaka moto Kwa kasi zaidi baada ya kusimama, siku moja tu baada ya waziri Blinken kuzuru Israel.

3. #2 hapo ikumbukwe Blinken alisema wanapenda vita iendelee, ila waone vifo vya raia vinapungua (japo kidogo) siyo vita kusimama

4. Baada ya Israeli kuuwa mateka wake Israel, nia ya kurejea mezani iliimatika Hadi UN: UNSC ikaitishwa kwa azimio la kusitisha vita:

UNSC kusimamisha vita Gaza

5. Kama safari ile, safari hii wanene wengine wakaelekea Israel; na alipoondoka tu mnene huyo wa Pentagon, vita vilivyokuwa vimeanza kupoa kuonesha dalili ya kufikia mwisho mwema vikarindima tena, kasi mpya, ari mpya na nguvu zaidi:

Vita Gaza katika mwelekeo mwema, busara inapoanza kurejea

6. Bwana Lloyd Austin akaitangazia dunia kuwa Sasa vita itakuwa 'more surgical," whatever that means, na eti kuwa haitakuwa "shoot to kill" ila "think first before shooting" eti wasiuwe mateka wengine kama wale kama watatokea tena.

7 Tokea hapo Marekani amekuwa anajivuta miguu na kura UNSC tokea jumatatu Kkla siku ati mpaka aridhike; hadi wa leo.

8. Mawaziri wote wawili hawa na ma spy masters wao kila wakifika Israel hushiriki kwenye vikao vya baraza la vita kama wajumbe kamili.

9. #8 hapo yawezekana hushiriki siku zote kupitia teknolojia.

10. Marekani hataki suluhu, hana haja na mateka mengine yote ni mbwembwe kumnyorosha mpalestina, bila shaka lengo kuu akimtafuta Iran ajichanganye.

11. #10 hapo ndiyo maana kaleta manowari zake pale na ana madege yake juu bega kwa bega katika operation hii.

12. Sasa hivi Blinken kafichama, kimya hasikiki; mnafiki mkubwa!

13. Hadi dunia itakapo mstukia beberu mkuu mwenye vita yake na Iran huyu, bado tupo tupo sana!

Kwa hiyo ni Marekani ndio waliwatuma Hamas wakawaue wananchi zaidi ya 1,000 nchini Israel?
 
1. Inayo hoja nzito taabu Russia anashindwa kusimama wima kiuadilifu kwa kumwonea Ukraine.

2. Asingekuwa na lake Ukraine hapa ndipo palikuwa pa kuonyesha uongozi wa dunia. Dunia yote Ingemwunga mkono.

3. Angalia kura hii:

Israel na Marekani wapewa za uso UNGA

Kwa hiyo vita imesimama?

Katika watu wasioaminika kabisa, jamii ya waarabu ni no.1. Na hilo alilidhihirisha hata Gadafi. Na akasema ni aheri awe mwanachama wa taasisi ya Waafrika kuliko waarabu, kwa sababu hawaaminiki na hawana msimamo.
 
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu. Ikumbukwe;

1. Israel anajinasibu kupambana na HAMAS akisema hana taabu na wapalestina huku wahanga wakiwa wapalestina; hadi West Bank ambako hakuna HAMAS.

3. Kila vita vinapotaka kusimama, maafisa wazito wazito wa Marekani huenda Israel na vita hurundima upya kwa kasi mpya na ari mpya punde tu wanene hao wanapoondoka:

View attachment 2848731

2. Vita viliwaka moto Kwa kasi zaidi baada ya kusimama, siku moja tu baada ya waziri Blinken kuzuru Israel.

3. #2 hapo ikumbukwe Blinken alisema wanapenda vita iendelee, ila waone vifo vya raia vinapungua (japo kidogo) siyo vita kusimama

4. Baada ya Israeli kuuwa mateka wake Israel, nia ya kurejea mezani iliimatika Hadi UN: UNSC ikaitishwa kwa azimio la kusitisha vita:

UNSC kusimamisha vita Gaza

5. Kama safari ile, safari hii wanene wengine wakaelekea Israel; na alipoondoka tu mnene huyo wa Pentagon, vita vilivyokuwa vimeanza kupoa kuonesha dalili ya kufikia mwisho mwema vikarindima tena, kasi mpya, ari mpya na nguvu zaidi:

Vita Gaza katika mwelekeo mwema, busara inapoanza kurejea

6. Bwana Lloyd Austin akaitangazia dunia kuwa Sasa vita itakuwa 'more surgical," whatever that means, na eti kuwa haitakuwa "shoot to kill" ila "think first before shooting" eti wasiuwe mateka wengine kama wale kama watatokea tena.

7 Tokea hapo Marekani amekuwa anajivuta miguu na kura UNSC tokea jumatatu Kkla siku ati mpaka aridhike; hadi wa leo.

8. Mawaziri wote wawili hawa na ma spy masters wao kila wakifika Israel hushiriki kwenye vikao vya baraza la vita kama wajumbe kamili.

9. #8 hapo yawezekana hushiriki siku zote kupitia teknolojia.

10. Marekani hataki suluhu, hana haja na mateka mengine yote ni mbwembwe kumnyorosha mpalestina, bila shaka lengo kuu akimtafuta Iran ajichanganye.

11. #10 hapo ndiyo maana kaleta manowari zake pale na ana madege yake juu bega kwa bega katika operation hii.

12. Sasa hivi Blinken kafichama, kimya hasikiki; mnafiki mkubwa!

13. Hadi dunia itakapo mstukia beberu mkuu mwenye vita yake na Iran huyu, bado tupo tupo sana!
Ghazzat (Gaza) kuna shimo la kuzimu lisiloonekana kwa macho ya nyama na binadamu wa kawaida anapumbazwa na haiba za sura za wenyeji kutoonesha hatia usoni lakini pia wanakuvuta uwe karibu nao ili wakusome vizuri kabla hawajakuangamiza.

Delila alikuwa mwanamke mwenye asili ya jamii ya Natuf (waarabu wa Gaza) ndiye aliyeingia urafiki na Samson mwenye nguvu nying kutoka Israel jamii ya Skhul na Qafzeh hominids (Hebrania) akashawishiwa kueleza chanzo cha nguvu zake alijitahidi kudanganya lakini hatimaye akatamka kwamba 'ukininyoa nywele zangu na nguvu zangu kwisha' ndipo mwanamke huyo mrembo alipotekeleza hilo na hatimaye akavamiwa na jeshi la wafilisti kumwangamizaakaamua kung'oa nguzo za jengo walimoingia akafa nao.

"Gaza is also mentioned in the Hebrew Bible as the place where Samson was imprisoned and met his death. The prophets Amos and Zephaniah are believed to have prophesied that Gaza would be deserted. According to biblical accounts, Gaza fell to Israelite rule, from the reign of King David in the early 11th century BCE"
 
Kwa hiyo vita imesimama?

Katika watu wasioaminika kabisa, jamii ya waarabu ni no.1. Na hilo alilidhihirisha hata Gadafi. Na akasema ni aheri awe mwanachama wa taasisi ya Waafrika kuliko waarabu, kwa sababu hawaaminiki na hawana msimamo.

1. Hiki ulichoandika unaweza kukitumia kupata dhamana mahakamani?

2. Wengine wanaema hivi kuhusiana na waafrika?

images.jpeg

3. Wengine wana kauli za hovyo kuhusu wanawake, wahaya, wachaga, watusi, wasukuma, wakurya, wagogo, wadigo, wazenji, nk.

4. #3 hapo ungependa kauli tata hizo zirasimishwe?
 
Ghazzat (Gaza) kuna shimo la kuzimu lisiloonekana kwa macho ya nyama na binadamu wa kawaida anapumbazwa na haiba za sura za wenyeji kutoonesha hatia usoni lakini pia wanakuvuta uwe karibu nao ili wakusome vizuri kabla hawajakuangamiza.

Delila alikuwa mwanamke mwenye asili ya jamii ya Natuf (waarabu wa Gaza) ndiye aliyeingia urafiki na Samson mwenye nguvu nying kutoka Israel jamii ya Skhul na Qafzeh hominids (Hebrania) akashawishiwa kueleza chanzo cha nguvu zake alijitahidi kudanganya lakini hatimaye akatamka kwamba 'ukininyoa nywele zangu na nguvu zangu kwisha' ndipo mwanamke huyo mrembo alipotekeleza hilo na hatimaye akavamiwa na jeshi la wafilisti kumwangamizaakaamua kung'oa nguzo za jengo walimoingia akafa nao.

"Gaza is also mentioned in the Hebrew Bible as the place where Samson was imprisoned and met his death. The prophets Amos and Zephaniah are believed to have prophesied that Gaza would be deserted. According to biblical accounts, Gaza fell to Israelite rule, from the reign of King David in the early 11th century BCE"
Wafilist sio waarabu,ni wagiriki.
 
1. Kwa hiyo huku kwenye kauli yako hii, tulimalizana?

IMG_20231221_130903.jpg

2. Kama #1 kwa hiyo sasa umekuja kiimani zaidi?

3. Kama #2 ni kweli, unasemaje kuhusu hili?

Kama Maji Maji au Mau Mau ilikuwa halali, iweje lawama kwa wapalestina?
 
Vita viendeleee washenzi wa Hamas wamalizwe kbs wao na mazalia yao maana wametuulia ndugu zetu

Pro Hamas mbona mnataka vita isitishwe na wakati nyie ndo mnasema inapoteza sana
 
Kwa hiyo ni Marekani ndio waliwatuma Hamas wakawaue wananchi zaidi ya 1,000 nchini Israel?

1. Kuingia mtegoni si lazima kutumwa ndugu; unaweza kuwa enticed; au wewe hujui hilo?

2. Kwenye matatizo ya muda mrefu baina ya Palestina na Israel:

IMG_20231213_063634.jpg

3. Marekani katega; hivyo hapa kama mbwa mwitu anayo imani kubwa kuwa windo lake litaingia mtegoni.
 
Back
Top Bottom