Jamani Bambo, pole sana! mungu akuponye haraka.
WanaJF, bado kuna tatizo kubwa na madereva wetu pamoja na miundo mbinu yetu, tena kubwa sana. Pikipiki hazijaanzia bongo jamani, kuna nchi nyingi sana kama Indonesia, Vietnam, Cambodia, South Korea, Japan na Malaysia usafiri wa pikipiki ni wa kawaida kabisa kama baiskeli mjini Shy au Tabora, lakini huwezi kukutana na ajali kila wakati.
1) Tatizo mojawapo ni madereva wetu kutojali watumiaji wengine wa barabara.
2) Jingine ni miundo mbinu yetu ni too stressful at all the time, unakuta mtu anatoka mwenge kuelekea posta anatumia zaidi ya saa moja hadi mbili.
3) Tatizo lingine watumiaje wengi wa pikipiki wanatumia hivi vifaa wakidhani ndo solution na ruhusa ya kuvunja sheria za barabarani, ndo kupenya penya kila sehemu bila kujali usumbufu unaowasababishia watumiaje wengine wa barabara, matokeo yake unakuta dereva mwingine kakomaa na upande anakoenda hapo ndo ajali kama hii inatokea.
4) Watumiaji wengi wa pikipiki hawajali wala hawana muda wa kuvaa helmet huenda sababu ya joto au kudharau sheria ambazo nazo ni chanzo cha rushwa.
Solutions:
1) Watumiaje wa pikipiki tujitahidi kukumbuka kuvaa helmet wakati tutumiapo pikipiki.
2) Tufuatane sheria kwa usalama wetu pamoja na usalama wa watumiaji wengine wa barabara.
3) Sawa, ajali haina kinga lakini wakati mwingine tunakuwa na haraka mno kiasi cha kukera watumiaji wengine wa barabara, maoni yangu watu tuheshimiane tunapotumia barabara, wote tunayo haki ya kutumia, kuishi na kufurahia kila kilichopo anapotokea mwingine anajifanya anaharaka ndo mwanzo ajali.