"Bambo" apata ajali mbaya

"Bambo" apata ajali mbaya

Duh kuna umuhimu sasa Vituo wanavyotumikia wasanii wetu hata watangazaji wamiliki wake kuona ulazima wa kuwakopesha hawa jamaa vipando vya miguu minne, japo ajali haina macho lakini kwa kiwango fulani wimbi la ajali za pikipiki ni kubwa zaidi kuliko gari na risk zake ni kubwa ulilinganisha na gari.

Wanatumia usafiri huu watangazaji wetu na wasanii kutokana na uduni wa kipato, wana majina makubwa na heshima kubwa katika jamii lakini mapato duni na wamiliki wao hata hawastuki wala kuwatazama licha ya kuwaingizia mabilioni ya fedha kwa mwaka.

Hili nalo sasa lifike ukomo, Kenya hawa watu ni lulu na maisha wanayoishi ni ya kiwango na stahiki ya hadhi yao. Muulize Parves Nagib anayeendesha Tathilia K24 baada ya kuacha sanaa bongo na kukimbilia Kenya.

Pole sana Bambo
 
Aisee....

Pole sana Bambo..... Hizi pikipiki jamani...dah!

Mungu amponye mapema
 
Aliumia kichwa ambapo kapata mtikisiko kidogo kwenye ubongo pamoja na kuvunjika mfupa wa paja la kulia.
Ameshafanyiwa operation kwenye hospitali ya mifupa ya MOI ambapo amewekewa chuma kwenye paja la kulia.
Anaendelea vizuri hapo MOI.
Mungu ampe quick recovery na abariki kazi nzito ya madokta na manesi waliomhudumia.
Hapo kwenye bold kunaweza kuleta athari za uwezo wa kuhifadhi kumbukumbu..... Tumuombee
 
kwani unadhani wanapenda kupanda hizo toyo tatizo bongo gari bado ni anasa, wewe fikiria kistarlet tu bila millioni 6 bado haujakimiliki. Boda boda zitatumaliza sana na kusababishiwa ulemavu wa viungo kwa jamii pana ya tanzania.
tatizo kubwa ni kazi za wasanii kuibiwa,hawanufaiki na kazi zao,wananufaika wengine. La sivyo hiyo jana mida hiyo ungemkuta ndani ya gari yake safi akielekea anakoelekea.
 
Duh Pole sanaa
Hii ni noma sana! Hz pikipiki kwa kweli hazifai sasa
Sijui tufanyaje mmmmh
 
hizo taarifa za kusikitisha, pole mwanakwetu. La Bambo limevuma kutokana na umaarufu wake. Japo nahisi, kwa siku hiyo inawezekana ajali zilikuwa kadhaa, na majeraha makubwa zaidi. Ni tatizo kubwa zaidi ya inavyodhaniwa. Kukosekana kwa mkakati maalumu kulidhibiti, je, ni kwa sababu tumejenga utamaduni wa kushtushwa na idadi ya majeruhi kwa tukio au? Je chanzo ni vyombo vyenyewe, madereva, abiria, wamiliki, mfumo wa sheria, miundombinu au wasimamizi na watekelezaji wa sheria.!? Tunatakiwa kulishughulikia.
 
Pole sana Bambo. Pole sana mwenzake Bambo. Mwenyezi Mungu awasaidie mpone haraka. Poleni sana.
 
Back
Top Bottom