Balozi wa REDDS 2008 arejesha Taji na Zawadi

Jamani inashangaza watu wengi wanazungumzia shinikizo la wazazi, kwa tukio lenyewe lilivyokwenda sioni dalili za shinikizo la mzazi/wazazi, pengine shinikizo la waumini/muumini katika kanisa lao, hapo yawezekana. nasema hivyo kutokana na kwamba wazazi wote walikuwepo kwenye kutunukiwa na kumpongeza sasa hilo shinikizo limekuja lini??? baada ya kufika nyumbani ama wapi?, mimi sioni hata mmoja kati ya wazazi wake kuwa ni muumini wa kweli katika imani za dhati ya kuabudu.
 
Kipanga, I cannot invest so much emotion in beauty pageants, lakini naona ishu hii imekugusa sana, hivyo naomba bila jazba na matusi nikujibu kiutu uzima Kabla ya yote naomba nitofautishe mada hapa. Kuna suala la mrembo binafsi na imani yake ya dini. Kuna suala la investment kwa upande wa waandaji. Kuna suala la mikataba.
Sasa naomba tuanze na imani ya binti ambayo ni eneo nililotumia kumsifu binti huyu. Imani yake binti ni private matter. Anaweza akawa ameshindana na kutokana na factors mbalimbali akaona kwamba alichokifanya ni kinyume na imani yake. Hivyo akajitokeza hadharani na kusema hataki taji na kulirudisha. Mi namsifu kwa sababu ni kheri afanye hivyo kuliko kuanza kuwapiga chenga waandaji, kutafuta vijisababu vya kutoshiriki au kuleta vituko na kuzima simu eti hapatikani kwenye shughuli mbalimbali. [Nakumbuka Nancy Sumari aliwafanyia hivyo waandaji mpaka wakaandikana kwenye magazeti, Mrembo huyu wa mwaka jana, Radhia naye hajafanya shughuli zozote za kijamii] Like this it is straight forward na Angela anampatia nafasi mrembo mwingine ambaye atafanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu. Ndiyo maana nimemsifia dada, amekuwa mwazi na hajapindisha.
Investment kwa upande wa waandaji: Waandaji waliandaa hafla mbalimbali, lakni ni hafla moja tu ambayo iliandaliwa specific for Angela, ni ile iliyofanyika wiki iliyopita ya kupokea taji kutoka yule mshindi wa 2007. Gharama zingine za fainali ya Miss Tanzania walipomtangaza, fashion show ya Redds iliyofanyika Mwanza, haziwezi kuhesabika maana shughuli ingefanyika whether Angela angeshiriki au la. Kama wana mpango wa kumdai compensation, nadhani this is the only area wanaweza kumdai (kukabidhi taji). Zaidi ya hapo, alikuwa ni mmoja ya washiriki. So hakuna investment kubwa iliyofanyika kwa upande wa Redds.
Mikataba: Kama Redds na Lino wanafanya shughuli hizi bila mikataba basi nitawashangaa sana. Redds huu ni mwaka wao wa 3 au 4 wanatoa taji, Lino ni miaka 10 na kitu wanaandaa Miss Tz na hawajajifunza kusaini mikataba na warembo? Kwa kweli hii si fundisho tosha. Ndiyo maana kumbe wanashindwa hata kumvua taji washindi wao wanaoboronga? Maana hawana legal premise ya kufanya hivyo!? Sasa kama ni kweli hawana mikataba hii fundisho haijawagharimu vya kutosha. Maana wana bahati dada huyu alikuwa mstaarabu.
...

Susuviri,
Tunawekana sawa mazee sioni kama kuna jazba au matusi kukosa busara au hekima kupo na watu wa aina hiyo wapo so sorry mkuu kama imekukwaza. Lakini narudi katika hoja zako 3 yaani imani Angela, Investment kwa waandaji na Mikataba. Mtu ana haki ya kuamini vile anavyoamini na kwa ukweli bado sioni mantiki ya Angela kurudisha taji na zawadi kwa kigezo cha imani yake. Kama ulivyosema mwenyewe Redd's wamekuwa na hili shindano kwa karibu mwaka wa 3 au 4 that means hata yeye alijua wazi kuwa akishiriki mashindano ya urembo wa Tanzania lazima kipengele cha kumtafuta mrembo wa Redd's hawezi kukiepuka so alikuwa na muda wa kuamua haikuwa ghafla kama moto umelipuka. Alipanda ndege toka Dar mpaka Mwanza alielewa kinachoenda kufanyika huko na imani yake ilikuwa iko vizuri tu wakati huo so again alitakiwa kuamua mapema kushiriki au kutoshiriki.

Investment kwa waandaji.. Ni kweli waliandaa hafla moja ya kumvisha taji Angela kwa kuwa amerudisha taji na zawadi. Sasa mrembo atakayechaguliwa tena na TBL (sijui kwa style ipi) atavishwa taji mbele ya waandishi wa habari au kwenye ofisi za TBL??? au naye itabidi afanyiwe hafla???

Mikataba; Kwa hili sina uhakika na uendeshaji wa mashindano kama washiriki husaini mikataba yoyote may be Bw. Lundenga au yeyote anayefahamu atufahamishe lakini suala ni kuwa kama kuna makubaliano baina ya pande mbili nadhani ni wajibu kwa kila upande kuheshimu unless kuna sababu za maana sana. Mimi si mwanasheria lakini kwa mtazamo wa kawaida tu Angela alikosea, kwa mfano warembo walielezwa mapema kuwa mshindi wa Redd's atapata zawadi ya Sh. 2.5ml na mambo mengine then ikawa Angela ameshinda na TBL hawakumpa zawadi kama walivyoahidi ungeichukuliaje wewe????
 
Mambo matata na utatanishi mkubwa... Sikujua kama kuna makanisa yanakubaliana na mchakato mzima wa mashindano ya Ulimbwende lakini yanagomea suala zima la kuhusiana na Pombe...

Kweli kuna utata katika dini zetu.!

Mkuu Mzozo

Hapo umeongea, hivi inaingia akilini kweli mtu kushiriki mashindano ya ulimbwende halafu ukatae zawadi za pombe?, maana nafikiri kushiriki tu ni mbaya zaidi ya pombe, mavazi ya kuogelea kupita mbele za watu, na je angeshinda kwenda Miss World ambako vichupi vinatawala angesemaje?. Mi nafikiri huyu binti huenda aliingia bila kuwataarifu waumini wenzake kuhusu ushiriki. Au ameombewa baada ya kupotea na sasa anarudi kundini. Huu ni upuuzi mkubwa sasa kambania mtu zawadi hiyo?. Next time kina Lundenga watoe form za hawa kujaza kama wanafungamana na imani yoyote kali kabla ya kuwa shortlist.
 
....
...Khoryere, alichofanya binti si sahihi na ni uvurugaji wa tukio zima la kumpata huyo mrembo wa Redd's na wala msitake kumsifu kuwa eti amefanya jambo la ujasiri si kweli kumbuka imeripotiwa kuwa aliamua kurudisha taji na zawadi baada ya baba yake ambaye ni mchungaji kubanwa huko kanisani kwake kwa nini binti amekubali kuwa mrembo wa redd's.

Nina imani kama baba wa huyo binti asingewekwa kiti moto huko kanisani asingerudisha taji na zawadi ukizingatia kuwa kinywaji cha redd's kinafahamika kwa watu wengi na kwa muda mrefu sitaki kuamini kuwa walikuwa yeye na wazazi wake kuwa hawakuelewa kuwa redd's ni pombe. Nadhani ni fundisho kwa Lundenga na kamati yake kuwa makini na hao mabinti wanaowachukua kushiriki hayo mashindano kwa vigezo vya imani na idhini ya wazazi kuliko kuwapotezea watu muda na kuharibu hata sifa ya mashindao yenyewe ni uswahili tu hapo hakuna cha kumpongeza ikibidi Lino na Redd's wamshitaki tu huyo mrembo kwa alichofanya ili iwe fundisho kwa wengine!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sipingi kama Redds au kina lundenga wamekwazwa na angela wachukue hatua za kisheria lakini navojua mambo yetu yanavofanywa kienyeji sidhani kuna mkataba unaombana angela,tusubiri tuone au waanze 2009
 
kwani ulipokuwa unagombania hukujua unagombania kuwa nani!!! hii kali alafu umekaa baada ya wiki eti unarudisha pesa umeambiwa utatengwa nini kanisani!!!!!!!!!
 
dada huyu alichemsha saaana.
mimi siamini kwamba kuna dini inaruhusu kabisa mtu aende katika mashindano ya urembo. Kumbuka kuna kuvaa vile vinguo vya kuogelea (hata kama hapa TZ wamekataa lakini huko ktk mashindano ya dunia bado vipo). Mashindano yenyewe yanadhaminiwa na kilevi - Redds . Alikuwa na miezi kadhaa ya kutafakari kabla ya kushiriki !

ameamua kushiriki, ameshinda, ameshangilia, amevikwa taji, kupewa zawadi, nk. then all of a sudden eti yeye ni mlokole ! ulokole gani huu. Kwa yesu unatakiwa uwe "moto" au "baridi" na sio uvuguvugu. ashindwe na alegee. anyway tunamsamehe kwa vile amegundua kosa na kumrudia muumba wake.

Bint amechanganyikiwa!!

Hebu nenda hapa

http://dailynews.habarileo.co.tz/st...ador2008AngelaLubalaTalksOnHerTitle.flv&id=46
 
Back
Top Bottom