BALOZI wa REDDS 2008 Angela Luballa ametamka rasmi leo kwamba ameamua kurudisha Taji hilo la Balozi wa kinywaji cha Redds wa Mwaka 2008 ambalo ni wiki moja tangu avalishwe kwenye mashindano ya kumtafuta Miss Vodacom Tanzania 2008.
Luballa ambaye pia alishika nafasi ya tatu katika shindano la kumsaka Miss Tanzania, amesema kuwa imani yake haimruhusu kuwa Balozi wa REDDS.Imani yangu kwa Yesu ni kubwa mno na hainiruhusu mimi kuwakilisha REDDS, hivyo nimeamua kurejesha taji na zawadi za fedha nilizopewa,alisema Luballa. Nimerudisha taji hili si kwa shinikizo la mtu yeyote bali ni imani yangu, siwezi kuwa balozi wa REDDS.
''Luballa ambaye inaaminika ni mtoto wa mchungaji ana imani ya kanisa lao ambalo haliruhusu kujihusisha na kitu chochote kinachohusu pombe. Luballa anasali katika Kanisa la World Alive International Outreach lililopo Sinza. Mrembo huyo alisema kuwa tayari ameshaiarifu Kamati ya Miss Tanzania na kurudisha taji na fedha Sh milioni 2.5 alizopewa kwa kutwaa taji hilo.
Source: Haki-Ngowi