Malengo ya uwekezaji wa China barani Afrika yanaendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111255042081.jpg

Baada ya China kupata maendeleo makubwa ya kiuchumi, nafasi yake ikiwa kama nchi mkopeshaji imeongezeka na kuwa mbele duniani. Malengo ya sera ya uwekezaji wa China kwa nchi za Afrika yanaendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030, na China inaonekana kuwa mchangiaji mkubwa ambaye anaziba pengo la fedha za maendeleo ya Afrika ambayo yatakuwa na manufaa katika kutoa sera za maendeleo duniani.

Hivi majuzi Idara ya Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa ya Taasisi ya Uchumi wa Muundo Mpya katika Chuo Kikuu cha Peking, imezindua ripoti kuhusu uwekezaji na mikopo katika nchi za Afrika. Ripoti hiyo iliyopewa jina la “Uchunguzi juu ya Ufanisi wa Ufadhili wa China katika Afrika, inaonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2006, hasa baada ya msukosuko wa fedha wa mwaka 2008, uwekezaji umeongezeka kwa kasi na kiasi kikubwa, ambapo katika miongo miwili iliyopita kutoka mwaka 2000 hadi 2020, China kwa ujumla imetoa ufadhili wa dola za Kimarekani bilioni 160 kwa nchi za Afrika, huku mingi 90% ikienda katika nchi zenye mapato ya chini na kati.

Ripoti hiyo pia imeweka wazi takwimu zake juu ya athari chanya za mikopo ya China kwa ukuaji wa uchumi wa Afrika, ambapo zinaonesha kuwa umiminikaji wa uwekezaji na mikopo umekua kutoka asilimia 0.176 hadi 0.300, ikiashiria kwamba ongezeko hili la mikopo la asilimia 1 limechangia ukuaji wa uchumi wa Afrika kwa asilimia 0.176.

Akiwa miongoni mwa jopo la wataalamu waliojadili ripoti hiyo balozi wa Zambia nchini China Ivan Zyuulu amesema China imefanya mambo mengi makubwa katika kulisaidia bara la Afrika, hata hivyo ameshauri kwamba uwekezaji pia uongezwe zaidi kwenye sekta ya kilimo.

Kwa maoni yake anaona kuwa kuna matokeo madogo sana kwenye uwekezaji wa sekta ya kilimo. Ikizingatiwa kuwa kilimo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa nchi nyingi za Afrika, ndio maana anaona kuna haja kubwa ya kuleta matokeo zaidi katika upande huo.

Ingawa nchi za Afrika sasa zinawekeza zaidi kwenye miundo mbinu, lakini ni matarajio ya Waafrika wengi kuona miundo mbinu hii inasaidia bidhaa za kilimo kuhama na kuingia maeneo yenye mahitaji zaidi na yenye walaji, na hicho ndio kilimfanya balozi Zyuulu atilie mkazo zaidi juu ya eneo hili. “Hili ndio eneo ambalo linahitaji uungwaji mkono zaidi kutoka China na tunataka kuona sekta ya kilimo inaendana na uwekezaji wetu” alisema balozi Zyuulu.

Akijibu kuhusiana na wasiwasi wa balozi Zyuulu wa kutowekeza zaidi kwenye sekta ya kilimo, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mambo ya Afrika ya Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Wu Peng, alisema katika miongo kadhaa iliyopita China imeazimia kutoa ushirikiano kwenye sekta hii ya kilimo, ambapo katika zaidi ya miaka 40 iliyopita serikali ya China ilituma timu ya wataalamu wa kilimo katika nchi za Afrika, na hata mwaka uliopita China pia ilianzisha viwanda vitatu vya kusaga mahindi nchini Zambia. Aidha katika wizara ya rais wa Zambia Hakainde Hichilema nchini China aliyofanya mwezi uliopita, Bw. Wu anasema walijadili namna ya kuchangia zaidi aina hizi za viwanda vya kusaga mahindi nchini Zambia.

“Halikadhalika kwa upande wa China pia inaruhusu bidhaa za kilimo za Afrika kuweza kuingia kwenye soko letu. Nakuhakikihsshia kuwa blueberry na asali am ahata na bidhaa nyingine za kilimo za Zambia zinaweza kusafirishwa na kuingia kwenye soko la China”. Alieleza Mkurugenzi Wu.

Kwa kuwa China inafahamu kuwa nchi za Afrika zinategemea sana kilimo kama nguzo yake kuu, imekuwa ikihamisha ujuzi wake na kupeleka wataalamu ambao wanatoa mafunzo ya kutumia mbinu bora za kuboresha kilimo. Hata kwenye hotuba yake wakati wa Mazungumzo ya Viongozi wa China na Afrika mjini Johannesburg, yaliyofanyika mwezi wa nane mwaka huu, Rais Xi Jinping wa China alisema China iko tayari kuanzisha Mpango wa Kusaidia Maendeleo ya Viwanda barani Afrika, ambao utasaidia Afrika katika kukuza sekta yake ya viwanda na kufikia ukuaji wa viwanda na uchumi mseto.

Hakuishia hapo bali pia alisisitiza kuwa China itaanzisha Mpango wa Kusaidia Uboreshaji wa Kilimo cha kisasa wa Afrika, na kuisaidia Afrika kupanua mashamba ya nafaka na kuhimiza kampuni za China kuongeza uwekezaji wa kilimo barani Afrika.
 
Attachments

  • VCG111175893359.jpg
    VCG111175893359.jpg
    90.7 KB · Views: 2
View attachment 2809251

Hakuishia hapo bali pia alisisitiza kuwa China itaanzisha Mpango wa Kusaidia Uboreshaji wa Kilimo cha kisasa wa Afrika, na kuisaidia Afrika kupanua mashamba ya nafaka na kuhimiza kampuni za China kuongeza uwekezaji wa kilimo barani Afrika
Mkuu unamaanisha as bantu people's can we trust this Beijing authority.
Hv ushawahi kuhudhiria vikao vyao vya siri ndani ya baraza kuu la kikomunisti na kusikiliza ajenda za mihuri kuhusu afrika?
Don't trust too much 100% Beijing authority.
 
Back
Top Bottom