Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,016
- 9,884
Katika mkutano wa wadau wa Demokrasia ulioandaliwa na TCD, Balozi wa Marekani Nchini Tanzania, Michael Battle amesema demokrasia sio lazima ifanane kwa kila nchi, lazima kila demokrasia izingatie mazingira yake.
Amesema demokrasia ya Tanzania, inabidi izingatie mazingira ya Tanzania, ifanane na Tanzania.
Aidha ameisifu Tanzania kuwa imekuwa ikipiga hatua vizuri, na wao (Wamarekani) wataendelea kuwa washirika wa Tanzania ili kusaidia kukuza demokrasia nchini.
Marekani ni moja kati ya wadau waliofadhili mkutano wa demokrasia wa mwaka huu, ambao kwa mwaka huu mgeni rasmi ni rais wa Zanzibar, Hussein Ally Mwinyi