Kwa Kauli hii ya Balozi wa Marekani Kuhusu Demokrasia, CHADEMA Wameumbuka

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Marekani Kupitia Balozi wake Nchini Tanzania amesema Demokrasia ya Kila Nchi lazima iendane na mazingira na tamaduni za Nchi husika.

Balozi alikuwa akizungumza kwenye kikao Cha wadau wa Demokrasia Tanzania..

Kwa msimamo huu wa marekani ni wazi Mabeberu wanamuelewa Rais Samia na kuwatupia virago Wapinzani uchwara.
---

Balozi wa Marekani, Dkt. Michael Battle: Demokrasia ya Tanzania ifanane na Tanzania
Balozi wa Marekani, Dkt. Michael Battle amesema si lazima demokrasia ya nchi moja ifanane na ya nchi nyingine kwani demokrasia inapaswa kuwa ya kipekee iliyoundwa na nchi husika.

Akizungumza katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Demokrasia ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) jijini Dar es Salaam amesema Demokrasia ya Tanzania inapaswa kuzingatia mazingira ya Tanzania.

“Ni muhimu kufahamu kwamba kila demokrasia haionekani sawa, kila demokrasia haipaswi kuonekana sawa, demokrasia lazima iangalie mazingira ya nchi. Demokrasia ya Tanzania haitakuwa mfumo wa utawala wa kifalme, demokrasia ya Tanzania lazima ifanane na Tanzania yenyewe, lazima ionyeshe utamaduni wa Tanzania, lazima iwe ya Tanzania pekee, lazima iwe milki ya Watanzania, lazima iundwe na Watanzania.

Demokrasia ya Tanzania lazima iwe ya kwake yenyewe na hakuna taifa lingine duniani linalo haki ya kuamulia Tanzania jinsi inavyopaswa kuwa,” amesema.

My Take
1. Hii Kauli ni msiba na nyundo ya utosini Kwa Chadema ikipigilia msumari Kauli ya Kinana kwamba Demokrasia na Uhuru lazima uwe na mipaka,matusi sio utamaduni wa Tanzania na kamwe haiwezi kuwa Demokrasia hapa kwetu.

2. USA anabadilo sera ya Nje Ili Kukabiliana na ushawishi unaokua wa Russia na China.
 
Japo Siungi Mkona Upande Wowote Ila Huyo Balozi Ni Kopo Haelewi Anachoongea Au Hakuielewa Maada,ndio Wale amepewa Jezi Na Kuvaa Na Mchezo Haujui.
Wewe Ulieandika Huu Uzi Je Unaona Kuna Ukweli Hapo?
Tuambie Ni Maeneo Gani Yanaonyesha Democracy Imekua?
Usije Ukasema Kisa Kuna Mikutano Ya Hadhara Iliyofunguliwa.
 
Hii itakuwa imefika kunako 🔨🔨
 
Balozi Michael Battle amesisitiza watanzania ndiyo wenye kujua hatima ya demokrasia ya Tanzania ya kuwa na watu-huru, uhuru, haki, demokrasia na maendeleo ya watu wake iweje kwa kuwa nchi duniani zinatofautiana katika values yaani mila, tamaduni, desturi hivyo wasiigize demokrasia za nchi zingine

View: https://m.youtube.com/watch?v=pNa6Oi4QOdA

More info :

Hotuba ya Balozi Dr. Michael A. Battle akijitambulisha mara baada ya kufika kituo cha kazi Tanzania :

Balozi Dr. Michael A. Battle ameitumikia nchi yake ya Marekani kwa zaidi ya miaka 40 na amewahi kutumikia jeshi la nchi yake kama kasisi jeshini chaplain in the US Army , kutumikia wizara ya mambo ya nje na pia kama mwalimu katika vyuo vikuu kadhaa nchini Marekani.

View: https://m.youtube.com/watch?v=8xZyDweh_G0&pp%3D
 
Demokrasia ya Tanzania ipoje ?
Kuiba kura za wananchi, kuharibu chaguzi zote na kujaza bungeni vihiyo kama akina Msukuma.

Rais wa nchi awe mungu mwenye uwezo wa kuuza maliasili za nchi yake kwa yeyote anayemtaka yeye bila kuhojiwa na yeyote.

Rais huyo anaamua yeye, kila jambo, hata liwe dogo. Akisema anataka Zanzibar wasilipie umeme, inakuwa hivyo, hakuna wa kuhoji.

Hii ni nchi ya demokrasia hii; huu ndio utamaduni wetu tunaotakiwa kuuenzi na wengine watutambue hivyo duniani?

Simlaumu Balozi, kwa sababu hakuwa na maana hiyo, ambayo baadhi ya wapumbavu hapa wanataka tuamini alikuwa na maana hiyo.
 
Huyu mpuuzi mleta uzi anatumia maneno ya balozi kwa matumizi ya ukunguni wake usio na tija
 
Huyu mpuuzi mleta uzi anatumia maneno ya balozi kwa matumizi ya ukunguni wake usio na tija
Hawa watu sasa wanatapatapa na kuhaha kila sehemu.
Ni kama wamechanganyikiwa.

Ukimsikia rais anazungumza vimaneno visivyo na maana yoyote, tena kwenye hadhara kubwa kama ile ya KKKT, unajua kuwa sasa hawajui wafanye nini.
 
Balozi ni mnafiki. Marekani ndiyo inaongoza duniani kwa ku-engineer mapinduzi kwenye nchi mbalimbali kwa kisingizio cha kueneza demokrasia. Unawezaje kutumia mtutu wa bunduki kueneza demokrasia? Demokrasia gani hiyo ya kuenezwa kwa mabavu?

Kwa kufadhiri kupinduliwa kwa rais wa Ukraine aliyekuwa madarakani kwa kuchaguliwa na wananchi, hiyo ndiyo demokrasia? Angalia mifano ya Libya, Tunisia, Syria, Iraq, nk, ndipo utajua kuwa huyo balozi hakuongea kitu cha kweli.
 
Back
Top Bottom