Balali yuko HAI - He is not dead

Status
Not open for further replies.
Nyamtoroka, heshima mbele!!!!!!
Naomba kuuliza na kuweka historia vizuri. Sehemu kubwa ya wizi wa EPA ulifanyika mwaka 2005, na fedha hizi zinadaiwa kumweka madarakani rais J.K. Safu ya uongozi ya mwaka 2005 katika CCM, Mwenyekiti alikuwa Mkapa, Makamu bara Malecela, Zanzibar akiwa Karume. katibu wake alikuwa Mangula na idara ya fedha na uchumi ilikuwa chini ya Marehemu Salome Mbatia. Kipindi kile Zakia Megji hakuwa katika kamati kuu ya chama bali alikuwa waziri wa maliasili na utalii. Najua naye ni mchafu sana hali iliyopelekea kuondolewa uwaziri wa fedha. Ila mwaka 2005 nadhani hakuhusika, huo ni uelewa wangu, kama ni tofauti naomba ufafanuzi.

Masaiti.....
 

Haina tija kwa sasa.
 
Ndg.yangu mtotowamjini umesahau kuwa CCM ina wenyewe?
 

Huo ndiyo ukweli, tusiwe tuaweza siasa katika masuala ambayo yanaweza kuelezeka hata mtu ambaye hakwenda shule. Majungu, fitina na chuki binafsi za nini?
 

Maneno kama hayo bila shaka yatakuwa yanasemwa na vijana wa CHADEMA kuwa yafaa sasa SLAA awapishe vijana ili kupiga hatua moja mbele, lakini kila chama kina wazee ambao ni nguzo za vyama vyao, tunapowashambulia wazee wa CCM ni sawa na memo NYANI haoni ku........le.
 

Noted.......Asante kwa kuongeza nyama....so what you are saying ni kwamba ni mchafu na hakufaa kuwepo ila ni kwamba hakuchafua wakati ule.........au sijakuelewa vizuri?????

Kujenga na kubomoa yote ni matendo katika ujenzi na hufanywa na fundi ila matokeo ndo huwa tofauti.....!!!!!
 

Namg'atuka,

Be realistic please, mtoto wa mjini ametoa maoni yake wewe yajibu na siyo kusema atakuwa ni mwana Cdm. Jibu hoja na siyo kukimbilia vyama. Elezea kuwa Mangula na CCM hawakuhusika na rushwa ya EPA, Zakia Meghji hakuwahi kuwa fisadi, hajawahi kuiba vitalu, hajawahi kusaini viti asivyovijua na kudai Balali alinidanganya. Kwa maoni yangu Kinana, Mangula na Megji hawafai kuwa viongozi wa chama, kwani mikono yao inanuka ufisadi. (Tukiacha na mambo mengine yao binafsi). Wako wengine walio wazuri mfano Shein, Migiro nk, hawa hawana/ hatujasikia kashfa yao ya rushwa. Na ndio maana watu hawawasemi, lakini watuhumiwa wa rushwa tutawasema mpaka kesho, hata na vizazi vijavyo vitasema. Tukianza U-CDM na U-CCM hatutafika mbali.
 
Mama mkwe yule jamani.
Mwacheni apumuwe.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Dr. Balali R.I.P
Alishaondoka duniani kiukweli baada ya kuondoka Tanzania ambapo tulitangaziwa kuwa ameondoka duniani. End of October and last year hivi
 

Olesaidimu,

Kama post yangu hapo juu nilivyosema, Megji ni mchafu, tena sana. Ana tuhuma nyingi za kifisadi na hivyo hafai kabisa kuwa kiongozi wa chama. Ila katika ufisadi wa EPA nadhani tutakuwa tunamwonea huyu mama, ingekuwa kuuza vitalu, mikataba mibovu aliyoingia akiwa waziri wa fedha nk, hapo ningekuelewa na siyo EPA
 

Mkuu Masaiti

Sisi kama wazalendo wa nchi hii kwanza ni kukataa wacahfu wote halafu kama inafika sasa kuanza kuwapanga kwa mafungu ya tuhuma hiyo ni next step kwa sasa kazi ni moja........

Wasafi pita huku.......mliobaki tokeni nje kwanza na mpige magoti
Tukimaliza na wasafi then tunatoka nje na kuwapanga kwa makundi ya uchafu wao huko huko juani.......in rows and columns for easier interpretation.....
 
We wadhan hata ukimwuliza atajibu nn? Sitegemei jibu lolote la maana.....
jamani! pinda alishasema balali kafa na anayebisha hajafa aonyeshe alipo.kisha akaonya kumjadili marehemu.
 
jamani! pinda alishasema balali kafa na anayebisha hajafa aonyeshe alipo.kisha akaonya kumjadili marehemu.


Nani kakudanganya!!? Marehem huwa ana-tweet? Mdingi mzima wa afya anakula pensheni na kumalizia alizotuibia!!! Hiyo ni Tz mkuu.
 

Mama mkwe amewekwa kulinda maslahi ya mkwe"
 
Nani kakudanganya!!? Marehem huwa ana-tweet? Mdingi mzima wa afya anakula pensheni na kumalizia alizotuibia!!! Hiyo ni Tz mkuu.

Hata mimi nimemwona akitweet, lakini tuna uhakika gani kama ni yeye? kwani mtu yoyote anaweza kusign kwa jina la Balali.
 
MAAJABU😀AUDI BALALI AIBUKA NA KUDAI KUWA YUKO HAI HUKU AKITABIRI ANGUKO LA CHADEMA






Wote tunafahamu kuwa aliyekuwa gavana wa benki kuu ya Tanzania Daudi Balali alifariki dunia tarehe 16.05.2008 huko Boston, Marekani na kuzikwa huko huko.


Lakini kwa watumiaji wa Twitter watakuwa wanamfahamu Daudi Balali wa kwenye mtandao huo ambaye ameendelea kumuumiza vichwa vya watu wengi kuwa ni nani huyu aliye nyuma ya akaunti hiyo na akiendelea kudai kuwa bado yupo hai?


October 1 alitweet, “Nitakutana na Rais Kikwete na ujumbe wake wiki hii hapa Marekani."

Anavyoonekana ni msomi haswaa na anaishi nje ya nchi. Ni mtu makini, ana hoja, anaijua siasa ya Tanzania na yupo consistent! Hivi karibuni mtu huyo alidai kuwa amekuja Tanzania na kulala kwenye hoteli iliyo karibu na ofisi yake ya zamani.


“In Dar es Salaam, Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kempinski Kilimanjaro Hotel. Feels good to be close to my former office, BoT,” alitweet November 13.

Kutokana na kile anachokiandika anaonekana kuwa ni kada mzuri wa CCM na leo ameibuka na kutabiri anguko la CHADEMA kwa kutweet,“Chadema will die by disintegration. Zitto Kabwe and 3 other prominent members will move to CCM,the rest will form 2 new political parties."

Anasema CHADEMA itavunjika ambapo Zitto Kabwe na wanachama wengine watatu wa chama hicho watahamia CCM na wengi wataanzisha vyama viwili vipya vya siasa.
Hata hivyo anadai ameamua kuondoka nchini mapema na kurudi Gaithersburg, Maryland kutokana kuhofia usalama wake.

“I am leaving Dar es Salaam tonight instead of Wednesday on security reasons.”

Mwisho ameendelea kusisitiza kuwa kweli yupo hai kwa kutweet:

I AM REAL. TAKE IT OR LEAVE IT. TWITTER IS THE MESSENGER. THE SURPRISE IS YET TO COME.
​
http://freebongo.blogspot.com/2012/11/maajabudaudi-balali-aibuka-na-kudai.html


 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…