Unajua yote mawili yanawezekana kabisa. Huyu jamaa inawezekana kabisa yuko hai au kweli amekufa. Lakini siku zote ukweli hujidhihirisha, ipo siku kama kweli huyu jamaa yuko hai, atajitokeza hadharani tu. It's just a matter of time. Kama kweli amekufa pia tutajua tu. Kuna watu hawana kazi za kufanya, watu hawa hutumia majina ya watu wengine kwenye mitandao kwa kujifurahisha wao na kuwachafua wengine. Mtu yeyote anaweza kuingia kwenye mtandao na kutumia jina la mtu yeyote yule awe hai au amekufa. Mimi binafsi sishangai kabisa. Inawezekana Balali akawa hai some where, Serikali nyingi duniani zina uchafu mwingi sana.