BAKWATA yamsafisha Mwalimu Julius Nyerere

BAKWATA yamsafisha Mwalimu Julius Nyerere

Kwenye maelezo yake amesema kuwa ni Waislamu wenyewe toka nchi nzima walionesha kutokuwa na Imani na EAMWS. Ingawa ameelezea jinsi Aga Khan alivyokuwa yupo tayari kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa waislamu.

Chanzo ni Gazeti la Mwananchi na siyo mimi!
Na miradi ikataifishwa na serikali.
 
Ugumu unauleta wewe. Mimi sijauliza swali bali nimeleta habari ya Omary Nzowa. Mzee Mohamed anaelezea upande wake anavyolifahamu jambo hili, na mwenyewe kasema kasoma habari niliyoleta. Kusoma Kitabu litakuwa ni suala langu binafsi na JF siyo mimi bali kuna wengi wanataka kujua mtizamo wa Mzee Mohamed hapa JF na si kwenye kitabu chake.
Narudi tna baadhi ya maswali yko majibu yke yapo ndani ya kitabu kwa hiyo unakuwa km unarudisha nyuma mjadala...
 
Angalau amefafanua maana zile hadithi za EAMWS zilituchanganya sana huenda ilikuwa propaganda tu.
Hiyo ni kawaida, ila wakija kujutajia mali zao zilizotaifishwa ndio utajua kama hadithi za EAMWS ni vigano au visasili.
 
Nantahulila Mohamed Said anataka kututoa nje ya mada. Mada hapa ni kwamba Nzowa kasema ni waislam wenyewe ndiyo walianzisha BAKWATA na si Serikali. Yeye Mzee Mohamed anasema ni Nyerere ndiye aliamuru EAMWS ivunjwe na ianzishwe BAKWATA. Sasa inatakiwa Mzee Mohamed aseme kama mkutano wa Iringa siyo ulioanzisha BAKWATA.

Lakini kuna hoja ya U- suni na U- Isimailia. Waislamu wengi sana Tanzania ni wasuni. Ingewezekanaje wakubali kuongozwa na Muisimailia!?

Halafu kusema tu kwamba zilitolewa rushwa za shilingi 40,000 bila ya kutaja mwaka zilipotolewa hizo fedha mzee wetu atakuwa hatutendei haki!!

Swali gani kwa mfano? Mambo ya EAMWS, Aga Khan na mengineyo yanatokana na makala ya Gazeti la Mwananchi.
 
Nantahulila Mohamed Said anataka kututoa nje ya mada. Mada hapa ni kwamba Nzowa kasema ni waislam wenyewe ndiyo walianzisha BAKWATA na si Serikali. Yeye Mzee Mohamed anasema ni Nyerere ndiye aliamuru EAMWS ivunjwe na ianzishwe BAKWATA. Sasa inatakiwa Mzee Mohamed aseme kama mkutano wa Iringa siyo ulioanzisha BAKWATA.

Lakini kuna hoja ya U- suni na U- Isimailia. Waislamu wengi sana Tanzania ni wasuni. Ingewezekanaje wakubali kuongozwa na Muisimailia!?

Halafu kusema tu kwamba zilitolewa rushwa za shilingi 40,000 bila ya kutaja mwaka zilipotolewa hizo fedha mzee wetu atakuwa hatutendei haki!!

Mag3 Nguruvi3
Allen,
Nadhani nimekushauri usome kitabu cha Abdul Sykes ambamo
haya yote unayouliza hapa nimeyaeleza kwa undani kabisa.

Kulikuwa katika kundi la Adam Nasibu afisa wa serikali ambae
ndiye alikuwa mshauri mwelekezaji wa mbinu na propaganda dhidi
ya EAMWS na viongoi wake.

Katika kitabu nimemtaja jina na nimeeleza nini kilimfika baada ya
kukamilisha kazi yake.

Huyu alikuwa Muislam.

Katika kitabu nimewataja watu wawili wenye vyeo vya juu katika
vyombo vya habari radio na gazeti ambao walifanya propaganda
kubwa dhidi ya EAMWS kwa kuwapa nafasi kundi la Adam Nasibu
kujitangaza na kusema uongo mwingi.

Mmoja katangulia mbele ya haki mwingine yu hai hadi hivi leo.
Majina yao yapo katika kitabu.

Hawa si Waislam.
Halafu kulikuwa na huyu ''paymaster,'' ambae nishamtaja.

Unataka mwaka wa haya yalipotokea.
Haya yote yalikuwa miezi mitatu ya mwisho mwaka wa 1968.

Kwa uhakika tarehe 24 October, 1968 ndipo Adam Nasibu katibu
wa EAMWS Bukoba alitokea katika magazeti akiwashambulia
viongozi wa EAMWS na kutangaza Bukoba kujitoa katika EAMWS.

Ikiwa unataka kujua fedha za kumwezesha kufanya haya yote
zilianza kutoka lini basi tunaweza kusema ilikuwa kuanzia mwezi
Oktoba, 1968.

Adam Nasibu mwalimu wa shule ya msingi ghafla akawa ana uwezo
wa kukodi ndege akisafiri nayo kwenda huku na huko na kupanga
hoteli nzuri zenye sifa.

Swali la kujiuliza ni fedha hizi alikuwa anazitoa wapi?

Hiki ni kipindi muhimu sana katika historia ya Waislam wa Tanganyika.

Sheikh Hassan bin Ameir katika darsa zake alikuwa akiwaambia
wanafunzi wake wamtegemee Allah, Hakimu Muadilifu.

Huu ndiyo ulikuwa uradi wake.
Hakika Allah alipitisha hukumu na wengi tuliishuhudia kwa macho yetu.

Mara nyingi ninapohadhir ninapofika katika historia ya Sheikh Hassan
bin Ameir
katika kipindi hiki cha kuundwa BAKWATA wasikilizaji wengi
hububujikwa na machozi.

Ajabu sana.
 
Wakati baadhi ya watanzania wakisubiri taarifa kutoka kwenye kile kikao cha wafanya mazingaombwe maarufu wa Tanzania, leo Gazeti la Mwananchi limechapisha mahojiano kati yake na Mdhamini wa BAKWATA, Omary Nzowa.

Katika makala inayoelezea Historia ya kuanzishwa kwa Baraza Kuu La Waislamu Tanzania (BAKWATA) Omary Nzowa amekanusha habari kwamba Baraza hilo lilianzishwa kwa shinikizo la Serikali zama za Mwalimu akiwa ndiye rais wa Tanzania.

Omary Nzowa amesema hoja ya kuanzishwa kwa BAKWATA na kutoka kwenye Jumuiya wa Waislamu wa Afrika ya Mashariki, ilitoka kwa Waisalmu wenyewe wa Tanganyika na siyo toka serikalini.

Nzowa amesema kwamba kabla ya Kikao cha waislamu toka nchi nzima ya Tanganyika kilichofanyika kwenye chuo cha Mkwawa mjini Iringa mwaka 1963. waislamu walishaonesha kutokuwa na imani na jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa na kiongozi wa Jumuia ya waisimailia duniani, Aga Khan.

Hoja ya Nzowa inawezekana likawa ni pigo kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwa wanasema kwamba BAKWATA ilianzishwa na Nyerere kama njia yake ya kuwahujumu waislamu wa nchi hii.

Nakala kwa:

Mohamed Said
FaizaFoxy
Ushalishwa matango pori,
 
Rubawa yote hayo hayatokani na utashi wangu kwenye kuuliza maswali bali ni kutokana na majibu ya Mzee Mohamed kutokana na Makala ya Gazeti la Mwananchi iliyomnukuu Omary Nzowa. Kama si makala ya Nzowa mimi na Mzee Mohamed tusingekuwa tunajadiliana.

Sasa maswali si yangu bali ni uchokonozi ili tujue msimamo wake kuhusu hoja za Nzowa. Kwenye kitabu haikuandikwa kwamba Serikali haihusiki na kuanzishwa kwa BAKWATA. Kwa ivo hicho kitabu si rejea nzuri kwa mjadala huu.
 
Mwandishi wa kitabu kama majibu yamo kwenye Kitabu alichoandika si ayaweke hapa na kunukuu kurasa ama aya ya kitabu!!
Allen,
Si rahisi kama unavyodhani kukuwekea hapa majibu kutoka kitabu
ambacho kina kurasa 416.

Ikiwa wewe kwa hakika unataka kujua ukweli wa historia hii lazima
usome kitabu.

Bahati mbaya mimi ndiye mwandishi na hata nikukueleza umuhimu
wa kazi hii itakuwa mimi najipigia zumari.

Lakini kaa ukijua kuwa kitabu hiki kimebadili historia nzima ya uhuru
wa Tanganyika na yatokanayo.
 
Kwa uhakika tarehe 24 October, 1968 ndipo Adam Nasibu katibu wa EAMWS Bukoba alitokea katika magazeti akiwashambulia
viongozi wa EAMWS na kutangaza Bukoba kujitoa katika EAMWS.
Hii hoja hasaidii kwamba ni waislamu wenyewe ndiyo walikuwa wanaikataa EAMWS? Wewe unazunguka dunia nzima unafadhiliwa na nani?
 
Mnakasha huu na Mzee Mohamed unatokana na makala ya Gazeti la Mwananchi iliyomnukuu mmojawapo wa wadhamini wa BAKWATA, Omary Nzowa.

Hayo ya kitabu ni safari ndefu sana ya mzunguko!!
Allen,
Imenichukua mimi zaidi ya miaka 10 kukamilisha hiki kitabu.
Wakati ule naandika kwa mkono oomputer zilikuwa bado.

Elimu kuipata unahitaji kupinda mgongo.
Ikiwa unataka kuijua historia hii huna budi kukisoma kitabu.
 
Allen,
Si rahisi kama unavyodhani kukuwekea hapa majibu kutoka kitabu
ambacho kina kurasa 416.

Ikiwa wewe kwa hakika unataka kujua ukweli wa historia hii lazima
usome kitabu.

Bahati mbaya mimi ndiye mwandishi na hata nikukueleza umuhimu
wa kazi hii itakuwa mimi najipigia zumari.

Lakini kaa ukijua kuwa kitabu hiki kimebadili historia nzima ya uhuru
wa Tanganyika na yatokanayo.
Mzee wangu MS Lets assume haya yaliyotokea ni kweli.Lets assume waislamu walinyanganywa mali nyingi kuliko wakristu,lets assume waislamu wamekandamizwa sana na Mwl.Nyerere.Position yako kuhusu marais Mwinyi na Kikwete na miundo mbinu ya kitaasisi ya waislamu ikoje?Nao walibanwa na mfumo Kristu?kwa nini hawakuuondoa kwa maslahi mapana ya dini ya Allah?Way forward yetu kama waislamu ni nini?Je Bakwata ni taasisi yenye mikakati ya kuwakomboa waislamu kiuchumi(Mind you 97%ya matajiri Tanzania ni waislamu) Lakini pia hizi taasisi za kiislam zilizoanzishwa ili kutetea maslahi halisi ya waislamu kijamii na kiuchumi zinakidhi matakwa,au nazo zimebanwa na serikali?Unapendekeza nini kifanyike maalim?Hatuwezi kuwa victims wa historia there has to be a way out?Do you agree with me that an enemy of islam is a fellow muslim? Napokea maoni yako nikiassume kuwa waislamu wameonewa na kukandamizwa na kunyanyaswa muno na utawala wa Nyerere.Naomba recommendations zako for a prosperous muslim community in Tz,nn Kifanyike?Je do you have enough capacity at your leaders'disposal to achieve the goals you desire under the so called mfumo Kristu?Wewe ni msomi naomba uchambuzi!
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Mzee wangu MS Lets assume haya yaliyotokea ni kweli.Lets assume waislamu walinyanganywa mali nyingi kuliko wakristu,lets assume waislamu wamekandamizwa sana na Mwl.Nyerere.Position yako kuhusu marais Mwinyi na Kikwete na miundo mbinu ya kitaasisi ya waislamu ikoje?Nao walibanwa na mfumo Kristu?kwa nini hawakuuondoa kwa maslahi mapana ya dini ya Allah?Way forward yetu kama waislamu ni nini?Je Bakwata ni taasisi yenye mikakati ya kuwakomboa waislamu kiuchumi(Mind you 97%ya matajiri Tanzania ni waislamu) Lakini pia hizi taasisi za kiislam zilizoanzishwa ili kutetea maslahi halisi ya N kijamii na kiuchumi zinakidhi matakwa,au nazo zimebanwa na serikali?Unapendekeza nini kifanyike maalim?Hatuwezi kuwa victims wa historia there has to be a way out?Do you agree with me that an enemy of muslims is a fellow muslim? Napokea maoni yako nikiassume kuwa waislamu wameonewa na kukandamizwa na kunyanyaswa muno na utawala wa Nyerere.Naomba recommendations zako for a prosperous muslim community in Tz,nn Kifanyike?Je do you have enough capacity at your leaders'disposal to achieve the goals you desire under the so called mfumo Kristu?Wewe ni msomi naomba uchambuzi!
Nan...
Mada iliyopo mezani ni historia ya BAKWATA.
Hii mada ilifungulie uzi mpya.
 
Nan...
Mada iliyopo mezani ni historia ya BAKWATA.
Hii mada ilifungulie uzi mpya.
Kwa heshima na taadhima nakuomba sana kwa faida yangu na wanabodi wengine kwa ajili ya ustawi mpana wa taifa letu (Tanzania ndiyo nchi pekee duniani yenye ratio inayokaribiana kati ya wakristu na waislamu na coexistance yetu katika level ya mtaa ni very impressive kwa maana ya kuwa tumeoleana na koo zetu regardless ya religious orientation ziko imara mno)
Tukiliacha hili liende bila ya kuzingatia ukweli kwamba history intels the past present and the future tutakuwa hatukitendei haki kizazi kilichopita,kilichopo na kijacho.
Nakuomba sana maalim!
 
Sheikh MS hiyo taasisi kufanya mengi sio justification ya kuwa wengi waliridhika nayo au ilikuwa haipingwi. Na ukweli huu ndio ulio sababisha kutokea BAKWATA. Na BAKWATA ilipatikanaje ni suala jengine kabisa. Lakini serikali makini yeyote isingepuuzia hitaji la walio wengi.

Nnyindo...
Kwa miaka EAMWS chini ya Aga Khan ilikuwapo na ilifanya mengi katika
maendeleo ya Waislam wala hapakuwa na tatizo.

Tatizo lilikuja mwaka wa 1968 pale EAMWS ilipotaka kujenga Chuo Kikuu.
Sivalon (1992) kaeleza yote kwa nini ilikuwa lazima hili lizuiliwe.

Unaweza pia kumsoma P van Bergen (1981) na Njozi (2000).
Kitabu cha Njozi kikapigwa marufuku.

Wizara ya Elimu Tanzania ina historia ya pekee,
Nimeeleza yaliyoko katika idara ile katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Ndiyo maana mjadal huu wahusika wanaukwepa ingawa Waislam mara
kadhaa wamekuwa wakilalamika.

Hofu ni kuwa ukweli utafahamika.
 
Iko sheria inayokataza vitabu visiongezewe chumvi? Na kama mwandishi wake ni mhafisina wa jambo analo liandika.

Uhuru wa Tanganyika ulidaiwa na Waislam!!? Unatakutuambia hiyo miaka ya 1960 kulikuwa hamna Muislam wa kwenda umoja wa mataifa mpaka wakaamua kumtuma Nyerere Mkatoliki? Acheni uongo maana sera za ni wadini yetu hazikuanza leo.

Kwanza kbs nakushauri tafuta hiki kitabu ukisome nafikiria itakusaidia kupata baadhi ya majibu kuliko kumsumbua mzee wetu Mohamed Said...View attachment 972514
 
Back
Top Bottom