BAKWATA yamsafisha Mwalimu Julius Nyerere

BAKWATA yamsafisha Mwalimu Julius Nyerere

Mimi kwa upande wangu nipo huru kifkra.

Najua kabisa kuna Waislam wasioitaka Bakwata lakini vilevile kuna taasisi nyingi tu za Waislam. Nachoshangaa sioni kama kuna taasisi kati ya hizo yenye kuwavutia Waislam wengi Kitaifa.

Lakini pili, kama ni kweli kuwa Waislam wameipuuza Bakwata iweje wawe na viongozi mpaka ngazi za misikiti na kuwa na halmashauri zao. Si wangejitenga nao tu. Mathalani tunajua Serikali hutoa mapumziko nyakati za sikukuu za Kiislam hasa mwongozo unapotolewa na Bakwata na vilevile wapo waumini wengine huamua kufuata muongozo wa kuswali (tafsiri ya mwandamo wa mwezi hasa Idd) tofauti na mwongozo wa Bakwata.

Ajabu ni kuwa wapo maelfu ya Waislam Nchi nzima hufuata muongozo wa Bakwata (rejea baraza la Idd).

Na hili nimeliona hata kama sikukuu itaangukia siku za Jmosi na Jpili na muongozo ukawa ni sherehe Jumapili Wapo Waislam kwa maelfu watafuata muongozo wa Bakwata.

Nafikiri Mzee MS tusi-underestimate nguvu ya Bakwata kama ambavyo unashawishi iwe hivyo.

Plato...
BAKWATA hawana watu katika umma wa Waislam wala hawana hao watu
unaosema katika misikiti ila ndani ya misikiti yao ambayo haijai mkononi.

Waislam na taasisi huru za Waislam nje ya BAKWATA ni nyingi sana na ndiyo
zinazofanya mengi kwa maslahi ya Uislam.

Kuswali Eid kwa mwandamo wa mwezi wa kimataifa au kuswali kinyume cha
hivyo wala si suala la BAKWATA bali la waumii wenyewe walivyopokea.

Wengi si BAKWATA lakini wanaswali Eid kwa kuona mwezi katika matlai zao.
Hivyo basi Waislam kwa kufanya hivyo si kuwa wanafuata BAKWATA.

Mimi si mtu wa chembelecho ku-''underestimate,'' BAKWATA.

Naijua vizuri sana na nimewataja katika ''paper,'' na makala nyingi nilizopata
kuandika .

Hata ile ''funfare,'' iliyoshuhudiwa katika sherehe za miaka 50 ya BAKWATA
yale si wao.

Bila ya msaada wa serikali BAKWATA ingeshakufa miaka mingi sana.
 
Weka ushahidi anuai.hizi zinabaki porojo za vijiweni km za mudi wa saigon.
Lukubuzo,
Tuepuke uhuni na fedhuli ili tuwe na mjadala wa kupendeza.
BAKWATA ilienezwa katika majimbo ya Tanganyika kwa rushwa.

Director wa Criminal Investigation wa wakati ule alipita katika
majimbo akiwaendea baadhi ya masheikh kuwataka kuunga mkono
BAKWATA kwa kishawishi cha hongo ya shs: 40,000.00.

Lukubuzo,
Sikutaka niseme haya lakini umenilazimisha na ndiyo maana sikuweka
jina wala picha ya mtoa rushwa.

Kwangu mimi hili nifanyalo hapa ni kumtumikia Allah yaani ni ibada na
ndiyo maana ingawa umenikejeli na kuja kwa ufedhuli nimestahamili na
nimerejea kwako na majibu.

Mimi si mtu wa porojo.

Saigon ni barza yangu toka utotoni na kwangu mimi hii ni sifa kuwa mimi
ni mwanamji ambao najivunia sana.
 
Hakika ule ni uonevu lakini nashangaa watetezi wa haki za binaadam wote kimyaaaaaaa.

Maana hata kama wanahatia si kesi iendeshwe wahukumiwe, uchunguzi gani miaka yote hii?
Ulisikia maneno ya MUFTI Zubery?, ili waislamu kupata haki nchi hii ni lazima BAKWATA ivunjwe, na ili bakwatwa ivunjwe ni lazima ccm ing'oke, kuliulizwa swali bungeni kwa nini wakristo kila taasisi inajitegemea lakini kwetu taasisi mpaka ipate ridhaa ya bakwata, halikujibiwa,

Mpaka cheti cha ndoa wenzetu kila taasisi inajitegemea lakini kwetu cheti lazima kitoke bakwata,
Lakini haya yote yanasababishwa na nyie wafia chama
 
Hatuji huko ng'oo. Wachukuweni misukule wenzenu.
 
Hahahaaa!!

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania... The National Muslim Council of Tanzania

Baraza la Wakristo Tanzania... The Christian Council of Tanzania (CCT).

Nyerere was very smart! Ili isionekane yeye ndie engineer wa hayo mabaraza, lile la Waislamu likabaki likiitwa kwa Kiswahili, yaani Baraza na lile la Kikristo likabaki kuwa Council... utampatia wapi; hata majina hawafanani!

Na wote hawa, tangu zama hizo wamekuwa wakinywa chai pamoja na Ikulu! Na ni nadra sana haat kwa CCT kukuta wakitoa matamako makali dhidi ay serikali! Siku kwa mfano, Baraza la Maaskofu wakitoa waraka mkali dhidi dhidi ya serikali, usishangae kukuta CCT wanakuja kuukanusha!!!

Hao wote, walifungishwa ndoa ya mkeka na serikali ya CCM na mfungishaji ndoa alikuwa Baba wa Taifa!!
Kuna tofauti kati ya baraza na council?
 
Proved,
EAMWS ulikuwa umoja wa Waislam wote wa Afrika ya Mashariki.
Umoja huu ulipopigwa marufuku Tanzani ikawa tena Afrika ya
Mashariki haipo.
Huko kwingine kwa maana ya Kenya na Uganda ambako hawakuzuiliwa hatuoni vyuo vikuu na mashule.Unaweza ukatufafanulia?Jambo hili linafikirisha akili yangu kwa sana tu.Kwa nini Bakwata hawakuendelea na idara ya elimu na kuyafanya yanayofanywa na TEC pamoja na CCT?
 
Allen,
Kwani taaasisi ikiwa imeanzishwa na Aga Khan ndiyo ipigwe marufuku?

Tuna taasisi nyingi nchini za Kikristo zilizoanzishwa na Wazungu kama
hizo hapo chini:

White Fathers (Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba);
Holy Ghost Fathers (Morogoro na Kilimanjaro); Benedictine Fathers
(Peramiho na Ndanda); Capuchin Fathers (Dar es Salaam); Consolata
Fathers (Iringa na Meru); Passionist Fathers (Dodoma); Pallotine Fathers
(Mbulu); Maryknoll Fathers (Musoma); na Rosmillian Fathers (Iringa).

Mbona haya makanisa ya Wazungu hayakubughudhiwa na haya ni kutoka
mataifa mengi ya Ulaya?

Shida iwe Aga Khan peke yake?.

Sasa miaka 50 Waislam wameuliza swali hili na wahusika hawajatoa jibu
mnakuja nyie akina Allen kwetu sisi Waislam na maswali ya vichekesho.
ati mnataka kujua EAMWS ya Kenya na Uganda.

Mambo kama haya ndiyo maana kwa miaka 50 Waislam tumeipuuza
BAKWATA na hao BAKWATA wanajua kama tumewapuuza.

Ndiyo sababu siku zote utawasikia viongozi wa BAKWATA wanajinasibisha
na Waislam.

Hujapata kusikia Waislam wanajinasibisha na BAKWATA.
Sasa hapa lazima hoja ya mzee Nzowa iwe na mashiko.Inawezekana kuna ukweli kuwa waislamu wazalendo hawakuridhishwa na mwenendo wa taasisi hii ya Agha Khan kwa maana ya kwamba hawakuwa na maamuzi na vilevile ushirikishwaji haukuwepo kabisa(Ukizingatia ni katika kipindi hiki ambako mkoloni tulishamuondoa kwa maana ya uhuru binafsi,Unafikiri waislamu wazalendo hawakutaka kuwa huru na magabachori?) na hili linadhihirika hata leo ukifuatilia utengamano wa waismailia na wazalendo wetu hawa.
Halafu nakuomba pia ujitahidi sana kujifunza kuhusu namna kanisa katoliki linavyojiendesha kusudi usiwapotoshe ndugu walio humu.Chombo kikubwa kiutendaji ndani ya kanisa katoliki ni baraza la maaskofu tanzania likifuatiwa na majimbo,parokia,baraza la walei,jumuiya na jumuiya ndogondogo.Hizo taasisi ulizozitaja zinawajibika moja kwa moja kwa baraza la maaskofu na kwa maaskofu wa majimbo husika zinakopatikana.Hao ni either wamisionari,mapadre au watawa ambao kwao huongozwa kiroho kwa kufuata kanuni za waanzilishi wa mashirika husika.Kazi za elimu,afya na maji pamoja na huduma nyinginezo ni missions za Yesu ambazo wao huzitekeleza kwa ajili ya kuwajenga waumini wao kiroho na kimwili.
Hakuna tofauti kati ya shula ya maimamu na holy ghost fathers kwa hiyo naamini kuwa hauko informed vizuri kuhusu mashirika ya kiroho ya either wamisionari au watawa wa kikatoliki.Hawa wote uahidi utii kwa mamlaka za kiaskofu kwa majimbo husika na ziko chini ya baraza la maaskofu.
 
Sasa hapa lazima hoja ya mzee Nzowa iwe na mashiko.Inawezekana kuna ukweli kuwa waislamu wazalendo hawakuridhishwa na mwenendo wa taasisi hii ya Agha Khan kwa maana ya kwamba hawakuwa na maamuzi na vilevile ushirikishwaji haukuwepo kabisa na hili linadhihirika hata leo ukifuatilia utengamano wa waismailia na wazalendo wetu hawa.
Halafu nakuomba pia ujitahidi sana kujifunza kuhusu namna kanisa katoliki linavyojiendesha kusudi usiwapotoshe ndugu walio humu.Chombo kikubwa kiutendaji ndani ya kanisa katoliki ni baraza la maaskofu tanzania likifuatiwa na majimbo,parokia,baraza la walei,jumuiya na jumuiya ndogondogo.Hizo taasisi ulizozitaja zinawajibika moja kwa moja kwa baraza la maaskofu na kwa maaskofu wa majimbo husika zinakopatikana.Hao ni either wamisionari,mapadre au watawa ambao kwao huongozwa kiroho kwa kufuata kanuni za waanzilishi wa mashirika husika.Kazi za elimu,afya na maji pamoja na huduma nyinginezo ni missions za Yesu ambazo wao huzitekeleza kwa ajili ya kuwajenga waumini wao kiroho na kimwili.
Hakuna tofauti kati ya shula ya maimamu na holy ghost fathers kwa hiyo naamini kuwa hauko informed vizuri kuhusu mashirika ya kiroho ya either wamisionari au watawa wa kikatoliki.Hawa wote uhaidi utii kwa mamlaka za kiaskofu kwa majimbo husika na ziko chini ya baraza la maaskofu.
Nanta...
Hapa tunaweza tukazungushana sana.
Waislam tunajua kilichotokea.

Wewe hujui yaliyotufika uko katika dhana.

Mgogoro wa EAMWS ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya kitabu cha
Maisha ya Abdul Sykes:

1545227646439.png

Sehemu hii ya tatu nimeeleza changamoto zilizokuja na uhuru kwa upande
wa Waislam.

Historia yote ya kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA imeelezwa
kwa kirefu na ndiyo sehemu ambayo imegusa wasomaji wengi sana.

Badala ya wewe kuwa unaandika kitu usichokijua vizuri bora ungesoma historia
hii na uone ushahidi nilioweka kwa yake ambayo nimeandika.

Hapo labda utaweza kujadili na mimi vinginevyo tutazungushana tu hapa.

Kusudi ya kitabu hiki ilikuwa kusahihisha historia ya Chama Cha TANU iliyoandikwa
na Chuo Cha CCM Kivukoni kitabu ambacho hakikueleza historia ya kupigania
uhuru kwa usahihi.

1545229347732.png

Hili likiwa moja ya changamoto zilizokuja na uhuru wa Tanganyika.
Mengi ambayo naandika hapa JF yanatokana na utafiti huu.
 
Na bado watamsafisha kuwa nia yake ya kutaifisha shule ni ili kuwaepusha ba ujinga. Ingawa aliwakosesha fursa ya kuijua kweli na kweli kuwaweka huru kwelikweli.
 
Nanta...
Hapa tunaweza tukazungushana sana.
Waislam tunajua kilichotokea.

Wewe hujui yaliyotufika uko katika dhana.

Mgogoro wa EAMWS ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya kitabu cha
Maisha ya Abdul Sykes:

View attachment 972304

Sehemu hii ya tatu nimeeleza changamoto zilizokuja na uhuru kwa upande
wa Waislam.

Historia yote ya kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA imeelezwa
kwa kirefu na ndiyo sehemu ambayo imegusa wasomaji wengi sana.

Badala ya wewe kuwa unaandika kitu usichokijua vizuri bora ungesoma historia
hii na uone ushahidi nilioweka kwa yake ambayo nimeandika.

Hapo labda utaweza kujadili na mimi vinginevyo tutazungushana tu hapa.

Kusudi ya kitabu hiki ilikuwa kusahihisha historia ya Chama Cha TANU iliyoandikwa
na Chuo Cha CCM Kivukoni kitabu ambacho hakikueleza historia ya kupigania
uhuru kwa usahihi.

View attachment 972335

Hili likiwa moja ya changamoto zilizokuja na uhuru wa Tanganyika.
Mengi ambayo naandika hapa JF yanatokana na utafiti huu.
Nakushukuru mzee MS kwa kunipa challenge ya kufanya utafiti zaidi ili kufahamu ukweli.
Lakini ukilinganisha maelezo yako na yale ya mzee Nzowa ukweli unaegemea zaidi kwa mzee Nzowa.
Kwa mfano sustainability ya jumuiya ya waislamu ya Agha Khan inajibiwa vizuri na kiu ya wazalendo kutaka kujitawala na wala hilo halina shaka.
Historia kamili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
Pili niliwahi kuandika humu kuhusu sheria iliyoyatunga mabaraza yanayosimamia maslahi ya kiimani ya watanzania kwa maana ya BAKWATA,CCT na TEC.kwamba kwa nini bakwata kimaendeleo iko nyuma sana ukilinganisha na haya mabaraza mengine?mjumbe mmoja alifikia hatua ya kudiriki kusema kuwa by 2015 Bakwata hawakuwa hata na strategic plan.Ningependa unifafanulie kuhusu backwardness ya Bakwata ukilinganisha na mabaraza menzake kiuchumi na kijamii(Nisingependa tujikite kiimani)
 
Sasa hapa lazima hoja ya mzee Nzowa iwe na mashiko.Inawezekana kuna ukweli kuwa waislamu wazalendo hawakuridhishwa na mwenendo wa taasisi hii ya Agha Khan kwa maana ya kwamba hawakuwa na maamuzi na vilevile ushirikishwaji haukuwepo kabisa(Ukizingatia ni katika kipindi hiki ambako mkoloni tulishamuondoa kwa maana ya uhuru binafsi,Unafikiri waislamu wazalendo hawakutaka kuwa huru na magabachori?) na hili linadhihirika hata leo ukifuatilia utengamano wa waismailia na wazalendo wetu hawa.
Halafu nakuomba pia ujitahidi sana kujifunza kuhusu namna kanisa katoliki linavyojiendesha kusudi usiwapotoshe ndugu walio humu.Chombo kikubwa kiutendaji ndani ya kanisa katoliki ni baraza la maaskofu tanzania likifuatiwa na majimbo,parokia,baraza la walei,jumuiya na jumuiya ndogondogo.Hizo taasisi ulizozitaja zinawajibika moja kwa moja kwa baraza la maaskofu na kwa maaskofu wa majimbo husika zinakopatikana.Hao ni either wamisionari,mapadre au watawa ambao kwao huongozwa kiroho kwa kufuata kanuni za waanzilishi wa mashirika husika.Kazi za elimu,afya na maji pamoja na huduma nyinginezo ni missions za Yesu ambazo wao huzitekeleza kwa ajili ya kuwajenga waumini wao kiroho na kimwili.
Hakuna tofauti kati ya shula ya maimamu na holy ghost fathers kwa hiyo naamini kuwa hauko informed vizuri kuhusu mashirika ya kiroho ya either wamisionari au watawa wa kikatoliki.Hawa wote uahidi utii kwa mamlaka za kiaskofu kwa majimbo husika na ziko chini ya baraza la maaskofu.

Nan...
Mgogoro wa EAMWS ni sehemu ya tatu na ya mwisho ya kitabu cha
Maisha ya Abdul Sykes:

1545227646439-png.972304

Sehemu hii ya tatu nimeeleza changamoto zilizokuja na uhuru kwa upande
wa Waislam.

Historia yote ya kuvunjwa kwa EAMWS na kuundwa kwa BAKWATA imeelezwa
kwa kirefu na ndiyo sehemu ambayo imegusa wasomaji wengi sana.

Badala ya wewe kuwa unaandika kitu usichokijua vizuri bora ungesoma historia
hii na uone ushahidi nilioweka kwa yake ambayo nimeandika.

Hapo labda utaweza kujadili na mimi vinginevyo tutazungushana tu hapa.

Kusudi ya kitabu hiki ilikuwa kusahihisha historia ya Chama Cha TANU iliyoandikwa
na Chuo Cha CCM Kivukoni kitabu ambacho hakikueleza historia ya kupigania
uhuru kwa usahihi.
 
Ukweli hata bila utafiti wa kina Waislam wa Tanganyika ambao wengi ni dhehebu la Sunni kamwe wasingeweza kuongozwa na taasisi iliyoanzishwa na Agakhan wa Ismailia, kamwe. Hizo nyingine ni hadithi za kutafutia ugali. Ukweli mchungu ndio huo.

Sasa wakienda kuomba nani awasaidie kutimiza lengo lao hilo ndio hizi Blabla nyingi utasikikia. Mara hivi mara hivi yote hiyo ni kutafuta kupotosha ukweli.

Nakushukuru mzee MS kwa kunipa challenge ya kufanya utafiti zaidi ili kufahamu ukweli.
Lakini ukilinganisha maelezo yako na yale ya mzee Nzowa ukweli unaegemea zaidi kwa mzee Nzowa.
Kwa mfano sustainability ya jumuiya ya waislamu ya Agha Khan inajibiwa vizuri na kiu ya wazalendo kutaka kujitawala na wala hilo halina shaka.
Historia kamili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
Pili niliwahi kuandika humu kuhusu sheria iliyoyatunga mabaraza yanayosimamia maslahi ya kiimani ya watanzania kwa maana ya BAKWATA,CCT na TEC.kwamba kwa nini bakwata kimaendeleo iko nyuma sana ukilinganisha na haya mabaraza mengine?mjumbe mmoja alifikia hatua ya kudiriki kusema kuwa by 2015 Bakwata hawakuwa hata na strategic plan.Ningependa unifafanulie kuhusu backwardness ya Bakwata ukilinganisha na mabaraza menzake kiuchumi na kijamii(Nisingependa tujikite kiimani)
 
Huko kwingine kwa maana ya Kenya na Uganda ambako hawakuzuiliwa hatuoni vyuo vikuu na mashule.Unaweza ukatufafanulia?Jambo hili linafikirisha akili yangu kwa sana tu.Kwa nini Bakwata hawakuendelea na idara ya elimu na kuyafanya yanayofanywa na TEC pamoja na CCT?
Nan...
Mazingira ya Kenya tofauti sana na yale ya Tanganyika.

Kenya Wakikuyu ndiyo walisimama kwa silaha kupambana na ukoloni
na ndiyo walioongoza vita vya uhuru.

Tanganyika vita vya Maji Maji viliongozwa na Waislam na harakati za
kudai uhuru ziliongozwa na Waislam pia.

Lakini kubwa Kenya Waislam ni minority wala na hivyo hata mchango
wao katika kupigania uhuru ulkwenda sawa na idadi yao.

Unataka nikueleze hapa mchango wa Waislam katika kupigania uhuru
wa Tanganyika au tayari unafahamika kwa urefu na mapana yake?

1545231102212.png

Nan...
Unauliza kwa nini BAKWATA hawakufanya yale wanayofanywa na TEC na CCT?

BAKWATA imeundwa ili kuzuia EAMWS isijenge Chuo Kikuu ilikuwa miezi michache
baada ya jiwe la msingi la chuo kuwekwa ndipo EAMWS ikavunjwa kwa amri ya rais.

Hii ndiyo hatari ya kujadili kitu usichokijua.
Soma kitabu cha Abdul Sykes yote haya nimeeleza.
 
Ukweli hata bila utafiti wa kiba Wauslam wa Tanganyika ambao wengi ni dhehebu la Sunni kamwe wasingeza kuongozwa na taasisi iliyoanzishwa na Agakhan wa Ismailia, kamwe. Hizo nyingine ni hadithi za kutafutia ugali. Ukweli mchungu ndio huo.
Nnyindo...
Kwa miaka EAMWS chini ya Aga Khan ilikuwapo na ilifanya mengi katika
maendeleo ya Waislam wala hapakuwa na tatizo.

Tatizo lilikuja mwaka wa 1968 pale EAMWS ilipotaka kujenga Chuo Kikuu.
Sivalon (1992) kaeleza yote kwa nini ilikuwa lazima hili lizuiliwe.

Unaweza pia kumsoma P van Bergen (1981) na Njozi (2000).
Kitabu cha Njozi kikapigwa marufuku.

Wizara ya Elimu Tanzania ina historia ya pekee,
Nimeeleza yaliyoko katika idara ile katika kitabu cha Abdul Sykes (1998).

Ndiyo maana mjadal huu wahusika wanaukwepa ingawa Waislam mara
kadhaa wamekuwa wakilalamika.

Hofu ni kuwa ukweli utafahamika.
 
Wakati baadhi ya watanzania wakisubiri taarifa kutoka kwenye kile kikao cha wafanya mazingaombwe maarufu wa Tanzania, leo Gazeti la Mwananchi limechapisha mahojiano kati yake na Mdhamini wa BAKWATA, Omary Nzowa.

Katika makala inayoelezea Historia ya kuanzishwa kwa Baraza Kuu La Waislamu Tanzania (BAKWATA) Omary Nzowa amekanusha habari kwamba Baraza hilo lilianzishwa kwa shinikizo la Serikali zama za Mwalimu akiwa ndiye rais wa Tanzania.

Omary Nzowa amesema hoja ya kuanzishwa kwa BAKWATA na kutoka kwenye Jumuiya wa Waislamu wa Afrika ya Mashariki, ilitoka kwa Waisalmu wenyewe wa Tanganyika na siyo toka serikalini.

Nzowa amesema kwamba kabla ya Kikao cha waislamu toka nchi nzima ya Tanganyika kilichofanyika kwenye chuo cha Mkwawa mjini Iringa mwaka 1963. waislamu walishaonesha kutokuwa na imani na jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa na kiongozi wa Jumuia ya waisimailia duniani, Aga Khan.

Hoja ya Nzowa inawezekana likawa ni pigo kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwa wanasema kwamba BAKWATA ilianzishwa na Nyerere kama njia yake ya kuwahujumu waislamu wa nchi hii.

Nakala kwa:

Mohamed Said
FaizaFoxy
Ngoja nimsikie Mohamed Said
 
Back
Top Bottom