Nan...
Mazingira ya Kenya tofauti sana na yale ya Tanganyika.
Kenya Wakikuyu ndiyo walisimama kwa silaha kupambana na ukoloni
na ndiyo walioongoza vita vya uhuru.
Tanganyika vita vya Maji Maji viliongozwa na Waislam na harakati za
kudai uhuru ziliongozwa na Waislam pia.
Lakini kubwa Kenya Waislam ni minority wala na hivyo hata mchango
wao katika kupigania uhuru ulkwenda sawa na idadi yao.
Unataka nikueleze hapa mchango wa Waislam katika kupigania uhuru
wa Tanganyika au tayari unafahamika kwa urefu na mapana yake?
View attachment 972399
Nan...
Unauliza kwa nini BAKWATA hawakufanya yale wanayofanywa na TEC na CCT?
BAKWATA imeundwa ili kuzuia EAMWS isijenge Chuo Kikuu ilikuwa miezi michache
baada ya jiwe la msingi la chuo kuwekwa ndipo EAMWS ikavunjwa kwa amri ya rais.
Hii ndiyo hatari ya kujadili kitu usichokijua.
Soma kitabu cha
Abdul Sykes yote haya nimeeleza.