Nnyi...
Unafananisha picha ya
Bi Tatu bint Mzee ya mwaka wa 1955 wakati
wamesimama na
Mwalimu Nyerere Uwanja wa Ndege kumsindikiza
safari ya kwanza UNO picha hii unaipa hadhi sawa na picha ya uhuru
ushapatikana ya
Mama Maria na mke wa Gavana?
Akili yako inakutuma kuamini kuwa picha hizi mbili zinaeleza taswira
moja?
Labda kwa kuwa hujui historia ya TANU.
Hawa akina mama katika picha
Bi. Tatu bint Mzee na
Mama Sakina
ndiyo ni mashoga wa
Mama Maria Nyerere na ndiyo waliompokea
yeye na
Mwalimu Nyerere mjini Dar es Salaam.
Ungetumia akili kidogo tungejiuliza vipi
Baba wa Taifa kasindikizwa
na akina mama hawa?
Hawa akina mama ni nani?
Hawa akina mama walifahamiana vipi na
Baba wa Taifa?
Nakudokeza kidogo tu.
Tatu bint Mzee alikuwa katika Halmashauri Kuu ya TANU 1955.
Una taarifa yoyote ya
Mama Maria Nyerere kualikwa na
Mrs. Turnbull
nyumbani kwake Government House 1955?
Nitakudokeza tena kitu kingine.
Mama Maria nyumba yake kuu ilikuwa nyumbani kwa
Abdul Sykes Mtaa
wa Stanley na Sikukuu na nyumba yake nyingine ilikuwa kwa
Bi. Chiku
bint Said Kisusa Mtaa wa Mchikichi na New Street.
Hawa akina mama wote walikuwa ndiyo wanachama wa mwanzo wa TANU
na ndiyo maana ukaona katika hiyo picha wako ubavuni kwa
Baba wa Taifa
wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Historia ya Malkia wa Waswezi ni muhimu ihifadhiwe kwa ajili ya kuwaenzi
mashujaa wetu.
Kwa kuwa umegusia njama ya Nyerere kulishwa sumu niruhusu nikupe kisa
kilicholeta tafaruku kubwa nyumbani kwa Abdul Sykes siku Nyerere alipougua
ghafla baada ya kula chakula cha mchana hapo katika ''retreat,'' kwani hiyo
nyumba ndiyo ilikuwa ngome ya mipango yote ya TANU:
Mohamed Said: KUTOKA JF: TAHARUKI - NYERERE KALISHWA SUMU 1950s
''Siku za mwanzo za TANU viongozi wake walikuwa wakiwa na jambo zito
la kujadili walikuwa wakikutana nyumbani kwa
Abdul Sykes Mtaa wa
Stanley na Sikukuu.
Walikuwa wakimaliza shughuli basi inakuwa chakula na vinywaji kujipongeza.
Siku hiyo baada ya kikao wakala chakula cha mchana.
Baada ya kula ghafla
Nyerere akaanza kulalamika kuwa tumbo linamkata.
Nyerere akawa anajipindua huku na huku kwa maumivu.
Siku zote TANU walikuwa wakiishi chini ya hofu ya
Nyerere kudhuriwa na
maadui wa TANU lakini katika chakula kile cha nyumbani kwake hapakuwa
na hofu kwani chakula chake kilikuwa kinatoka Kariakoo na kwa watu maalum
ambao Market Master,
Abdul Sykes akiwafahamu na
Mzee Mshume na ndiye
akikinunua, mpelekaji wa chakula hicho kwa
Mama Maria alikuwa dereva wa
TANU,
Said Kamtawa maarufu kwa jina
Said TANU.
Nyerere kalala kwenye kochi anaugulia na taharuki ikazuka na minong'ono
haikuweza kukwepeka.
Nyerere kalishwa sumu!
Sumu
Nyerere alishwe nyumbani kwa
Abdul Sykes?
Uani jikoni walikuwa mama yake
Nyerere Bi. Mgaya, Mama Maria, mama
yake Abdul Sykes Bi. Mruguru bint Mussa, mkewe
Abdul Sykes, Mama
Daisy.
Bi. Mgaya hakuweza kustahamili alipoona wanaume ingia toka kule ndani.
Aliposikia kuwa
Nyerere anaumwa baada ya kula chakula kitu cha kwanza
kilichomjia ni kuwa mwanae kalishwa sumu akawa sasa mikono kichwani
analia na kutembea ua mzima.
Bi. Mgaya anasema Kizanaki na anachanganya na Kiswahili.
Ikawa patashika kumtuliza.
Wote waliokula chakula kile walikuwa salama na hawa ni watu waliokuwa
wakijuana vizuri na wakiaminiana mwisho wa imani.
Nani anaweza kupenya nyumbani kwa
Abdul akampa sumu
Nyerere?
Nani?
Mama Daisy ndiye alikua akinihadithia alipomaliza aliinamisha kichwa
akasema, ''Mwanangu
Mohamed,
Abdul na
Nyerere wametoka mbali
sana na walikuwa zaidi ya ndugu.''
Iko siku nitakileta hapa kisa cha sanduku la fedha la
Abdul Sykes.''