Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,453
- 34,004
Nguruvi,Mijadala kama hii tumekuwa nayo jamvini kwa muda. Kwavile si 'objective' wengi wanakaa pembeni. Hatuwezi kuchanganya kila kitu tukapata mwelekeo
Nitachangia kidogo. Allen na Nan wameuliza kwa kutumia maneno 'the way forward au the way out''
Maneno hayo yana maana na nilidhani ndiyo yangekuwa chachu katika hali ilipo
Kwa bahati mbaya sana miaka 50 ya Bakwata na 20 ya kifo cha Nyerere bado watu wapo katika 'denial state'
Kulitambua na kulikubali tatizo ni sehemu muhimu ya jawabu. Unapokana uwepo wa tatizo, huwezi kupata jibu
Uwepo wa Bakwata ''direct or indirect'' ni udhaifu wa Waislam.
Baada ya uhuru 98% ya halmashauri ya TANU ilikuwa ni Waislam. Waliotumiwa ''kuhujumu taasisi'' ni Waislam
It does not matter EAMWS ilikufaje au BAKWATA ilianzaje, the bottom line, ni matokeo ya udhaifu wa Waislam
Ni kauli isiyopendeza lakini ukitaka kupata jawabu la tatizo ni lazima uitaje na kukiri hali hiyo
Allen, ni kweli Bakwata ni 'wing' ya serikali hasa ukiangalia inavyohudumiwa kuliko organization nyingine
''Wing'' hiyo inafanya kazi kutokana na udhaifu wa Waislam wanaotumiwa na wanaounga mkono
Ni udhaifu wa waislam wa taasisi nyingine nje ya Bakwata, wanaoshindwa kutumia udhaifu wa Bakwata
Kwa ufupi, badala ya kuangalia udhaifu ndani ya jamii, kuna watu wanatafuta ''flimsy excuses'' ku justify udhaifu badala ya kutafuta jawabu sahihi la kudumu.
Moja ya sababu zinazotumiwa ni uwepo wa Nyerere! siyo udhaifu wa Waislam.
Nyerere amefariki takribani miaka 20 bado watu wanamzungumzia badala ya kuzungumzia tatizo.
Bakwata ipo miaka 50, badala ya kuiongelea watu wanaongelea Nyerere kila siku
Udhaifu huo ndio tunaouona, watu wanakwepa hoja wanahamisha magoli,hatuelewi nini kinaongelewa
Badala ya kuongelea Nyerere, watu waongelee 'the way forward au out''
Kuifanya Bakwata iwe useful au useless bila kuanglia nyuma au makando makando yasiyo na maana
1. Kusababisha uasi utakaowezesha uongozi mpya kwa masilahi ya waislam 'useful'
2. Kuunda taasisi zenye nguvu na kuifanya Bakwata iwe ''useless'' hata wanaofadhili waelewe hivyo
Msingi mkubwa wa kufanikiwa ni Waislam kukiri udhaifu ndani na miongoni mwao, na kuacha kutafuta sababu ambazo kamwe haziwezi kutoa jawabu kwa udhaifu wa wao kwa wao
Kuundwa kwa Taasisi za baraza kuu, Bkwata na taasisi nyingine kuaongeza udhaifu kwa kuwagawa Waislam badala ya kuwasadia waelewe, udhaifu ndio unawafanya watumike, watumiwe, wagawanyike, wagawanywe n.k.
Natambua kauli zangu zitaudhi baadhi ya watu, kwangu mimi ''nitakuambia ninachotaka kukuambia na si kile unachotaka kusikia'', koleo ni koleo si kijiko kikubwa. Watu warudi kutafakari waache hisia zisizo na majibu
Waislam sasa kwa miaka mingi hawashughuliki tena na BAKWATA hili
nadhani hulijui ndiyo maana umeandika hayo uliyoandika hapo juu.
''Advantage,'' kubwa niliyonayo kwenu ni kuwa kwanza mimi ni Muislam,
pili nimetafiti na kuandika mengi katika Uislam Tanzania ''paper,'' ambazo
nimezitoa katika majukwaa ya vyuo vikuu, katika makongano, mikutano na
nimefanya vipindi katika radio na TV na yote niliyosema na kuandika hivi
sasa yanatumika kama rejea katika somo hili.
Nyie wenzangu mnaandika bila ya kuwa na uelewa wa historia ya BAKWATA.
Mnaandika na kusema kwa hisia zenu tu bila kuwa na ushahidi wowote.
Hii hapo chini ni sura katika mswada, ''Christian Hegemony and the Rising of
Muslim Militancy,'' (unpublished) humo nimeeleza ''turning point,'' pale Waislam
walipoagana na BAKWATA na kuishinikiza serikali ya Rais Mwinyi iruhusu
Waislam wasajili taasisi zao huria kama wanavyofanya waumini wa dini nyingine.
Kabla ya hapo Waislam walikuwa hawawezi kujikusanya nje ya BAKWATA.
Serikali kwa shingo upande ilikubali.
Ingia hapo chini kupata historia nzima na hii ilikuwa 1992 baada ya BAKWATA
kuondolewa madarakani kwa nguvu na Waislam na serikali iliingilia kati kutaka
kuleta sulhu na BAKWATA wakakiuka makubaliano yaliyofikiwa Ikulu.
Mohamed Said: WAISLAM NA BAKWATA 1990s
Sasa kuanzia hapo Waislam kila walipo wamekuwa wakisajili taasisi zao na
kushughulikia maendeleo yao na ndiyo leo unaona Waislam wanajenga shule,
vituo vya kulea mayatima, wana magazeti, TV na wanafanya shughuli zao nyingi
kwa utulivu mkubwa.
Nini matokeo ya mabadiliko haya?
BAKWATA imekuwa kama moja ya taasisi katika taasisi za Kiislam na haina
nguvu tena ya kuwasumbua Waislam.
Lakini jambo kubwa katika juhudi hizi ni kuwa taasisi hizi zote kutaka kuishi
kwa amani na BAKWATA bila ya kusuguana kama ilivyokuwa huko nyuma.
Bahati mbaya sana ni kuwa BAKWATA wao wanataka ndiyo watawale hizi
taasisi na hili mara kwa mara limekuwa tatizo kwa Waislam kukataa kuwa chini
yao kutokana na historia ya BAKWATA kwani hawaaminiki na hakuna taasisi
yoyote inataka kuwa hata na harufu ya BAKWATA mlangoni pake.
Ndiyo maana hata siku moja hutosikia Waislam wanajinasibisha na BAKWATA
ila utasikia BAKWATA wao ndiyo wanajinasibisha na Waislam.
Huu ndiyo ukweli ambao serikali na BAKWATA hawaukubali na hawautaki.
Mimi nisingeandika lolote kuhusu BAKWATA laiti si kama hapa JF pasingewekwa
historia ya uongo ya Omary Nzowa kuhusu kuasisiwa kwa BAKWATA iliyochapwa
na gazeti moja maarufu.
Hii ndiyo sababu nimekuja hapa kueleza ukweli kuondoa dhima kwa Allah anishuhudie
kuwa ule ukweli uliosababisha EAMWS ivunjwe 1968 na BAKWATA iundwe nimeueleza.
Ukweli utabaki tu kuwa EAMWS ilikuwa inajenga Chuo Kikuu kwa ajili ya Waislam
ili na wao waelimike na washiriki katika utawala wa nchi na hii ndiyo sababu ya
kuvunjwa kwake na Waislam kuundiwa BAKWATA.
Hayo mengine si muhimu kwa hiyo nimeyaacha kama yalivyo.
