BAKWATA yamsafisha Mwalimu Julius Nyerere

BAKWATA yamsafisha Mwalimu Julius Nyerere

Good question. Ulipitwa na tamko la CCT (uliodai huwa hawatoi matamko makali dhidi ya serikali).
Waraka ambao ulikuwa ni tamko kali dhidi ya serikali ulitoka kwa Maaskofu wa RC na sio wa CCT! Ni waraka ambao hata akina Pengo, wanufaika wa mfumo wakaja kukanusha kwamba huo haukuwa waraka wa maaskofu bali uliandikwa na watu wanne tu!!!
 
Mimi nachoweza kusema ni kwamba hata humo BAKWATA kwenyewe siyo wote walio njia moja na CCM kinachotokea ni wao kupata bubujiko la furaha {hali ya furaha iliyopitiliza} kutokana na ahadi alizowaahidi mkuu jana.hili swali wangeulizwa siku kabla ya jana usitegemee jibu lingekuwa smooth kiasi hiki.

Mchana nimesoma mahali mahojiano ya Mufti na chombo kimoja cha habari akaulizwa "ninini maoni yake kuhusu mashehe walioko gerezani",aloo alijibu kama vile ndo wameshaoneka na hatia au labda ameshajua matokeo ya kesi yenyewe.
 
Mwambie akueleze na kwanini BALUKTA iliuliwa mkuu. Sikuambii chochote Bali nakupa hints ili utakapoenda kuchimbua ndo utapata majibu mengi. Hii inaitwa learning by participatory approach
Bila shaka, maana Mzee Nzowa haipiti wiki hatujaonana!!
 
Hivi kwa miaka hamsini Bakwata imefanya nini? Katika Elimu, Afya nk. Wanajivunia kitu gani? Wameshindwa kujitegemea. Wanasaidiwa na serikali, hata juzi wamesaidiwa. Ni aibu kusaidiwa na asiye muislamu katika kujenga msikiti.
 
bakwata ni moja ya tasisi za serikali kwahyo usishangae kusaidiwa mkuu!!!
 
Wakati baadhi ya watanzania wakisubiri taarifa kutoka kwenye kile kikao cha wafanya mazingaombwe maarufu wa Tanzania, leo Gazeti la Mwananchi limechapisha mahojiano kati yake na Mdhamini wa BAKWATA, Omary Nzowa.

Katika makala inayoelezea Historia ya kuanzishwa kwa Baraza Kuu La Waislamu Tanzania (BAKWATA) Omary Nzowa amekanusha habari kwamba Baraza hilo lilianzishwa kwa shinikizo la Serikali zama za Mwalimu akiwa ndiye rais wa Tanzania.

Omary Nzowa amesema hoja ya kuanzishwa kwa BAKWATA na kutoka kwenye Jumuiya wa Waislamu wa Afrika ya Mashariki, ilitoka kwa Waisalmu wenyewe wa Tanganyika na siyo toka serikalini.

Nzowa amesema kwamba kabla ya Kikao cha waislamu toka nchi nzima ya Tanganyika kilichofanyika kwenye chuo cha Mkwawa mjini Iringa mwaka 1963. waislamu walishaonesha kutokuwa na imani na jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa na kiongozi wa Jumuia ya waisimailia duniani, Aga Khan.

Hoja ya Nzowa inawezekana likawa ni pigo kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwa wanasema kwamba BAKWATA ilianzishwa na Nyerere kama njia yake ya kuwahujumu waislamu wa nchi hii.

Nakala kwa:

Mohamed Said
FaizaFoxy
Ulimuuliza Nzowa ni nani aliipiga marufuku EAMWS?
 
Ulimuuliza Nzowa ni nani aliipiga marufuku EAMWS?
Kwenye maelezo yake amesema kuwa ni Waislamu wenyewe toka nchi nzima walionesha kutokuwa na Imani na EAMWS. Ingawa ameelezea jinsi Aga Khan alivyokuwa yupo tayari kusaidia miradi mbali mbali ya maendeleo kwa waislamu.

Chanzo ni Gazeti la Mwananchi na siyo mimi!
 
Mzinifu,mlevi,Mwizi n.k shari zao ni kidogo mno kuliko shari za BAKWATA
kwasabab
Mlevi,mzinifu,mwizi, wote wanajua haya ni makosa na muda wowote wanaweza kutubia na kurejea kwa MUUMBA wao.
Lakin BAKWATA hawatobalika kwani wanajiona wao wapo sawa sawa
 
Wakati baadhi ya watanzania wakisubiri taarifa kutoka kwenye kile kikao cha wafanya mazingaombwe maarufu wa Tanzania, leo Gazeti la Mwananchi limechapisha mahojiano kati yake na Mdhamini wa BAKWATA, Omary Nzowa.

Katika makala inayoelezea Historia ya kuanzishwa kwa Baraza Kuu La Waislamu Tanzania (BAKWATA) Omary Nzowa amekanusha habari kwamba Baraza hilo lilianzishwa kwa shinikizo la Serikali zama za Mwalimu akiwa ndiye rais wa Tanzania.

Omary Nzowa amesema hoja ya kuanzishwa kwa BAKWATA na kutoka kwenye Jumuiya wa Waislamu wa Afrika ya Mashariki, ilitoka kwa Waisalmu wenyewe wa Tanganyika na siyo toka serikalini.

Nzowa amesema kwamba kabla ya Kikao cha waislamu toka nchi nzima ya Tanganyika kilichofanyika kwenye chuo cha Mkwawa mjini Iringa mwaka 1963. waislamu walishaonesha kutokuwa na imani na jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa na kiongozi wa Jumuia ya waisimailia duniani, Aga Khan.

Hoja ya Nzowa inawezekana likawa ni pigo kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwa wanasema kwamba BAKWATA ilianzishwa na Nyerere kama njia yake ya kuwahujumu waislamu wa nchi hii.

Nakala kwa:

Mohamed Said
FaizaFoxy
Allen...
Sijapata hapa JF kuandika nikaanza na kumtaja Allah.
Lakini kwa hili jinsi ya uzito wake nitaanza kwa kumtaja Mungu.

Bismillah Rahman Rahim...

Nimesoma makala ya Omary Nzowa katika Mwananchina wala sikuwa na haja ya kutaka
kumjibu kwani historia ya BAKWATA ni mashuhuri yeye anaijua kama wanavyoijua wengi
katika jamii ya Waislam.

Bwana Nzowa ni Muislam na kama Muislam anamjua Allah na uwezo wake usio
na kikomo na ikiwa atasoma haya niliyoandika hapa atajua kwa nini mimi nimeamua
kumtanguliza Allah katika haya majibu yangu na kama ana akili atawaidhika.

Bwana Nzowa atajua nimelitanguliza jina la Allah ili Yeye Mwenyezi Mungu atushuhudie
baina ya Bwana Nzowa na mimi ni nani anaesema kweli.

Sina ujasiri wa kumwita Allah kama shahidi katika jambo la uongo.

Bwana Omary Nzowa kasema uongo katika jambo la dini na Allah anajua na Waislam
wote wanajua kuwakasema uongo na yeye mwenyewe Bwana Nzowa nafsi yake inajua
kuwa kasema uongo.

Ingetosha kwangu mimi nikasimama hapa ikawa mwisho wa maneno yangu lakini hakika
naamini kuna watu watataka kujua ukweli ni upi?

Naweka hapo chini ujumbe niliomwandikia mmoja wa viongozi wa BAKWATA kama
zinduo kwao nikiamini kuwa na wasomaji watajua nini khasa ilikuwa sababu ya serikali
kuivunja EAMWS:

''Baada ya uhuru kupatikana mwaka 1961 Waislam waliamini kuwa hali yao ya baadae
katika serikali huru itakuwa nzuri.

Mwaka 1962 ukaitishwa mkutano wa Waislam wa nchi nzima kujadili nafasi ya Uislam
katika Tanganyika huru.

Taasisi zifuatazo zilihudhuria mkutano huo: East African Muslim Welfare Society (EAMWS),
Daawat Islamiyya, Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika
na Muslim Education Union.

Mkutano ule ulikubaliana pamoja na mambo mengine umuhimu wa kuanzisha Idara ya Elimu
chini ya EAMWS.

Waislam hawakusubiri serikali itimize ahadi yake ya kurekebisha upogo uliokuwepo wa
elimu nchini.

Waislam walianzisha mipango yao wenyewe ili isaidiane na juhudi ya serikali.

Mipango ikatayarishwa ya kujenga shule Tanganyika nzima na mwishowe kujenga Chuo
Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya Mashariki.

Mkutano ukamchagua Tewa Said Tewa waziri wa serikali, mwanasiasa wa TAA na mmoja
wa wale wazalendo 17 walioanzisha TANU kuwa mwenyekiti wa EAMWS kwa upande wa
Tanganyika.

Huu ndiyo ukawa mwanzo wa uadui kati ya Waislam na serikali.

Uelewano uliodumu wakati wa kudai uhuru ukaanza kutoweka na siasa zikachukua sura
mpya ya uhasama, kutoaminiana na kutafutana.

Kisa cha hali hii mpya ikiwa ni sababu ya Waislam kutaka kuondoa hali ya kikoloni ambayo
iliyowakandamiza kwa miaka mingi kwa kuwanyima elimu.

Waislam waliona kuwa hili lilikuwa ni jambo lisilokuwa na pingamizi kufanyika.

Uhuru walioupigania ili uwe na maana ni lazima Waislam wajitoe ndani ya unyonge wa miaka
mingi waliogubikwa na wakoloni.

Hii ilisababisha hofu kuu na ikawa lazima EAMWS ivunjwe na BAKWATA iundwe ili hizi juhudi
za kuelimisha Waislam zikome mara moja.''

Bwana Allen,
Hivi ndivyo mipango yote ya elimu chini ya EAMWS na ujenzi wa Chuo Kikuu ilivyohujumiwa.

Bwana Nzowa hakuwa na ujasiri wa kuyaeleza haya wala kusema kuwa BAKWATA iliundwa
baada ya mgogoro uliodumu takriban miezi mitatu.
 
Back
Top Bottom