Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 25,941
- 51,063
Wakati baadhi ya watanzania wakisubiri taarifa kutoka kwenye kile kikao cha wafanya mazingaombwe maarufu wa Tanzania, leo Gazeti la Mwananchi limechapisha mahojiano kati yake na Mdhamini wa BAKWATA, Omary Nzowa.
Katika makala inayoelezea Historia ya kuanzishwa kwa Baraza Kuu La Waislamu Tanzania (BAKWATA) Omary Nzowa amekanusha habari kwamba Baraza hilo lilianzishwa kwa shinikizo la Serikali zama za Mwalimu akiwa ndiye rais wa Tanzania.
Omary Nzowa amesema hoja ya kuanzishwa kwa BAKWATA na kutoka kwenye Jumuiya wa Waislamu wa Afrika ya Mashariki, ilitoka kwa Waisalmu wenyewe wa Tanganyika na siyo toka serikalini.
Nzowa amesema kwamba kabla ya Kikao cha waislamu toka nchi nzima ya Tanganyika kilichofanyika kwenye chuo cha Mkwawa mjini Iringa mwaka 1963. waislamu walishaonesha kutokuwa na imani na jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki iliyoanzishwa na kiongozi wa Jumuia ya waisimailia duniani, Aga Khan.
Hoja ya Nzowa inawezekana likawa ni pigo kubwa kwa baadhi ya watu waliokuwa wanasema kwamba BAKWATA ilianzishwa na Nyerere kama njia yake ya kuwahujumu waislamu wa nchi hii.
Nakala kwa:
Mohamed Said
FaizaFoxy