BAKWATA waomba serikali kuharakisha upelelezi kesi za ugaidi

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeviomba vyombo vya dola kuharakisha upelelezi wa kesi za ugaidi ili haki itendeke kwa wakati.

Mwishoni mwa mwaka jana baraza hilo lilitahadharisha kuwa suala la ugaidi linaweza kutumiwa kama njia ya kulipiza visasi katika jamii na kusababisha raia wema wasio na hatia kuhusishwa na vitendo hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, alisema haki inatakiwa ionekane inatendeka na kitendo cha kuichelewesha ni sawa na kumnyima mtu haki yake.

“Sio masheikh tu bali waumini wote wanaohusishwa na kesi za ugaidi, tunaomba upelelezi uharakishwe ili kesi zilizokaa muda mrefu ziweze kufikia mwisho, na watakaoonekana wana hatia wahukumiwe na wasio na hatia waachiwe huru na kuendelea na shughuli zao,” alisema.

Alisema Katiba imetamka wazi kwamba mtu yeyote atabaki kuwa mtuhumiwa hadi mahakama itakapothibitisha kosa lake. Hivi karibuni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislam ya Imam Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, aliwataka waislamu wote nchini kuungana na kupigania haki za masheikh na waislamu waliopo magerezani.

Mwezi uliopita pia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alimtaka Rais Dk. John Magufuli kutafakari upya juu ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho ambao wanasota gerezani kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Chanzo: Mtanzania
 
Bakwata nao wameshanunuliwa Siku zote mlikuwa wapi nimeamni lowassa ni kirusi kibaya sana kama serikali haitokuwa makini nae taifa letu litaingia kwenye matatizo makubwa na vita yenyewe kwa wenyewe inaweza ikatoke kama wakimchukilia poa lowassa huyu mzee sio MTU mzuri nimeshajua kwann mwalimu alimkataa
 
Wawakamate kwa uchochezi basi kama Lowssa!!! Kwenye mambo kama haya hutomuona Alhad Musa-Sheih wa BAKWATA DAR wala sheikh Mkuu!!

Uzuri hii karata inazidi kunoga,tarehe 20 July lazima Grey hair wamuache ama waamshe tafrani!!

Kama kumnyamazisha basi wamfungulie kesi za ufisadi na uhujumi uchumi tu ila kwa suala la masheikh itakuwa sawa na kuchambia mkuki mtu anayeharisha!!!!!!!!!!!
 
Hawa wameamka leo... Kazi kweli kweli. Hapo wametumwa na Lumumba sababu wameona yule mzee kaliamsha kwahiyo waislam wengi wanamuona angalau anawazungumzia mashehe kuliko Bakwata, sasa nawao wameamshwa na Harakaharaka wa Lumumba..
 
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeviomba vyombo vya dola kuharakisha upelelezi wa kesi za ugaidi ili haki itendeke kwa wakati.

Mwishoni mwa mwaka jana baraza hilo lilitahadharisha kuwa suala la ugaidi linaweza kutumiwa kama njia ya kulipiza visasi katika jamii na kusababisha raia wema wasio na hatia kuhusishwa na vitendo hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, alisema haki inatakiwa ionekane inatendeka na kitendo cha kuichelewesha ni sawa na kumnyima mtu haki yake.

“Sio masheikh tu bali waumini wote wanaohusishwa na kesi za ugaidi, tunaomba upelelezi uharakishwe ili kesi zilizokaa muda mrefu ziweze kufikia mwisho, na watakaoonekana wana hatia wahukumiwe na wasio na hatia waachiwe huru na kuendelea na shughuli zao,” alisema.

Alisema Katiba imetamka wazi kwamba mtu yeyote atabaki kuwa mtuhumiwa hadi mahakama itakapothibitisha kosa lake. Hivi karibuni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislam ya Imam Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, aliwataka waislamu wote nchini kuungana na kupigania haki za masheikh na waislamu waliopo magerezani.

Mwezi uliopita pia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alimtaka Rais Dk. John Magufuli kutafakari upya juu ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho ambao wanasota gerezani kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Chanzo: Mtanzania
BAKWATA nina waheshimu sana ila kwa hili la viongozi wa UAMSHO nawakatalia

UAMSHO ni hatari kwa usalama wa nchi, muungano wetu na umoja wa kitaifa

Kamwe viongozi wa UAMSHO wasiachiwe

Cc: TISS, TPDF, Police Force, Tanzania Prison Force, Union government, The ruling party, Judges, and All nationalists
 
Back
Top Bottom