BAKWATA waomba serikali kuharakisha upelelezi kesi za ugaidi

Ukiangalia kwa jicho la tatu unaweza kujiuliza, ni uamsho kweli wanaotetewa au ni yule naniliu ndio anatetewa kiaina?!!!
Mkuu vipi hoja ya mleta unaona haina mashiko? Watu wazima wanashauri uchambaji ufanyike kikamilifu hadi kunawa mikono iliyotumika.
 
BAKWATA nina waheshimu sana ila kwa hili la viongozi wa UAMSHO nawakatalia

UAMSHO ni hatari kwa usalama wa nchi, muungano wetu na umoja wa kitaifa

Kamwe viongozi wa UAMSHO wasiachiwe

Cc: TISS, TPDF, Police Force, Tanzania Prison Force, Union government, The ruling party, Judges, and All nationalists
Wewe itakuwa ni lukuvi,hatari ya usalama wetu ni ccm.
 
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeviomba vyombo vya dola kuharakisha upelelezi wa kesi za ugaidi ili haki itendeke kwa wakati.

Mwishoni mwa mwaka jana baraza hilo lilitahadharisha kuwa suala la ugaidi linaweza kutumiwa kama njia ya kulipiza visasi katika jamii na kusababisha raia wema wasio na hatia kuhusishwa na vitendo hivyo.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, alisema haki inatakiwa ionekane inatendeka na kitendo cha kuichelewesha ni sawa na kumnyima mtu haki yake.

“Sio masheikh tu bali waumini wote wanaohusishwa na kesi za ugaidi, tunaomba upelelezi uharakishwe ili kesi zilizokaa muda mrefu ziweze kufikia mwisho, na watakaoonekana wana hatia wahukumiwe na wasio na hatia waachiwe huru na kuendelea na shughuli zao,” alisema.

Alisema Katiba imetamka wazi kwamba mtu yeyote atabaki kuwa mtuhumiwa hadi mahakama itakapothibitisha kosa lake. Hivi karibuni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kiislam ya Imam Bukhary, Sheikh Khalifa Khamis, aliwataka waislamu wote nchini kuungana na kupigania haki za masheikh na waislamu waliopo magerezani.

Mwezi uliopita pia Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alimtaka Rais Dk. John Magufuli kutafakari upya juu ya masheikh wa Jumuiya ya Uamsho ambao wanasota gerezani kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Chanzo: Mtanzania
hawana mpya njaa tu inawasumbua hao
 
BAKWATA nina waheshimu sana ila kwa hili la viongozi wa UAMSHO nawakatalia

UAMSHO ni hatari kwa usalama wa nchi, muungano wetu na umoja wa kitaifa

Kamwe viongozi wa UAMSHO wasiachiwe

Cc: TISS, TPDF, Police Force, Tanzania Prison Force, Union government, The ruling party, Judges, and All nationalists
nani kasema?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ASANTE UJUMBE WA KUZARAULIWA HIKI CHOMBO CHA SEREKALE UMEKIINGIA NA SASA ETI SAA 12 JIONI NDIO MNAAMKA. HOVYO KABISA NYIE.. MNGEENDELEA KULALA TU KWANI HAMNA FAIDA YOYOTE KWA WAISLAM WA TZ
 
Ndugu wanajamvi someni hayo matamshi ya viongozi hawa wawili halafu mnisaidie tofauti yake, maana mimi sioni tofauti.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, amesema

“tunaomba upelelezi uharakishwe sio kwa masheikh tu bali kwa waumini wote wanaohusishwa na kesi za ugaidi, ili kesi zilizokaa muda mrefu ziweze kufikia mwisho, na watakaoonekana wana hatia wahukumiwe na wasio na hatia waachiwe huru na kuendelea nashughuli zao,”

Edward Lowassa, alisema

"Tunaiomba mahakama iharakishe upelelezi kwa mashehe wa kikundi cha uamsho wanaosota mahabusu kwa tuhuma za ugaidi, kama kuna ushahidi wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria au la waachiwe huru baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka minne bila kushitakiwa".

Kama Lowassa anahojiwa polisi kwa matamshi hayo tutegemee polisi kumuita Sheikh Khamis Mataka kwa mahojiano zaidi.
 
Hii inanikumbusha habar moja hivi niliisoma ktk chanzo flani cha habar,Kipindi kilee cha Ukusanyaji wa Maoni yaKatiba mpya..Chanzo kiliripoti kuwa DC kule Mikoa yaKusini Iringa/Mbeya km sijakosea hivi..kuwa "DC adhalilishwa" Kumvua Kitambaa Cha kichwa mbele ya Umati wa watu na Kundi la watu wanao daiwa kua ni Wafuasi wa Cdm..DC/Mama yule alikua ni Muislam jina..ghafla BAKWATA wakatoa tamko kuwa UISLAMU UMEDHALILISHWA..kwa Mama yule kuvuliwa kitambaa cha Kichwa ktk zile purukushani..Uchunguzi kufanyika ikaonekana yule Mama/DC anaishi naMume Mkristo hapo inaMaana hakuna ndoa,af kingine hapo kwao wanapoishi wanafuga Nguruwe..(Astaqafiru llah)..ivo hapo haitaji tena kujua Uhalali wa Uumini ktk dini ya Kiislamu kwa huyo Mama,na pili huitaji Kuwa na imani na BAKWATA hata kama wakisema ukweli Maishani.
 
Ndugu wanajamvi someni hayo matamshi ya viongozi hawa wawili halafu mnisaidie tofauti yake, maana mimi sioni tofauti.

Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, amesema

“tunaomba upelelezi uharakishwe sio kwa masheikh tu bali kwa waumini wote wanaohusishwa na kesi za ugaidi, ili kesi zilizokaa muda mrefu ziweze kufikia mwisho, na watakaoonekana wana hatia wahukumiwe na wasio na hatia waachiwe huru na kuendelea nashughuli zao,”

Edward Lowassa, alisema

"Tunaiomba mahakama iharakishe upelelezi kwa mashehe wa kikundi cha uamsho wanaosota mahabusu kwa tuhuma za ugaidi, kama kuna ushahidi wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria au la waachiwe huru baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka minne bila kushitakiwa".

Kama Lowassa anahojiwa polisi kwa matamshi hayo tutegemee polisi kumuita Sheikh Khamis Mataka kwa mahojiano zaidi.
kwa kauli hii sheikh mataka anafaa sana kusaidia GESHI RETU... ngoja tuone uongozi wa JUU utatoa kauli gani akamatwe ahojiwe au tumuache sababu bakwata ni tawi letu tutaharibu mambo.
 
Bakwata hovyo ,hili siyo jambo la kuomba. Bakwata should demand unconditional release of Muslims unjustly detained.
 
BAKWATA nina waheshimu sana ila kwa hili la viongozi wa UAMSHO nawakatalia

UAMSHO ni hatari kwa usalama wa nchi, muungano wetu na umoja wa kitaifa

Kamwe viongozi wa UAMSHO wasiachiwe

Cc: TISS, TPDF, Police Force, Tanzania Prison Force, Union government, The ruling party, Judges, and All nationalists
Kwanini usisome bandiko lote ndio utoe mchango wako? Hakuna mahali bakwata wamesema waachiwe.

Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
 
Kanuni/Sheria za Wizara ya Mambo ya Ndani

Kuanzia kesho na kuendelea kutakuwa na kuna kanuni mpya za mawasiliano.

Simu zote zinarikodiwa.

Simu zote zinazorikodiwa zinahifadhiwa.

Whatsapp inafuatiliwa.

Twitter inafuatiliwa.

Facebook inafuatiliwa.

Vyombo vyote vya habari vya kijamii na vikao vinafuatiliwa

Waambie wale wasiojua.

Vifaa vyako vinaunganishwa na mifumo ya huduma ya wizara.

Jihadharini kutuma ujumbe usiohitajika.

Wajulishe watoto wako, jamaa na marafiki zako kuhusu jambo hili ili wawe waangalifu.

Usitume machapisho au video yoyote n.k unayoipokea kuhusu siasa / hali ya sasa kuhusu Serikali / PM nk.

Polisi wameweka taarifa inayojulikana .. Uhalifu wa Cyber ... na hatua itachukuliwa ... futa tu ...

Wajulishe rafiki zako na wengine pia.

Kuandika au kupeleka meseji yoyote ya mjadala wa kisiasa na kidini ni kosa kwa sasa .... kukamatwa bila hati ...

Hili ni jambo nyeti sana. Tafadhali wajulishe wanachama wetu wote wa groups (vikundi) vyetu, na kwa Admin wa Groups inaweza kuwa matatizo makubwa.

Jihadharini kutuma ujumbe usiohitajika.

Mwambie kila mtu juu ya hili ili awe na tahadhari.

Tafadhali tuma hii kwa wengine; Ni kweli sana.

IMETUMWA KAMA ILIVYOPOKELEWA
43303dda8c6059b4d4e3667019db613f.jpg

Back
Top Bottom