Siri wajumbe kamati ya BAKWATA kujiengua

Oldmantz

JF-Expert Member
Jan 24, 2023
428
996
Siku moja baada ya wajumbe watano kati ya saba wa kamati ya maboresho ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kujiuzulu, wajumbe hao wameeleza sababu za kufanya hivyo, ikiwamo ugumu wa kupata taarifa sahihi za fedha.

Kamati hiyo ilizinduliwa na Mufti, Abubakar Bin Zubeir, Februari 16, mwaka huu ikiongozwa na Mwenyekiti, Sheikh Issa Othman Issa, ambaye jana alitangaza kujiuzulu kwa kumwandikia barua Sheikh Zubeir ambaye naye alimtangaza Alhaj Suleiman Kova kungoza tume hiyo.

Mbali na Sheikh Issa wajumbe wengine waliomua kujiweka kando ni Mohammed Nyengi, Daudi Nasib, Iddi Kamazima na Omar Igge, huku Sheikh Qaasim Jeizani na Alhaj Nuhu Mruma ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Bakwata, wakisalia kwenye tume hiyo.

Licha ya barua ya wajumbe hao kujiuzulu pasina kuweka wazi sababu, gazeti hili limejuzwa na chanzo cha ndani ya Bakwata kuwa, tume ilipokuwa inatekeleza majukumu yake, ilikosa ushirikiano wa kuhakiki madeni.

“Wamekaa kando kwani waliotakiwa kuwapa ushirikiano wamekuwa wakitoa sababu nyingi. Ili wajumbe waweze kutekeleza majukumu yao, walipaswa kuhakiki mali mfano za Wakfu, sasa hili limeshindikana na wao wameona hawawezi kufanya lolote,” kilieleza chanzo chetu na kuongeza:

“Unajua zile mali za Wakfu kama majumba na viwanja ni vingi, lakini kuna wajanja wananufaika nao, wakati utaratibu ukiwekwa vizuri Bakwata itakuwa na fedha za kutosha kujiendesha na kuacha kuomba omba.”

Chanzo kingine kilieleleza: ‘‘Uhakiki huo ukifanyika na kumalizika, kuna watu watakosa kunufaika na mali za Wakfu ambao wamezigeuza kama kitega uchumi chao. Kwa hiyo kinachohitajika ni lazima utashi kweli uwepo kwa viongozi wenyewe wa Bakwata.”

Mmoja wa muumini wa Kiislamu, Salehe Abdallah ambaye ni Mkazi wa Jijini Dar es Salaam alisema, ili suala hilo liweze kufanyika kwa ufanisi, kuna haja ya wajumbe kutoka nje ya Bakwata. “Tume inayoundwa itoke nje ya Bakwata lakini ipewe ushirikiano bila hivyo, zitaundwa tume hata kumi hazitafanikiwa.”

Alichosema Sheikh Issa
Jana, gazeti hili lilizungumza na aliyekuwa Mwenyekiti, Sheikh Issa, ambaye pia ni Imam mkuu wa Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, aliyesema kuwa alichofanya ni kuripoti kwa kiongozi wake, huku akishangaa barua yake kusambaa mitandaoni.

“Siwezi kuongea zaidi, mimi nilikuwa naripoti tu kwa kiongozi wangu na hata hiyo barua kusambaa mitandaoni, nashangaa imefikaje huko, kwani ilikuwa ni ripoti ya ndani,’’ alisema Sheikh Issa aliyedai kuwa kwa nafasi yake kama mjumbe wa ulamaa hawezi kuongea zaidi.

Hata hivyo, katika barua yake, Sheikh Issa aliandika kuwa lengo lake na wajumbe wenzake kuchukua uamuzi huo ni kudumisha umoja ndani ya Baraza pamoja na kuondosha taharuki kubwa iliyojitokeza ndani ya baraza.”

Katibu Bakwata ajibu
Kwa upande wake, Alhaj Mruma alisema: “Hao waliojiuzulu na mimi nimeona kwenye mitandao, bahati mbaya siko Dar es Salaam niko safarini. Wenye maelezo mazuri ni hao waliojiuzulu na huyo aliyepelekewa, mimi kama mjumbe nafasi yangu inabaki palepale kama mjumbe.”

Alisema akirejea jijini Dar es Salaam atazungumza na mwenyekiti pamoja na Mufti Zubeir. Hata hivyo, jitihada za gazeti hili kumpata Mufti jana hazikuzaa matunda.

Kuhusu madai ya wajumbe waliojiuzulu, Alhaj Mruma alisema ni kweli kulikuwa na changamoto za kibenki zilizoainishwa na wajumbe.

‘‘Kulikuwa na changamoto za kibenki na wao waliziainisha na sisi kama Bakwata tukazifanyia kazi, lakini kabla hatujamaliza hizo changamoto zingine zilitokea, tukaingia kwenye likizo za Eid,’’ alisema na kuongeza:

“Hazikuwa changamoto zinazokwamisha kwa asilimia 100, lakini kuna sehemu watia saini walipaswa kusaini ili kupata ‘bank statement (taarifa za benki) “alisema.

Sheikh Ponda aguswa
Sakata la mali za Bakwata na kujiuzulu kwa wajumbe hao, kumemuibua Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyeeleza kuwa atalizungumzia suala hilo leo mbele ya wanahabari.

MWANANCHI
 
Hiyo taasisi ya Ponda iko ndani ya Bakwata?
Kama sio Mambo ya Bakwata anayaingiliaje?
Awaache ma alwatan wapige pesa.
 
BAKWATA ni taasisi ya kidini, iweje iwe na mgogoro wa kuhakiki mali zake, kwani miongoni mwao hakuna waumini waaminifu kwa mali zao, mbona wanatia aibu kwa imani yao?
 
Nyumba na ardhi zulizotolewa waqf naona wamejigawia wote ndio maana wanaona aibu
Majizi yamejaa kila kona
Ila kama wamejiuzuru kwa sababu nao wamepiga nyumba na ardhi za waqf basi ni laana kubwa sana
 
BAKWATA ni taasisi ya kidini, iweje iwe na mgogoro wa kuhakiki mali zake, kwani miongoni mwao hakuna waumini waaminifu kwa mali zao, mbona wanatia aibu kwa imani yao?
Bakwata ni tawi la ccm ndio maana wanafanana tabia
 
Siku moja baada ya wajumbe watano kati ya saba wa kamati ya maboresho ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) kujiuzulu, wajumbe hao wameeleza sababu za kufanya hivyo, ikiwamo ugumu wa kupata taarifa sahihi za fedha.

Kamati hiyo ilizinduliwa na Mufti, Abubakar Bin Zubeir, Februari 16, mwaka huu ikiongozwa na Mwenyekiti, Sheikh Issa Othman Issa, ambaye jana alitangaza kujiuzulu kwa kumwandikia barua Sheikh Zubeir ambaye naye alimtangaza Alhaj Suleiman Kova kungoza tume hiyo.

Mbali na Sheikh Issa wajumbe wengine waliomua kujiweka kando ni Mohammed Nyengi, Daudi Nasib, Iddi Kamazima na Omar Igge, huku Sheikh Qaasim Jeizani na Alhaj Nuhu Mruma ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Bakwata, wakisalia kwenye tume hiyo.

Licha ya barua ya wajumbe hao kujiuzulu pasina kuweka wazi sababu, gazeti hili limejuzwa na chanzo cha ndani ya Bakwata kuwa, tume ilipokuwa inatekeleza majukumu yake, ilikosa ushirikiano wa kuhakiki madeni.

“Wamekaa kando kwani waliotakiwa kuwapa ushirikiano wamekuwa wakitoa sababu nyingi. Ili wajumbe waweze kutekeleza majukumu yao, walipaswa kuhakiki mali mfano za Wakfu, sasa hili limeshindikana na wao wameona hawawezi kufanya lolote,” kilieleza chanzo chetu na kuongeza:

“Unajua zile mali za Wakfu kama majumba na viwanja ni vingi, lakini kuna wajanja wananufaika nao, wakati utaratibu ukiwekwa vizuri Bakwata itakuwa na fedha za kutosha kujiendesha na kuacha kuomba omba.”

Chanzo kingine kilieleleza: ‘‘Uhakiki huo ukifanyika na kumalizika, kuna watu watakosa kunufaika na mali za Wakfu ambao wamezigeuza kama kitega uchumi chao. Kwa hiyo kinachohitajika ni lazima utashi kweli uwepo kwa viongozi wenyewe wa Bakwata.”

Mmoja wa muumini wa Kiislamu, Salehe Abdallah ambaye ni Mkazi wa Jijini Dar es Salaam alisema, ili suala hilo liweze kufanyika kwa ufanisi, kuna haja ya wajumbe kutoka nje ya Bakwata. “Tume inayoundwa itoke nje ya Bakwata lakini ipewe ushirikiano bila hivyo, zitaundwa tume hata kumi hazitafanikiwa.”

Alichosema Sheikh Issa
Jana, gazeti hili lilizungumza na aliyekuwa Mwenyekiti, Sheikh Issa, ambaye pia ni Imam mkuu wa Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam, aliyesema kuwa alichofanya ni kuripoti kwa kiongozi wake, huku akishangaa barua yake kusambaa mitandaoni.

“Siwezi kuongea zaidi, mimi nilikuwa naripoti tu kwa kiongozi wangu na hata hiyo barua kusambaa mitandaoni, nashangaa imefikaje huko, kwani ilikuwa ni ripoti ya ndani,’’ alisema Sheikh Issa aliyedai kuwa kwa nafasi yake kama mjumbe wa ulamaa hawezi kuongea zaidi.

Hata hivyo, katika barua yake, Sheikh Issa aliandika kuwa lengo lake na wajumbe wenzake kuchukua uamuzi huo ni kudumisha umoja ndani ya Baraza pamoja na kuondosha taharuki kubwa iliyojitokeza ndani ya baraza.”

Katibu Bakwata ajibu
Kwa upande wake, Alhaj Mruma alisema: “Hao waliojiuzulu na mimi nimeona kwenye mitandao, bahati mbaya siko Dar es Salaam niko safarini. Wenye maelezo mazuri ni hao waliojiuzulu na huyo aliyepelekewa, mimi kama mjumbe nafasi yangu inabaki palepale kama mjumbe.”

Alisema akirejea jijini Dar es Salaam atazungumza na mwenyekiti pamoja na Mufti Zubeir. Hata hivyo, jitihada za gazeti hili kumpata Mufti jana hazikuzaa matunda.

Kuhusu madai ya wajumbe waliojiuzulu, Alhaj Mruma alisema ni kweli kulikuwa na changamoto za kibenki zilizoainishwa na wajumbe.

‘‘Kulikuwa na changamoto za kibenki na wao waliziainisha na sisi kama Bakwata tukazifanyia kazi, lakini kabla hatujamaliza hizo changamoto zingine zilitokea, tukaingia kwenye likizo za Eid,’’ alisema na kuongeza:

“Hazikuwa changamoto zinazokwamisha kwa asilimia 100, lakini kuna sehemu watia saini walipaswa kusaini ili kupata ‘bank statement (taarifa za benki) “alisema.

Sheikh Ponda aguswa
Sakata la mali za Bakwata na kujiuzulu kwa wajumbe hao, kumemuibua Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, aliyeeleza kuwa atalizungumzia suala hilo leo mbele ya wanahabari.

MWANANCHI
Bakwata hata sh 10,000,000/benki hawana anae bisha tuko hapa tusubili kwanza hawana miradi wala msikiti walio ujenga maisha yao wanategemea mali za waqf tu kodi za majumba na kuomba misaada serikalini tu hakuna mfadhiri anae weza kuipa bakwata hata sh 100 hawa aminiki hao wakiona hela roho inawataka

Wakati inaanzishwa wafadhiri waliweka hela zao nyingi mfano rais wa misiri miaka hiyo anuari sadati alipa Dolla 800 nchi nyingine ikawapa magali mafiati yenye tela yakaishia kukodiwa na kusomba pombe

Waisilamu wakatoa wakif mashamba majumba viwanja hela kama sio ufujaji baada ya tasisi ya kiloma ingekuwa inafuatia bakwata

Kila kiongozi akija anajitia heti kudhibiti mali za waisilamu kumbe uongo mtupu mfano sheikh ponda alipo fatilia sheikh issa simba akasema huyo ahusiki na mali hizo zaidi hanahatarisha amani serikali ikaanza kutafuta utadhani alitaka kupindua rais Kikwete

Nguvu ya bAkwata hiko serikalini kazi ya bakwata kuvizia waisilamu wakisha jenga misikiti wao usajili na kuita mali yao wakati wa Magufuli ukisikika unaikosoa ccm ukiwa msikitini viongozi wa bakwata wanapiga simu polisi na kusema unahatarisha amani unasombwa hao wazee wote wa bakwata kuanzia muft mpaka sheikh wa kata wete hao ni vibaraka wa ccm

Wanacho pata zaidi kutoka ccm hakipo labda mufuti na kundi lake na masheikh wa mkoa kidogo ndio wanakula hasa mfuti walio baki masheikh wa wilaya mikoa zaidi wanaambulia bahasha baada ya kuomba dua kwenye mikutano na kupikiwa futari na wabunge na wenyeviti wa vyama mwezi wa ramadhani zaidi ya hapo hawati chochote

Bora ya mbunge wa cdm alie hasi na kuhamia ccm na kupewa ukuu wa wilaya wakati bado mbunge wa Ifakara alimnunulia sheikh wakoa Ifakara pikipiki mpiya akampa nampongeza sana bwana jua kali ingawa alisha hamia ccm lakini wema wako ulio ufanya kwa sheikh wa bakwata Ifakara Morogoro hautasaulika

Sio kama wa ccm kuishia kuwapa futari na uji na sh 1000,000,baada ya kusoma dua kwenye mikutano serikali ujitoe bakwata hili waisilamu Wawa nyooshe hao waizi walio jazana wilayani na mkoani na pale kinondoni kwenye majengo yaliyo chakaa miaka yote tangu yalipo tolewa wakf kidogo Makonda ndie kayajenga na kuyakarabati bakwata hawafai wala hawa aminiki
 
Back
Top Bottom