Bahati Bukuku amuimbia Lowassa wimbo

Bahati Bukuku amuimbia Lowassa wimbo

Amaonesha dhairi yuko kwa ajiri ya mini( umalaya) na binafsi niseme ukweli,Bukuku alikuwa ni mwimbaji wangu simply the best.Sasa kuanzia sasa she is bullshit,choko tu kama wenzie!

Unapomuita Mama wa watu choko, je Mama yako akiitwa choko utajali?
 
Mbona Edward Sambai unahangaika sana na jambo lisilo kuhusu? Kila mtu ana haki ya kufanya jambo lolote lile bila kuvunja sharia.Sasa dada yetu Bahati Bukuku kaamua kwa moyo safi kabisa kumtungiwa wimbo murua Mh.Edward Ngoyai Lowasa akimsifia kwa mazuri yote anayoyafanya kwa jamii yetu ya watanzania lakini wewe hii inakuuma saaaana kwanini? Au ulitaka amuimbie nani? Mwacheni Bahati Bukuku atimize kile nfsi yake imemtuma afanye.Mbona nyie mnafurahia sana Kakobe kuiunga mkono Chadema?Sisi watanzania wapenda amani na wenye mapenzi mema nchi yetu tumefurahshwa sana na mtumishi wa Mungu kuona na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na Mh.LOWASA.MUNGU MPE ULINZI WA KUTOSHA MAANA WENYE WIVU NA CHUKI NI WENGI SANA.

Nani kwakwambia kuwa hili jambo haliniusu?

Bahati bukuku alijipambanua kuwa ni muimba nyimbo za Mungu na tumekuwa tukinunua CD as to sacrifice to Gog. Sasa leo baada ya kupata umaarufu kutokana na sadaka zetu ndo aje kusifia watu wasiostaili ata kuitwa muumini sembuse kumfananisha na Mfale Daudi au Sulemani?

Ni bora sasa Bukuku ajitangaze rasmi kuwa yeye ni mfanya biashara wa mziki kama kina Jide na Dimond ili aandaliwe show na Clouz FM, na sio kujificha nyuma ya kanisa na kuja kuza CD zake kwenye mikutano ya Injili na ndani ya makanisa.
 
Na papa msofe na ndama mtoto ya ng'ombe anavyoimbwa na wazee wa ngwasuma hao unaweza kuwaitaje kama bahati bukuku umemuita mala.ya?
 
Naona sasa kila hoja mnaokuja nao ni kututenga kwa misingi ya kidini!! Kuanza kuhusisha kila jambo na udini ni kuamusha hasira za watanzania wakati tuko wamoja bila kujali dini zetu...Sijaona MANTIKI yoyote ya kulihusisha mambo haya na udini vinginevyo ninachoona ni kutugawa watanzania kwa misingi ya kidini ili kufanikisha malengo yenu ya kisiasa!! Mods mada kama hizi zenye kuamsha hisia za kidini msiwe mnaruhusu kabisa na ikiwezekana wahusika wafungiwe.
 
jana ulikuja na cd ya lowasa kwenda kwenye mazishi ya John nyerere baada ya kuona lowasa ndiye kiongozi wa juu aliyehudhuria na kupewa heshima kubwa kiitifaki na pia familia ya Mwalimu Nyerere leo mmekuja na CD mpya nawahakikishia lowasa anakua rais mchana kweupe na tayari mmeshasambaratka timu mdmu lakini silaha zilezile lowasa alizotumia kumuingiza kikwete ikulu ndizo hizohizo atakazoziongeza makali kuingia ikulu time will tell tupo....Team Membe ata mbinu mliyotumia kumtumia kinana na Mangula kusimamisha wagombea tunajua mlengwa ni lowasa ila mbinu yenu tuliijua kabla kwanini mnaogopa kupambana na lowasa uwanjani na mnatumia hujuma jibu ni kuwa anawazidi uwezo .....ukawa nao kwenye vikao vya siri mnamuofia lowasa mktoka mafchon mnakohoa facebook za watoto wakati mnajua lowasa ni kiboko yenu

Naona mnampenda sana Edward Lowasa, mungu naye karibu atampenda zaidi ili kuirekebisha akili yenu inayokengeuka haiyumkini kuwapotosha wateule.

Mwenzake kepteni aliacha wosia azikwe kwa kutumia mitambo, musee asituachie wosia mgumu i.e ng'ombe watumike kufukia kaburi halafu bahati bukuku ndiye amsindikize kwa kupakata jeneza na kufukiwa akitumbuiza kwa wimbo huu huu mnaoupenda.
 
Mwenzenu kaingiza hela siku nyie mnakalia kakosea wewe mkosoe mwenzio anapiga mahela.. Jiachie tu mwanawani utakuja kupata ukuu wa wilaya..
 
Njaa mbaya Sana huyo mchumia tumbo kashindwa kuimba injili kahamia siasa
 
6. Kumpigia debe mgombea ni kuwagawa waumini. Kuna wafuasi wa Bahati Bukuku hawamkubali Lowassa, sasa haoni anawakwaza?o

7. Pia Kuna wafuasi wa Lowassa si Wakristo. Wengine ni waislamu na wengine hawana dini. Sasa Bukuku haoni anawakwaza kwa wimbo wake?


8. Wimbo huu unaibua chuki za kidini na kuonekana Lowassa yupo kwa ajili ya wakristo tu. Kama Lowassa anawapenda pia Waislamu mbona hatujasikia akiimbiwa "Kaswida"? Kumuimbia "mapambio" tu ni ishara ya kuwatenga waislamu na kuwaonesha kuwa Lowassa si mtu wao.

9. Wimbo huu unajenga ushawishi upande mmoja tu wa wakristo. Mbona Waislamu hawakuguswa na wimbo huu? Hivi unawezaje kumshawishi Muumini safi wa kiislamu amkubali Lowassa kwa kusikiliza Pambio??

NB:
Soma post elewa post
Kawaida yake kudandia treni kwa mbele!!!
 
we ndo hamna kitu bukuku kama mtumishi wa mungu hawezi kuwaacha kondoo wake wapotee kwa kufanya uchaguzi wa mtu asie sahihi na hayo ni maoni yake hajakulazimisha pia wewe au mtu yeyote kuamini kama yeye anavoamini
 
Sisi Wa Afrika tuna matatizo sana, angeimbwa Dr Slaa, Kikwete au yeyote tunayempenda hungesikia maneno ya Kashfa.

Who is Sambai and Malisa any way? just a normal human beings.
Great minds discus ideas and foolish mind discus peoples,hapo kuna hoja za kiimani ambazo kama great thinker ungezijibu,

Kwa ufupi MTU aliyejitanabaisha kumtukuza Mungu ni sahihi kutumia maandiko na sifa za wateule wa Mungu kama Suleiman na Saudi na kumpa msaka urais? Tena Mwenye tuhuma za kukosa uadilifu?
 
ELimu yake ni form six

Nakumbuka alimaliza meta sekondari mwaka 2000 alipata divisheni ziro, baada ya hapo sijawahi kusikia kama alijiendeleza tena kielimu au la mpaka nilipokuja kumsikia kwenye nyimbo za injili. over
 
ACHA WIFU WAKO wewe kila MTU ana haki ya kuimbwa akipenda / hata akina papa msofe waliimnwa pia acha! acha! acha hiyo WiFi k.ke.
Kiongozi mtoa hoja hujamwelewa. Kapt John Komba (R. I. P) aliimba kuisifia CCM lakini Hilo halikuwa Tatizo sababu yeye alijipambanua kama mhamasishaji wa Chama. Kitu kinacholeta "ukakasi" kwa dada yetu huyu ni kujipambanua kama mtumishi wa Yahweh akisifu & kutukuza lakini ghafla anaanza kupunguza na kusifia weye pumzi kama yeye. Kama Hilo kaona ndilo lenye kumfaa basi ingekuwa vyema akaifahamisha jamii.
 
11059652_835990166492677_7522716275738120309_n.jpg

MUOGOPENI BAHATI BUKUKU.!

Nimesikitika sana kuusikia wimbo wa Bahati Bukuku aliomuimbia Lowassa na kumpamba kuhusu mbio zake za Urais. Sina tatizo la Lowassa kutafuta Urais maana ni haki yake kikatiba. Ana haki ya kugombea, kupigiwa kura na hata kushinda. Ila nina tatizo na Bukuku aliyeamua kuacha kumuimbia Mungu na kumtukuza mwanadamu.

Nimeainisha makosa 10 ya Bahati Bukuku yanayohusiana na wimbo huo;
1. Bukuku anasema Lowassa atatawala kwa amani na ubora ambao Rais yoyote hataweza kufikia. Hapa kuna makosa mawili. La kwanza ni kusema atatawala.

Nani kamhakikishia Bukuku kuwa Lowassa atatawala? Hivi Bukuku anajua kuwa jina la Lowassa linaweza kupelekwa NEC na lisirudi? Au likarudi halafu wananchi wakamkataa? Sasa yeye anajihakikishiaje kuwa Lowassa atatawala?

2. Pili kasema Lowassa ataongoza kwa ufanisi kuliko wote waliomtangulia na watakaomfuatia. Huu ni ujuha wa kiwango cha "PhD". Hivi unawezaje kupima uwezo wa mtu kabla hajafanya kazi? Ni sawa na kununua nguo za mtoto wa kiume kisa mkeo akiwa na mimba alipenda kula sana ugali, mwishowe anazaliwa wa kike..!

3. Bukuku anasema Lowassa ana hekima kama Suleimani. Hii ni kufuru kubwa kwa Mungu. Maandiko yanasema hakuwahi kutokea mtu mwenye hekima kama Suleimani na hatatokea. Sasa Bukuku kamtoa wapi Lowassa? Ina maana Bukuku ana akili kuliko Mungu aliyeruhusu maandiko hayo?

4. Bukuku anasema Lowassa amepakwa mafuta kama Daudi. Maandiko yanasema Daudi alikuwa Mteule wa Mungu na alipakwa mafuta na Kuhani mkuu Samuel. Kujaribu kumfananisha Lowassa na Daudi ni makosa makubwa. Ni Kuhani gani amempaka mafuta Lowassa? Labda Kuhani Yusuph Makamba.. Na alimpaka mafuta gani? Ya Alizeti au Baby Care.!

5. Si sahihi kwa mtumishi wa kiroho kumfanyia kampeni mgombea waziwazi. Either ni Mchungaji, Padri, Askofu, Sheikh, Ustaadh etc sio sahihi kumsifia mgombea hadharani. Kama unampenda mgombe ibaki moyoni mwako na ufanye maamuzi mwenyewe bila kushawishi wengine.

6. Kumpigia debe mgombea ni kuwagawa waumini. Kuna wafuasi wa Bahati Bukuku hawamkubali Lowassa, sasa haoni anawakwaza?

7. Pia Kuna wafuasi wa Lowassa si Wakristo. Wengine ni waislamu na wengine hawana dini. Sasa Bukuku haoni anawakwaza kwa wimbo wake?

8. Wimbo huu unaibua chuki za kidini na kuonekana Lowassa yupo kwa ajili ya wakristo tu. Kama Lowassa anawapenda pia Waislamu mbona hatujasikia akiimbiwa "Kaswida"? Kumuimbia "mapambio" tu ni ishara ya kuwatenga waislamu na kuwaonesha kuwa Lowassa si mtu wao.

9. Wimbo huu unajenga ushawishi upande mmoja tu wa wakristo. Mbona Waislamu hawakuguswa na wimbo huu? Hivi unawezaje kumshawishi Muumini safi wa kiislamu amkubali Lowassa kwa kusikiliza Pambio??

10. Wimbo huu umemfanya Bukuku kuonekana "Changudoa wa kiroho". Hawezi kuwacheka wanawake wanaouza miili yao kwa fedha, maana na yeye kauza utu wake wa kiroho kwa tamaa ya fedha na mali za dunia.

NB: Kwa ujumla Bukuku amejipunguzia sana heshima yake mbele ya jamii. Waislamu wamemuona ni mdini, wakristo tumemuona mnafiki. Wapo wakristo kadhaa waliojiapiza kutonunua tena kazi zake kutokana na upuuzi alioufanya.

Najua njaa ya pesa ndiyo imemfanya akaamua kuwa vuvuzela la Lowassa. Lakini kwa heshima kubwa aliyokua ameijenga kwenye jamii ni bora asingefanya hiyo kazi. Bora angekubali kukosa hizo hela kuliko upuuzi alioufanya. Njaa ya siku moja haiuwi.

Pesa alizozipata atazitumia na zitaisha lakini doa alilojiwekea halitatoka hata siku anaingia kaburini.

Muasisi wa taaluma ya Public Relations, Arthur Page aliwahi kusema "You may need 20 years to build your reputation, but it takes only 5 seconds to destroy it".

Akimaanisha unaweza kutumia miaka 20 kujenga haiba yako mbele ya jamii lakini sekunde 5 tu zinatosha kuharibu kile ulichokijenga kwa miaka 20. Na hivi ndivyo alivyofanya Bahati Bukuku. R.I.P Bukuku.!

Chanzo: fb




Malisa Godlisten

huo ni mtazamo wako na si wakristo wote au waislamu wote. Acha kubwabwaja wewe.
 
Back
Top Bottom