Narudia tena!
Maana kuna watu wanajifanya njuguyugu hawataki kuelewa!
=========
Bahati Bukuku hana kosa, ni haki yake kumuimbia na kumsifia Lowassa, Ibara ya 18 ya katiba inamruhusu. Acheni umbea na hoja za kijinga. yani leo kwasababu kamuimbia na kumsifu Lowassa ndio amekosea. Mchungaji Msingwa anaisifia CDM na kuihubiri kwenye majukwaa mbona hamjahoji kwanini Mchungaji anakihubiri na kukisifia chama chake wakati yeye ni Mhubiri wa neno la Mungu? Mbona hamjahoji kwanini mchungaji mama Lwakatare anaihubiri na kuisifia CCM wakati yeye ni mhubiri wa neno la Mungu? Watu wazima mnakalia umbea umbea tu. Kama hamjawanyoshea kidole Mchungaji Msigwa, Mchungaji Mama Lwakatare na wengine wote mnaowafahamu, hamna haki ya kumnyoshea kidole Bahati Bukuku, inahitajika mtu mwenye mapungufu ya kifikra kubagua watu hao wa Mungu na kuchagua kuona yupi ana haki na yupi hana haki. Bahati ana haki kama hao watu wa Mungu ambao mmewaangalia miaka yote bila kuwanyoshe kidole. Lowaassa "Kila jaribu ulilopitia maishani mwako, kumbe umebeba majibu ya wengi! Bahati Bukuku.
==========
Taarifa kwa Wote ule mkutano mkubwa wa aina yake nchini wa mhe. edward Lowassa uliotarajiwa kufanyia tar 16 uwanja wa Amani Arsuha umeahirishwa, utatangazwa tena badae. poleni kwa usumbufu wowote uliojitokeza. Wajulishe na ambao bado hawana taarifa ya kuahirishwa kwa mkutano Huo