Bahari ni kiboko ya usafiri wa wachawi

Bahari ni kiboko ya usafiri wa wachawi

Unanikumbusha show za wana Lumumba kwa kuwatumia hawa wanyama!
1454254695426.jpg
 
Aisee....kwa hiyo ile dhana ya uchawi hauvuki bahari ni kweli kumbe.......na hebu tupe hints za Meli ya Nungwi kama unajua chochote ktk ulimwengu wa roho..........
Duh we noma hilo swali akijibu ajibu na la titanic
 
Kaka haya mambo yapo, yapo sana tu.
Watu wanamuona Mshana jr mzushi, lakini ukikaa na waliofanya kazi ya uvuvi kwa miaka mingi huwa wanatoa story mambo wanayokumbana nayo Baharini mpaka unaweza kuona Kama hadithi vile.
Kwa mfano; kwenye miaka ya mwanzoni mwa 1990 au kati kati ya 1990 kuja 2000,niliwahi kusoma Kwenye gazeti la Majira Mwandishi alieponea chupu chupu pamoja na wengine kufa kwenye Meli ya uvuvi.
Mwandishi anasema Safari yao ilianzia Mafia, lakini siku hiyo ilikuwa sio siku ya uvuvi, Samaki walikuwa nao Tayari kwenye Meli, washamaliza kuvua wanarudi Dsm.
Mle ndani ya Meli kulikuwa na wachina 2 ambao ndio walikuwa wamiliki, na wafanyakazi wa ki-TZ idadi yao sikumbuki.
Mwandishi anasema Safari ilienda vizuri tu, kuna sehemu walifika wale wafanyakazi wakamwambia (Mwandishi) ile sehemu ina kina kirefu sana cha maji na ni eneo lenye Samaki wengi lakini ni kipande chenye mauza uza sana.
Kwa mujibu wa Mwandishi muda huo wanapita eneo hilo ilikuwa jioni kabisa.
Ghafla wakaona kiwingu, yaani maji yalikuwa yamefunikwa na ukungu dk chache baadae Mwandishi anasema zikaja dhoruba za kutisha, dk chache baadae ule ukungu ukatoweka.
Ile sehemu ambayo kulikuwa kumefunikwa na ukungu, ulipotoweka wakawa wanaiona Meli Inazama Mwandishi hakujua Kama ya uvuvi au vipi.
Baadae hali ilipokuwa mbaya mmoja ya wale wachina alikuwa kavaa mkufu, akauvua akautupa Baharini, kwenye Meli mle kulikuwa na Mbuzi, akaenda akachukua mmoja akamtupa Baharini pia, halafu akarudi ndani ya Meli, baada ya yule mchina kufanya vile dhoruba ikaanza kupungua nguvu taratibu, na ile Meli waliyokuwa wakiiona ikizama ikapotea Machoni mwao.
Mwandishi nakumbuka alisema lilikuwa tukio la kutisha ambalo kifo kilikuwa nje nje.
Mpaka leo nikijumlisha matukio ya baadhi niliyokuwa nahadithiwa na wazee wavuvi, na lile la yule Mwandishi, nikisikia kuhusu mauza uza ya Baharini huwa sipingi.
Aah na wewe umekuja?karibu shujaa mimi nawapenda watu wanaokufa kishujaa,aah tu tayari tunainoa midomo yetu kama tai na mikuki yetu inang'aa katika miali ya jua.
Unakikumbuka kipande hicho kara shujaa?
 
Dah...! Leo umechelewa kweli kuja ulikuwa wapi siku nzima? Post bila watu kama wewe hazinogi kabisa!
Jibu unachoulizwa acha ngonjera na usipende kujibu maswali mepesi mepesi tu na mazito kuyavalia Miwani ya Mbao.
 
Duh we noma hilo swali akijibu ajibu na la titanic
Maswali ya hivyo huwa hajibu na hujifanya hayaoni,hujibu maswali ya wale watu ambao kisha washika akili coz vyovyote atakavyowajibu wataitikia tu "Ndio muheshimiwa"
 
Katika hayawani wa mwituni huyu ndio namba moja
Namba moja kwa kitu gani? Weka fact ya wewe kumpa Fisi huo u namba wani kwa ku compare na Wanyama wengine,Weka maelezo ya kiutu uzima acha hadithi za Bed time au za Babu na Wajukuu zake.
 
Maswali ya hivyo huwa hajibu na hujifanya hayaoni,hujibu maswali ya wale watu ambao kisha washika akili coz vyovyote atakavyowajibu wataitikia tu "Ndio muheshimiwa"
Duu bado upo tuu pumua kidogo basi usishindane na forum
 
Namba moja kwa kitu gani? Weka fact ya wewe kumpa Fisi huo u namba wani kwa ku compare na Wanyama wengine,Weka maelezo ya kiutu uzima acha hadithi Bed time.
Shida yako moja unapenda mno kubana pua ni kizalia au maringo??? Hizi nyuzi unaziponda hapa lakini rohoni zinakukuna ndio maana huchoki kuzifuatilia
 
Wenzako wamesha amini hizo Porojo!! Aisee kuna mijitu rahisi sana kuikamata kifikra!! Sijui tatizo ni elimu?!
Usitumie nguvu nyingi basi kijana ujue utakufa siku si zako , usilazimishe watu wakubaliane na mitazamo yako
Ushauri; Anzisha mada za kupinga yale yote ninayoandika uweke facts ambazo sio upuuzi wala porojo
 
Maswali ya hivyo huwa hajibu na hujifanya hayaoni,hujibu maswali ya wale watu ambao kisha washika akili coz vyovyote atakavyowajibu wataitikia tu "Ndio muheshimiwa"
Ha ha haa umeona eee
 
Usitumie nguvu nyingi basi kijana ujue utakufa siku si zako , usilazimishe watu wakubaliane na mitazamo yako
Ushauri; Anzisha mada za kupinga yale yote ninayoandika uweke facts ambazo sio upuuzi wala porojo
Naomba tafsiri ya kumwambia mtu atakufa siku si zake,tuanzie hapo kwanza
 
Umeshindwa kujibu hata swali langu moja tu!! Si umesema watu kama sisi ndio hufanya mada inoge? Au umeshajisahau? Naomba ujibu maswali niliyokuuliza.
 
Back
Top Bottom